Hivi Katiba ya Zanzibar iliandikwa na kupitishwa lini? Ningependa kujuwa hilo.
Mwaka 1984 na kufanyiwa amendments mwaka 2010 (Naweza kusahihishwa kama nimekosea)
Hivi Muungano wetu ulipoasisiwa, hatua hiyo ndiyo iliyohitimisha kwamba Muungano huo umekuwa kamilifu,
Mimi sijasema hivyo.
Hata hivyo, jibu la swali lako ni HAPANA. Kwa sababu Muungano ni makubaliano ya pande mbili au zaidi. Hakuna makubaliano yasiyoweza kufanyiwa marekebisho kwa kadiri mnavyoendelea mbele kuyatekeleza. Mara nyingine makubaliano huvunjika au hufikia ukomo na kila upande ukaenda kivyake.
Upo mkataba wa makubaliano mmoja tu maarufu kama "agano" ambalo ni irreversible. Ni lile kati ya Mungu Muumba na wanadamu. Unalijua?
au ilitegemewa kwamba patakuwepo na hatua kadhaa kuendelea kuurutubisha zaidi?
Obviously, ni hivyo. Soma hapo juu
Mwisho mkuu wangu 'Uzima Tele', isikuwie rahisi sana kuwadharau waTanzania kuwa ni watu wasiokuwa na akili.
Sijadharau mtu tafadhali!
Ila ni kweli kuwa Kwa miongo kadhaa timejengwa ktk misingi ya unafiki na uongo na kuhanganyana kwingi kiasi cha baadhi yetu kuanza kujiita "waheshimiwa" badala ya "ndugu" eti tu Kwa sababu wako kwenye nafasi ya utawala au uongozi fulani.
Huu ni utamaduni mbaya sana. Wakaenda mbali zaidi na kuingiza mambo haya mpaka kwenye mitaala ya shule za watoto wetu.
Ndiyo, kati yetu, na hasa enzi hizi, pamekuwepo na waTanzania wenzetu wengi ambao unafiki na mambo mengi ya hovyo yamekuwa kama ndiyo tamaduni ya nchi hii.
Vyema umelitambua hili. Na hoja yangu iliwahusu wao
Ni Mwalimu huyo huyo aliyehimiza watu wjitambue na wajue haki zao, au umesahau?
Hakuna mahali Mimi au pengine hata Tundu Lissu tunayemjadili hapa amesema Hayati Mwl Nyerere J. K hakufanya mema ktk nchi hii. Alifanya mema mengi na mazuri, and we appreciate them
Lakini pia alifanya mengi mabaya na yaasiyofaa ambayo kizazi chetu na vile vijavyo havipaswi kuyaiga isipokuwa yatumike kama kumbukumbu ya kujifunzia kufanya mema zaidi. Hii ndiyo hoja ya Tundu Lissu nami nakubaliana naye 100%. Kuna ubaya hapo?
Au Kuna shida gani kwani ndugu
Kalamu kusema makosa yaliyofanywa na yanayofanywa na viongozi wetu?
Je, si Kwamba tujifunze ili wengine wasifanye makosa hayo?
Mbona sasa "kukosoana" mnakuita ni kutusiana au kukashifiana? Mna matatizo gani nyie???
Kwa hiyo, unapoona kuna waTanzania wanaoheshimu mambo mengi yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere, ukadhani wamejitoa akili kichwani bila ya kujua sababu za kumuenzi mwasisi huyo wa taifa letu.
Nisome hapo juu.
Kwa lugha rahisi ndugu
Kalamu iko hivi:
Mazuri ya viongozi wetu yaenziwe na kila mtu na makosa na mabaya yao yote tuyapinge na kuyakataa Kwa uwazi bila hofu yote. Ndicho afanyacho Tundu Lissu. Na nakubaliana naye kabisa 100%
Au kusema mabaya na kuwakosoa viongozi wetu kwenu ninyi huko ni mwiko na ni matusi?
USHAURI: Ukitaka kujifanyia mambo yako mwenyewe Kwa namna yoyote na Kwa njia yoyote bila kujali watu, basi huyo mtu awe kiongozi wa familia yake mwenyewe japo hata ndani ya familia kama ana watoto, basi ategemee kukosolewa na kupingwa tu!
Ni heshima iliyo dhati anayoistahili Mwalimu Nyerere katika mambo mengi sana aliyoyafanya katika uhai wake kama kiongozi wa nchi yetu.
Exactly, anastahili heshima
Lakini usisahau kuwa alikuwa mwanadamu. Msikilize Tundu Lissu vizuri kwenye video hiyo tena ili umwelewe.
Mabaya yake lazima yasemwe ili kizazi cha leo na cha kesho kijifunze na kisije kufanya makosa kama yake.
Sasa, tunapotoa heshima hiyo, tafadhali usione kuwa sote ni wanafiki.
Na sisi wengine tunapoonesha mapungufu yake, msituone ni wanafiki vilevile Kwa sababu tunathibitisha ubinadamu wake!!
Au huyu mtu alikuwa Mungu Kwa umbo la binadamu?
Thibitisha ili tumheshimu Kwa masafa hayo. Kama sivyo, basi ni vyema tukubaliane kutokukubaliana!!
Thanx