Low IQ Tanzania, wanafurahia Polisi kuondolewa barabarani!

Trafiki wetu siyo waadilifu, wanalalamikiwa kwa kutofanya kazi zao scientifically, rushwa kwanza mengine baadaye
Trafiki polisi Tanzania ni kero kubwa. Lakini hii haihalalishi mwanasiasa mzee aliyekwisha kaa kwenye uongozi mpaka akapitiliza muda wake, na ambaye ni mmoja ya watu waliotengeneza hilo tatizo, kujaribu kutoa solution kwa tamko la jukwaani. Haya mambo yafanyike kitaalam!
 
Trafiki wetu siyo waadilifu, wanalalamikiwa kwa kutofanya kazi zao scientifically, rushwa kwanza mengine baadaye
Lakini mada imehama kutoka rushwa kuwa kuondolewa.
Chonde chonde IGP na makamishina wako, msiwaondoe matrafiki. Maskini wa nchi hii ndio watakufa. Kinana na wanasiasa wengine wana magari binafsi. Hawategemei order of public transport.
 
Tatuzo sio JPM kufa au kufufuka tatizo ni ccm tangu tumepata Uhuru wameshindwa kujenga miundo mbinu kutaka madalakani awataki matoke yake nchi mzima kero tupu
''Seen and endosed''. Asante. Mimi msimamo wangu huu hapa: ''Trafiki polisi Tanzania ni kero kubwa. Lakini hii haihalalishi mwanasiasa mzee aliyekwisha kaa kwenye uongozi mpaka akapitiliza muda wake, na ambaye ni mmoja ya watu waliotengeneza hilo tatizo, kujaribu kutoa solution kwa tamko la jukwaani. Haya mambo yafanyike kitaalam!''
 
Lakini mada imehama kutoka rushwa kuwa kuondolewa.
Chonde chonde IGP na makamishina wako, msiwaondoe matrafiki. Maskini wa nchi hii ndio watakufa. Kinana na wanasiasa wengine wana magari binafsi. Hawategemei order of public transport.
Traffic wanahaha hivi sasa maji shingoni
Tuwekeze kwenye teknolojia siyo watu kuacha kulinda raia na mali zao
 
Naomba nitofautiane na wewe,Kati ya Kinana na Polisi nani Wana taaluma ya ulinzi na Usalama?

Tutakuwa na Polisi wapumbavu kama watafuata ushauri ambao kwao wanaona sio sawa..
 
Nilazima watu wawajibike kwakutokuwa na mipango ya muda mrefu

Wasio na hatia pay the ultimate price- their lives.

Bongo bila traffic ni fungulia mbwa.
 
Polisi hawajawahi zuia ajali....

Polisi wajiwekeze kwenye technolojia, waweke Camera na Speed Radars, mapato yataongezeka maradufu maana utawekewa angalizo na usipotii camera zitanasa gari lako na kukubill...
Waanze pilot study kwa Jiji la Dsm, wilaya 1 tu, afu ndo wasambazo nchi nzima...
 
Hizi ajali zote zinazotokea Trafiki hawakutosha? Suluhisho la ajali barabarani ni mwendokasi kuwe na vidhibiti mwendo au abiria wawe wanamdhibiti dereva. Pia barabara ziwe angalau na upana unaotosha na sio kujaza trafiki.
Kwenye ubora wa magari na matairi, magari mengi yamezingatia...
Tatizo ni miundo mbinu, barabara zinaviraka sana, nyingine unakuta zimetobolewa tayari
 
Reactions: Tsh

Haikatazwi kutoa maoni
We umetoa maoni nayeye ametoa maoni.
 
Hujaelewa, hawajasema wondoke, alimaanisha polisi wamezidi, kutoka Kawe hadi KKOO unakutana na Polisi mara 6

Huko Iringa ni hatari
 
Mkuu hili swala nilishawahi kulianzishia na ka Uzi kabisa humu
 
Tangu hilo tamko litoke ndio nasoma post ya mtu anaefikiri zaidi ya urefu wa pua. Watz wana unafiki sana. Mtu anaendeshwa na msafara unaopita wrong side,asiejali watumiaji wengine analalamika wingi wa trafiki, huyu hawatakii mema
 
Polisi watoke njiani

Camera na Speed Radar ziongezwe

Mfumo wa usajili magari, namba ya mwenye gari iwepo ili Speed Radar ikidaka overspeed, mwenye gari anatumiwa details ie location, control number

Faini ya overspeed iwe kubwa watu wataheshimu sheria tu, hapo hawatakuwa na njia ya bargain maana hajadakwa na mtu
 
Kwani wabongo wanatofauti gani raia wa nchi zingine?

Hutujui wabongo sio? Wabongo hatuendi bila fimbo waafrika kwa ujumla esp watanganyika.

Ustaarabu, utaratibu, kufuata sheria bila shurti sio utamaduni wetu ipo wazi wala tusiume maneno.

Hii ishu ita-backfire tu huwezi mpa mbongo uhuru asikufurahishe.
 
Polisi hawana msaada, ziwekwe speed radars, camera hii itasaidia sana maana watu watafata sheria, faini kwa speeding iwe kubwa hata 100,000 na hapo utaletewa tu taarifa yenye control number ambapo utapewa siku za kulipa.

Speed radars auto ni ngumu kwa mtu kuanza lia apunguziwe
 
Ajali za barabarani Tanzania zinachangiwa zaidi na hali ya miondombinu ya barabarani.
Tunahitaji double roads.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…