Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤣🤣🤣 daah ulivowaelezea hao jamaa daaah...umewaelezea katika funny ways sasa mtu unabaki ucheke au upate huruma1) Mr Nice - huyu Afrika mashariki nzima na baadhi ya nchi za kusini kama vile Malawi, Msumbiji na Zambia hakuna mtu ambae alikuwa hamjui. Mpaka watoto wadogo huko vijijini Malawi walikuwa wanaimba kidali poo. Miaka ya 2002 mpaka 2005 alipiga hela sana lakini akaishia kushusha zipu, leo hii anazurura tu mitaani hana mbele wala nyuma.
2) Ferouz - Nyimbo kama kamanda, barua, kwaherini aliyoimba na prof Jay zilimpa umaarufu mkubwa hadi kupelekea kutunzwa gari na aliekuwa raisi wa JMT wa wakati huo hayati Benjamin W Mkapa. Na yeye alishika sana hela enzi hizo. Lakini leo inasemekana mambo yake yamekwenda ndivyo sivyo kwahiyo ni kama vile ashapoteza
3) 20 Percent - Huyu nae alikuja vizuri japo kwa muda mchache. Alikuja na vibao vyake matata na ile style yake ya kukwaruza kwaruza sauti huku mistari akiwa kaipangilia vilivyo, pia ukijulimsha na movie yake iliyovunja rekodi. Akaendekeza endekeza mjani na togwa. Leo hii inasemekana ukikutana nae mtaani lazima akupige mkuki umuunge buku akanywe chai.
Wapo wengi lakini acha niwataje hawa wengine mtaongezea wenyewe wasanii waliopata umaarufu na mwisho kupaki juu ya mawe kama gari isiokuwa na matairi.
Daah we jamaa unachekesha sana 🤣🤣🤣Chid ukikutana nae usimuangalie mara mbili lazima aombe umuungie za mihogo.
MwanzaWapi hiyo 😂😂
Oh kumbe haikuwa ya kwake. Mbona taarifa ilisambaa kuwa raisi Mkapa alimpa kutokana na ule wimbo wake ambao ulihamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi!!Kwanza nkusahihishe
Ferooz hakuwahi kupewa zawadi ya gari na Mkapa ...Kipindi ngoma ya starehe imepata umaarufu , Ferooz album yake ya Safari ilifanya vizuri sana na kupelekea kupata fedha nyingi ndo akajinunulia ile gari ya Jeep
Inaonekana maisha huyajui alafu hujawahi pitia msoto mtu kukuomba hela ana shida ni kawaida usimuhukumu unakosea sana kuwaona ni wajinga na hawana akiliKweli FA anaonekana yupo vizuri muda wote wa maisha yake ya mziki.
Hakuwahi kufulia na kupiga watu mikuki kama wengine.
Ishu hapo ni Maadili FA na AY ni watu wanaonekana walilelewa kwenye misingi ya maadili mema kwahiyo ni watu ambao sio wa starehe na shobo! Wanaishi maisha yao!Kweli FA anaonekana yupo vizuri muda wote wa maisha yake ya mziki.
Hakuwahi kufulia na kupiga watu mikuki kama wengine.
Ni mtoto alafu ana dharau sana ukishaona mwanaume ana mdharau mwanaume mwenzake yuko kwenye msoto ujue hapo hamna mtuDaah we jamaa unachekesha sana 🤣🤣🤣
Swala sio maadili ni basi wamshukuru Mungu mambo mengine sio ya kujisifu sanaIshu hapo ni Maadili FA na AY ni watu wanaonekana walilelewa kwenye misingi ya maadili mema kwahiyo ni watu ambao sio wa starehe na shobo! Wanaishi maisha yao!
Kuna kanuni za kiulimwengu ukizifuata na kutokua na papara na maisha lazima utoboe
Sifurahii kuanguka kwao mkuu, ila nazungumzia jinsi walishindwa kutengeneza mazingira ya kujisimamia vizuri kimaisha.Inaonekana maisha huyajui alafu hujawahi pitia msoto mtu kukuomba hela ana shida ni kawaida usimuhukumu unakosea sana kuwaona ni wajinga na hawana akili
Assume unakamata let say million 30 au 50 kwa miaka ile alafu una miaka 20's na umetokea mazingira duni a.k.a uswahili acha kukufuru na usijione mkamilifu
Mim wasanii ambao wakati mgumu siwez walaumu that's life bro shit happen
Ulichoandika kina make sense na kinaeleweka vizuri mkuu. Ni kama funzo fulan ambalo mtu akijifunza litamsaidia.Ishu hapo ni Maadili FA na AY ni watu wanaonekana walilelewa kwenye misingi ya maadili mema kwahiyo ni watu ambao sio wa starehe na shobo! Wanaishi maisha yao!
Kuna kanuni za kiulimwengu ukizifuata na kutokua na papara na maisha lazima utoboe
Kabisa mkuu huwa kuna maisha ya watu wengine lazima yatumike kama funzo.hiyo ndo iko hivo ni moja ya kanuni ya kuishi duniani.Sasa nashangaa wengine wanaposema eti unawadharau..hapana upo sahihi kabisa. Na nadhani wanamziki wa sasa wengi wanawekeza kutokana na mafunzo toka kwa waliowatangulia.Ulichoandika kina make sense na kinaeleweka vizuri mkuu. Ni kama funzo fulan ambalo mtu akijifunza litamsaidia.