Lissu ukitufafanunulia kuhusu ushirika wako na Mbowe katika kumsafisha Lowassa utaeleweka sana

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Hellow Tanganyika!!

Katika mengi umejaribu kujitofautisha na mkt wako Ili kupata uungwaji mkono wananchi na wanachama,na umefanikiwa sana katika hili.

Sasa Kuna kihunzi Cha mwisho Cha kukiruka Ili urudishe Imani ya wananchi iliyoondoka baada ya ujio wa Lowwassa, mliotuambia kuwa ni fisadi mkishirikiana na Mh Mbowe. Baadae alipoingia CDM mkashirikiana kumsafisha.

Swali No 1:
Mh Lissu, Lowwassa alikuwa fisadi au la?

Swali No 2.
Kwanini ulikaa upande wa Mh Mbowe kumsafisha Lowwassa, kwanini hukukaa kimya kama Ndugu Mnyika?

Swali no 3.
Kuna mgao wowote nawe ulipokea katika ujio wa Lowwassa maana inaaminika kuwa alikuja na mapesa mingi?

Karibu Kwa majibu πŸ™
 
Too late , hana muda huo na hawajibiki kufafanua hilo maana si sera ya uchaguzi wa ndani
 
Maana ujio wa Lowwassa CDM Kwa kiasi kikubwa uliondoa uwwzekano wa CHADEMA kushinda uchaguzi.
 
Lissu huna haja kujibu hoja dhaifu wajumbe wako tayari kupigia kura tarehe 21 kanyaga twende. Uliyokwisha sema yanatosha wajumbe wamekuelewa na jana Nabii Lemma kahitimisha.
 
Lissu huna haja kujibu hoja dhaifu wajumbe wako tayari kupigia kura tarehe 21 kanyaga twende. Uliyokwisha sema yanatosha wajumbe wamekuelewa na jana Nabii Lemma kahitimisha.
Amalizie kujibu swali hili tu la mwisho, ni muhimu mnoπŸ™
 
Ninyi mnaofanya mahojiano na Lissu, muulizeni swali hili tafadhali πŸ™
 
You're too Naive.
 
Muda ukienda sana hata uzito linakosa, na linakuwa irrelevant. Kuna time na muda sahihi wa kuuliza such things, huo muda haupo tena
Sasa ukiona unaulizwa swali Hilo Hilo baada ya kujibu, jiulize,

Yaezakuwa swali halijajibiwa ipasavyo hivyo kiu haijakatwa.
 
Sasa ukiona unaulizwa swali Hilo Hilo baada ya kujibu, jiulize,

Yaezakuwa swali halijajibiwa ipasavyo hivyo kiu haijakatwa.
Kuna muda na wakati, huo muda sio sasa, na halizimiki kujibu. Subiri uchaguzi uishe
 
Mjiulize nyie pia baada ya kurudi mkampokea tena baada ya kumuita fisadi
 
Wewe si mfuatiliaji sana ameshalijibu hilo swali several times.
Alijibuje?

Ikiwa alisema ni maamuzi ya vikao vya chama.

Basi hajaeleweka, na ni muhusika wa kupunguza Imani ya wananchi Kwa CHADEMA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…