Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Kwani unaona maendeleo ya Tanzania yanafanana na Tanzania? Unafahamu bandari tu ya Dar inaweza walisha wanyarwanda?Rwanda ina Rasilimali kama za nchi yako?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani unaona maendeleo ya Tanzania yanafanana na Tanzania? Unafahamu bandari tu ya Dar inaweza walisha wanyarwanda?Rwanda ina Rasilimali kama za nchi yako?
Maendeleo ya Tanzania hayafanani na Tanzania yenye rasilimali aina zote plus ardhi yenye rutubaKwani unaona maendeleo ya Tanzania yanafanana na Tanzania? Unafahamu bandari tu ya Dar inaweza walisha wanyarwanda?
Huyo @ephen na mumewe wote vichwa maji.Na Wewe Ephen unakurupuka na kujichanganya sijui ni mihemuko au? Niliomba maoni ya Lucas na yeye akaja na maneno mengi yenye kujichanganya mpaka anamtaja na Samia.
Kwa sababu kamtaja na Rais Samia huyo unayemtetea, kwa kuwa anamtaja Rais atusaidie kutuchambulia hii Mikataba aliyeiingia Rais imetusaidia nini Watanzania?
1. Waarabu wa familia ya kifalme Dubai, (DP WORLD) wamepewa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa mikataba ya kiduanzi unaotajwa miaka thelathini
2. Waarabu wa familia ya kifalme ya Dubai (Blue Carbon LLC) wamepewa kusimamia na kuhifadhi misitu ya Tanzania. Hii ni hekta milioni 8.1 (8% ya ardhi yote)
3. Watu wa Korea Kusini wamekabidhiwa kipande cha bahari ya Hindi na ardhi wachimbe madini nadra. Ajabu, hawa na mkopo wametoa na TUTALIPA na riba
4. Watu wa Australia (URANEX) wamepewa ardhi nzuri wachimbe madini nadra ya kimkakati na graphite Mkoa wa Lindi. Kampuni zao tatu zitauza madini nje
5. Watu wa Canada (BARRICK GOLD) wanaondoka na dhahabu. Hawajajenga hata smelters moja. Wanaacha mashimo na watu wetu kupigwa risasi
6. Waarabu wa familia ya kifalme Dubai (OBC) wao wameongezewa 1,500km² kutoka 4,000km² zilizokuwa kwa Maasai ambao wamebaki na 2,500km²
7. Watu wa Netherlands (SHELL) na Norway (EQUINOR) wamepewa kuchimba gesi asilia eneo la bahari kuu kusini mwa Tanzania, eneo la Likong’o Lindi
8. Waarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wamepewa kuendesha huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Dar es Salaam.
9. Watu wa France, Maurel & Prom Exploration Production (T) Ltd. (MPEP) wamenunua hisa kitalu cha uzalishaji wa gesi asilia cha Mnazi Bay, Mtwara.
10. Kandarasi ujenzi Bwawa la Nyerere (JNHPP) kapewa Egypt. Kandarasi ya ujenzi wa SGR kapewa China na Turkey. Waswahili mtapewa Kanda Bongoman.
NB; Umepewa nini wewe? Unaendelea kuwa admin wa kundi la WhatsApp, kuwatishia watu na ‘remove button’ wanaokosoa serikali? Shensisana. Zoea hiyo sauti
Martin Maranja Masese, MMM.
Unategemea PS ataelewa kilichoandikwa hapo?"If the owners of the natural resources go around begging, then you should know there's something wrong with their minds”
View attachment 3009379
Sababu ya kuongozwa na majangili ya mali za ummaMaendeleo ya Tanzania hayafanani na Tanzania yenye rasilimali aina zote plus ardhi yenye rutuba
😂Wanabubujikwa na machozi ya furaha.Acha dharau zako wewe. Mimi nimepiga shule sana na nilikuwa kinara wa kuongea kizunguu kwenye mijadala shuleni mpaka wanafunzi wanashangilia kwa kelele za shangwe huku wanabubujikwa na machozi ya furaha.
