Lissu ukirudi Tanzania zingatia hili, kumkashifu Baba wa Taifa ni off limits

Nchi hii watu wengi uwezo wenu wa akili na uelewa wa mambo ni mdogo mnoooooo
 
Anayemkashifu Mwl. Nyerere baba wa taifa la Tanzania ni punguwani. Period
 
nyerere ndie rais ovyo sana katuletea azimio la arusha kadhulumu nyumba za watu na kuipa jina NHC watu wamekufa kwa presha kwa kuzulumiwa. kaleta bakwata kuuwa uislamu. kila kaya kupewa dawa ya mswaki 1 kwa kila kaya sukari kilo 1 kwa kila kaya kwa mwezi mnatumia dawa ya mswaki mkiwa mpo 10 kaya moja mtaitumia wote kwa mwezi sukari hivyo hivyo redio kununua kwa kibali sabuni ya kufulia kwa kibali ilikuwa ni shida utawala wake
 
Katika siasa kuna watu wanaitwa reactionaries.
Hawa ndiyo kina Tundu Lissu.

Wanaweza kutibua na kuleta mapungufu ya mfumo fulani.
Lakini hawajui na hawana uwezo wa kuona mbali ya kile wanacho kilaumu.

Tundu Lissu ni fundi wa kulaumu, kukashifu na kutukana.
Lakini hata kule kwao Singida hajui namna ya kuwaendeleza wananchi wa kijijini kwake kwa maisha bora.

Mtupe mfano wa maendeleo kijiji chochote alichokiwakilisha bungeni.
 
Watoto wa 1990.
 

Hili ni doa ambalo haliwezi kufutika. Huwezi kumtukana baba wa taifa. Halafu ubaki salama.
 
Kwa maoni yangu, moja ya legacy za Nyerere ni ile inayotokana na Kumfanya raisi wa Tanganyika(Tanzania) kuwa kama Mfalme/Malkia. Tena wale wa zama za kale, yaani;
  • Asemacho raisi ndio sheria (katiba/no katiba).
  • Hapingiki
  • Hakosolewi
  • Yeye ni mtukufu (noble) .nk

Hivyo sishangai kabisa, mfumo wa fikra za mtoa maada. Ni legacy ya anaeitwa Baba wa Taifa.
 
Hatuhangaika na waliokufa
 
Popote Nyerere alipokosea lazima isemwe waziwazi bila ya kumung'unya maneno, kwa sababu gani watu waogope kuyasema yale aliyokosea?
Kama yakisemwa na wale wenye upeo mdogo au wale waliogubikwa na mahaba kwake wakaanza kuchukulia kuwa kukosoa alipokosea ni kashfa hiyo itakuwa ni matatizo yao wenyewe.
 
Ninakubaliana nawe, ila sioni sababu tena ya kumrudisha ulaya, labda apende mwenyewe, na kwa kweli ningependa yeye ndiye awe mstari wa mbele kuhakikisha kwamba waTanzania, kwa sababu yoyote ile hawalazimishwi kukimbilia kokote bila ya utashi wao.

Juu ya kumkashifu Mwalimu, natumaini yeye mwenyewe Lissu anatambua kwamba ajenda hiyo haimwongezei chochote, na wala haikijengi chama chake.

Kuzungumzia maswala ya wakati wa Mwalimu, na kuyaleta katika nyakati za leo sioni kuwa zinamjengea heshima mahali popote.

Hata hivyo, akipenda kupigana mieleka na 'legacy' ya Mwalimu kwa wakati huu, sina shaka yoyote kwamba ataangukia pua kwa aibu sana, kwa sababu maswala aliyoyasimamia Mwalimu hadi leo yana maana kubwa sana katika uhai wa waTanzania na heshima kubwa ya nchi yao.

Lakini inanibidi niulize swali: kwani tofauti kuu iliyopo kati ya mambo anayoyasimamia Lissu na yale aliyoyaamini na kuyasimamia Mwalimu ni ipi hasa? Ningependa kujua hili.

Kwa maana, uelewa wangu kuhusu Lissu ni kwamba ni mpigania haki za watu. Kachaniwa magwanda na polisi na kubaki na 'singlet' kule Mara, akiwa kwenye harakati za kupigania HAKI za waTanzania.

Sasa ni kipi hasa anachotofautiana na Mwalimu? Ujamaa; au namna ya utekelezaji wa baadhi ya mambo kwa wakati ule wa Mwalimu, ambao pengine leo hii hata Mwalimu angetekeleza kileo kuliko kijuzi.

Karibu sana nyumbani 'Ndugu' Lissu.
 
Mwalimu alivikuta vyama vingi nchini, kulikuwa na vyama vingi tangu enzi za ukoloni.
Vingapi?
Mi nakijua cha Mtemvu, vingine ni vipi?
Hata hicho cha Mtemvu kiliundwa kwa mbinde wa wakoloni kutafuta njia za kuififisha TANU..

Nasubiri hilo jibu la vyama vingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…