Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Wengi hawajui Kiswahili wala Kiingereza ambazo ni lugha rasmi za taifa.

Hili ni tatizo na siyo sawa kwa wananchi kutoweza kuongea na kuandika lugha rasmi za taifa lao kwa ufasaha.

Ni muhimu kwa viongozi, waandishi, watangazaji na jamii kwa ujumla kujifunza kwa bidii badala ya kutoa utetezi wa kijinga.
 
Wewe shida yako sio lugha, ni ama u-mvivu wa kusoma au mgumu wa kuelewa! Kha, humu JF kuna watu wa ajabu!!
 
Kwahiyo hayo maendeleo ambayo anasema atawaletea watu kumbe ilikuwa anamaanisha kuongea kingereza vizuri??

Daah Chadema mmetuletea mtu wa aina gani??
Hivi mmeelewa alicho maanisha Lissu au?
Mbona mataga mna behave kama mmechomekwa cable, yaani wote akili zinafanana!!
 
Nadhani we ndo huna akili
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Kwa uelewa huu bado tuna kazi ndefu kama taifa.
 
Slavery Mentality!! Ilishasemwa karne ya 17 na mzungu Lord Macaulay huyu hapa!! Wakati mwingine nafikiri Lissu ameshaathirika kwenye ubongo wake kuna uwezekano hao Wabelgiji watakuwa wamemharibu kiakili!!

Mkuu hicho ndio kitu hasa ninachouliza hapa tukiwa Kama jukwaa huru tuanze kwanza sisi kujibu haya maswali .
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Unajua kuwa sheria zetu na hata hukumu zetu ni English tupu ?! Barua zetu za ki serikali na mawasiliano na dunia ni only in English !!
 
Mkuu hicho ndio kitu hasa ninachouliza hapa tukiwa Kama jukwaa huru tuanze kwanza sisi kujibu haya maswali .

..najua kwamba umejaribu kuchokoza mada.

..ushauri wangu ni kwamba sikiliza hiyo interview kati ya Jenerali Ulimwengu, Richard Mabala, na Prof.Margareth Qorro.

..ukimaliza kuisikiliza naamini utakuwa uko well equiped kuchangia mada ambayo umeichokoza.
 
Lissu ameongea vizuri sana. Ila nashangaa wanaopinga bila hoja ya msingi.
 
Kwahiyo hayo maendeleo ambayo anasema atawaletea watu kumbe ilikuwa anamaanisha kuongea kingereza vizuri??

Daah Chadema mmetuletea mtu wa aina gani??
Kujua namna ya kujieleza ndio ni maendeleo. leo hii Magufuli hawezi kujieleza badala yake anakimbilia kupiga push up, Mkiambiwa tatzo ni mfumo mnajitoa ufaham.mmekua Watu wa kusema ndio/hapana
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Kwani kama hujaisoma "thread" ni lazima uchangie. Sasa "thread" imewekwa Kiswahili nayo huwezi kusoma humu unatafuta nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…