Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Wengi hawajui Kiswahili wala Kiingereza ambazo ni lugha rasmi za taifa.

Hili ni tatizo na siyo sawa kwa wananchi kutoweza kuongea na kuandika lugha rasmi za taifa lao kwa ufasaha.

Ni muhimu kwa viongozi, waandishi, watangazaji na jamii kwa ujumla kujifunza kwa bidii badala ya kutoa utetezi wa kijinga.
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu
Wewe shida yako sio lugha, ni ama u-mvivu wa kusoma au mgumu wa kuelewa! Kha, humu JF kuna watu wa ajabu!!
 
Kwahiyo hayo maendeleo ambayo anasema atawaletea watu kumbe ilikuwa anamaanisha kuongea kingereza vizuri??

Daah Chadema mmetuletea mtu wa aina gani??
Hivi mmeelewa alicho maanisha Lissu au?
Mbona mataga mna behave kama mmechomekwa cable, yaani wote akili zinafanana!!
 
Tundu Lissu asitufanye wajinga kiasi hicho. China wanajua kiingereza?????? Ujinga mtupu wala hatupotezi muda na mjiinga huyo, ajenda yetu kwa sasa ni kukiweka kiswahili lugha ya Kwanza Afrika halafu yeye anatuletea upupu.We want to make Tanzania great nation,kiswahili ni ajenda kuu
Nadhani we ndo huna akili
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Kwa uelewa huu bado tuna kazi ndefu kama taifa.
 
Tundu Lissu amesema haya kuhusu lugha ya kufundishia

Ukiniuliza mimi, honest opinion Nchi yetu haiwezi kuzungumza Kiingereza, hivyo tunahitaji kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha, tusipokuwa na mjadala huu, hatufiki popote kwani language of instruction is everything.

Mimi ni Wakili, Majaji wengi hawajui kiingereza, ukienda Nchi za wenzetu huko Mtanzania akiongea unatamani kuingia uvunguni mwa meza, Kiingereza chetu ni kibaya, sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha.

Tangu tumepata Uhuru tumekua na ndimi mbili kuhusiana na lugha na ndimi mbili ni hatari, ulimi mmoja tumesema Kiswahili ni lugha ya Taifa na tumeiendeleza kwelikweli, ulimi wa pili tumesema Kiswahili si lugha ya kufundishia.

Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.
Slavery Mentality!! Ilishasemwa karne ya 17 na mzungu Lord Macaulay huyu hapa!! Wakati mwingine nafikiri Lissu ameshaathirika kwenye ubongo wake kuna uwezekano hao Wabelgiji watakuwa wamemharibu kiakili!!

IMG-20200608-WA0007.jpg
 
..TL amesema kutakuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu lugha inayofaa kufundishia.

..Yeye hajatupa karata yake kwamba twende na Kiswahili, au twende na Kiingereza.

..ukipata muda sikiliza hawa wataalamu wa lugha na waalimu wa muda mrefu hapa chini.

Mkuu hicho ndio kitu hasa ninachouliza hapa tukiwa Kama jukwaa huru tuanze kwanza sisi kujibu haya maswali .
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Unajua kuwa sheria zetu na hata hukumu zetu ni English tupu ?! Barua zetu za ki serikali na mawasiliano na dunia ni only in English !!
 
Mkuu hicho ndio kitu hasa ninachouliza hapa tukiwa Kama jukwaa huru tuanze kwanza sisi kujibu haya maswali .

..najua kwamba umejaribu kuchokoza mada.

..ushauri wangu ni kwamba sikiliza hiyo interview kati ya Jenerali Ulimwengu, Richard Mabala, na Prof.Margareth Qorro.

..ukimaliza kuisikiliza naamini utakuwa uko well equiped kuchangia mada ambayo umeichokoza.
 
Lissu ameongea vizuri sana. Ila nashangaa wanaopinga bila hoja ya msingi.
 
Kwahiyo hayo maendeleo ambayo anasema atawaletea watu kumbe ilikuwa anamaanisha kuongea kingereza vizuri??

Daah Chadema mmetuletea mtu wa aina gani??
Kujua namna ya kujieleza ndio ni maendeleo. leo hii Magufuli hawezi kujieleza badala yake anakimbilia kupiga push up, Mkiambiwa tatzo ni mfumo mnajitoa ufaham.mmekua Watu wa kusema ndio/hapana
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Kwani kama hujaisoma "thread" ni lazima uchangie. Sasa "thread" imewekwa Kiswahili nayo huwezi kusoma humu unatafuta nini!
 
Back
Top Bottom