List ya wasanii wa Bongo ambao walipata umaarufu na mafanikio makubwa, lakini leo wako juu ya mawe

List ya wasanii wa Bongo ambao walipata umaarufu na mafanikio makubwa, lakini leo wako juu ya mawe

1) Mr Nice - huyu Afrika mashariki nzima na baadhi ya nchi za kusini kama vile Malawi, Msumbiji na Zambia hakuna mtu ambae alikuwa hamjui. Mpaka watoto wadogo huko vijijini Malawi walikuwa wanaimba kidali poo. Miaka ya 2002 mpaka 2005 alipiga hela sana lakini akaishia kushusha zipu, leo hii anazurura tu mitaani hana mbele wala nyuma.

2) Ferouz - Nyimbo kama kamanda, barua, kwaherini aliyoimba na prof Jay zilimpa umaarufu mkubwa hadi kupelekea kutunzwa gari na aliekuwa raisi wa JMT wa wakati huo hayati Benjamin W Mkapa. Na yeye alishika sana hela enzi hizo. Lakini leo inasemekana mambo yake yamekwenda ndivyo sivyo kwahiyo ni kama vile ashapoteza

3) 20 Percent - Huyu nae alikuja vizuri japo kwa muda mchache. Alikuja na vibao vyake matata na ile style yake ya kukwaruza kwaruza sauti huku mistari akiwa kaipangilia vilivyo, pia ukijulimsha na movie yake iliyovunja rekodi. Akaendekeza endekeza mjani na togwa. Leo hii inasemekana ukikutana nae mtaani lazima akupige mkuki umuunge buku akanywe chai.

Wapo wengi lakini acha niwataje hawa wengine mtaongezea wenyewe wasanii waliopata umaarufu na mwisho kupaki juu ya mawe kama gari isiokuwa na matairi.
🤣🤣🤣 daah ulivowaelezea hao jamaa daaah...umewaelezea katika funny ways sasa mtu unabaki ucheke au upate huruma
 
Kwanza nkusahihishe

Ferooz hakuwahi kupewa zawadi ya gari na Mkapa ...Kipindi ngoma ya starehe imepata umaarufu , Ferooz album yake ya Safari ilifanya vizuri sana na kupelekea kupata fedha nyingi ndo akajinunulia ile gari ya Jeep
Oh kumbe haikuwa ya kwake. Mbona taarifa ilisambaa kuwa raisi Mkapa alimpa kutokana na ule wimbo wake ambao ulihamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi!!
 
Kweli FA anaonekana yupo vizuri muda wote wa maisha yake ya mziki.

Hakuwahi kufulia na kupiga watu mikuki kama wengine.
Inaonekana maisha huyajui alafu hujawahi pitia msoto mtu kukuomba hela ana shida ni kawaida usimuhukumu unakosea sana kuwaona ni wajinga na hawana akili

Assume unakamata let say million 30 au 50 kwa miaka ile alafu una miaka 20's na umetokea mazingira duni a.k.a uswahili acha kukufuru na usijione mkamilifu

Mim wasanii ambao wakati mgumu siwez walaumu that's life bro shit happen
 
Kweli FA anaonekana yupo vizuri muda wote wa maisha yake ya mziki.

Hakuwahi kufulia na kupiga watu mikuki kama wengine.
Ishu hapo ni Maadili FA na AY ni watu wanaonekana walilelewa kwenye misingi ya maadili mema kwahiyo ni watu ambao sio wa starehe na shobo! Wanaishi maisha yao!
Kuna kanuni za kiulimwengu ukizifuata na kutokua na papara na maisha lazima utoboe
 
Swala sio maadili ni basi wamshukuru Mungu mambo mengine sio ya kujisifu sana
 
Inaonekana maisha huyajui alafu hujawahi pitia msoto mtu kukuomba hela ana shida ni kawaida usimuhukumu unakosea sana kuwaona ni wajinga na hawana akili

Assume unakamata let say million 30 au 50 kwa miaka ile alafu una miaka 20's na umetokea mazingira duni a.k.a uswahili acha kukufuru na usijione mkamilifu

Mim wasanii ambao wakati mgumu siwez walaumu that's life bro shit happen
Sifurahii kuanguka kwao mkuu, ila nazungumzia jinsi walishindwa kutengeneza mazingira ya kujisimamia vizuri kimaisha.

Sio wote walioanguka kwa changamoto za maisha, wengi ni wale walioendekeza ulevi, uteja na chupi.
 
🤣🤣🤣 daah ulivowaelezea hao jamaa daaah...umewaelezea katika funny ways sasa mtu unabaki ucheke au upate huruma
Comment yako imenichekesha sana😂😂😂
 
Ishu hapo ni Maadili FA na AY ni watu wanaonekana walilelewa kwenye misingi ya maadili mema kwahiyo ni watu ambao sio wa starehe na shobo! Wanaishi maisha yao!
Kuna kanuni za kiulimwengu ukizifuata na kutokua na papara na maisha lazima utoboe
Ulichoandika kina make sense na kinaeleweka vizuri mkuu. Ni kama funzo fulan ambalo mtu akijifunza litamsaidia.
 
Ulichoandika kina make sense na kinaeleweka vizuri mkuu. Ni kama funzo fulan ambalo mtu akijifunza litamsaidia.
Kabisa mkuu huwa kuna maisha ya watu wengine lazima yatumike kama funzo.hiyo ndo iko hivo ni moja ya kanuni ya kuishi duniani.Sasa nashangaa wengine wanaposema eti unawadharau..hapana upo sahihi kabisa. Na nadhani wanamziki wa sasa wengi wanawekeza kutokana na mafunzo toka kwa waliowatangulia.

So big up! Hata huku mtaani maisha yetu tunaishi kwa kujifunza toka kwa wengine.

Mfano vijana wa sasa wanamziki wanajifunza sana kutoka kwa Diamond nae diamondi alishajifunza huko toka kwa waliomtangulia. Ni maisha ya kawaida kabisa
 
Back
Top Bottom