Hawa UWT ni wajinga haswaHapo hawezi kukomenti chochote as anafurahishwa na hali ya Mama wa Taifa kwenda kukopa na kuweka rehani Rasilimali zetu za Nchi
Wakishapewa Ujira wao wa buku 7 basi uwezo wao wa kufikiria kuhusu hatima ya Nchi yetu miaka 50 ijayo wanakuwa hawana Tena 🙌
Kwa upumbavu kabisa tunapiga makofi na kushangilia, asee inauma snWafrika kinachotusumbua ni akili za watawala wetu
Hatuwezi tukawa na rasilimali zote
Anakuja mtu anavuna anapeleka kwao alafu anakuja tena kutuuzia
Vifaa nk,kwa mali iliyotoka kwetu wenyewe
Ova
Siku atakapomweka rehani Lucas Mwashambwa Ili tupate mkopo ndo itakuwa poaCCM Hoyee
Mwenye Rasilimali Anasafiri Kuombaomba Haa
Lumumba Buku Saba FC Hatutaweka Comment Popote Kwenye Thread Hii
Rasilimali zetu zipo katika mikono salama ya Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, MZALENDO WA KWELIKWELI kwa Taifa letu.Siku atakapomweka rehani Lucas Mwashambwa Ili tupate mkopo ndo itakuwa poa
Siyo Rasilimali za asili pekee unazomiliki ndio zinakufanya uwe tajiri.bali inahitaji akili ,pesa, teknolojia,maarifa na ujuzi wa watu wako unaotokana na kupata Elimu bora na ya viwango vikubwa.
Embu fikiria hata kama una gesi asilia lakini huna pesa, wataalamu wenye ujuzi na uzoefu, teknolojia na mengine mengi ni vipi utavuma gesi hiyo?
Hiyo ndio sababu ya viongozi wenye Akili kubwa ,maarifa na maono makubwa aina ya Daktari Samia Suluhu Hasssan hutumia akili kutafuta pesa kwa njia mbalimbali kama ya mikopo nafuu kabisa isiyo na athari wala maumivu kwa walipakodi na mali na utajiri wa Taifa letu.
Lakini pia kuna masuala ya ubia kati ya serikali na Secta binafsi kama ambavyo hufanyika hapa Nchini na njia nyingine mbalimbali zinazokubalika na zenye maslahi kwa Taifa letu.
Angalia hata Mheshimiwa Paul Kagame yeye na Nchi yake wanadaiwa shilingi ngapi kutoka mataifa ya nje,taasisi za kifedha na mashirika mbalimbali ya kifedha kutoka maeneo mbalimbali Duniani?
Mtoa ujumbe mwenyewe huyo anamadeni kibao sana Nchini kwake. Muulizeni kwanini alikopa na kuomba msaada?
Baadaye akija Kiongozi mwingine, wanageuka tena kumsema huyu aliyepo, wakati walikuwa na nafasi ya kumshauriHawa UWT ni wajinga haswa
Kumbe una akili nyingi sana ukituliaga vizuri chini na kuandika. Bonge moja la Comment . Nimefurahi sana majibu na andiko lako hili. Japo huwa tunakwaruzana mara kwa mara ila leo umenikosha na wala sina nyongeza .Huu ndio upinzani naoupenda mimi. Upinzani wa hoja.ambao mtu akiandika hoja kama ulivyofanya wewe mpaka mwingine unaona aibu kupinga ukweli huo.Kama ni mtihani, hapo Mwashambwa umejitahidi. Umepata 70%.
Jibu sahihi hapo ni moja tu, na umeliweka kwenye majibu yako. Ungepata 100% ila umeharibu kwa kuongeza mengine yasiyo sahihi.
Rasilimali kubwa inayoweza kukufanya umudu mazingira yako iwe kiuchumi, kitekinolojia, kielimu na hata maarifa, ni AKILI. Siyo mikia ya fisi, siyo madini, gesi, mito na maziwa yenye maji mazuri, mafuta au ardhi nzuri ya kilimo. Ila ukiwa na AKILI, halafu ukajaaliwa kuwa na rasilimali asilia, hakika unapaa kimaendeleo. Ukiwa huna akili, ukajaaliwa kuwa na mito mingi, utaanza kulalamika na kuona mito ni kero kwa sababu huna uwezo wa kujenga madaraja. Utaanza kulalamikia mawe yenye madini ni kero kwa sababu milima ya mawe inakufanya ushindwe kutengeneza barabara nzuri, utalalamikia uwepo wa wanyama pori kwa sababu wanakula mbuzi wako na wanaua wananchi, kwa vile tu wananchi wako, hawana makazi bora na salama.
Switzerland hawana rasilimali asilia karibia zote lakini viongozi wa Afrika wanashindana kwenda kuhifadhi pesa huko, na Waswiz wanatumia pesa hiyo kuwakopesha wananchi wao na wawekezaji mbalimbali wa kimataifa na kujipatia faida kubwa.
Jibu ni moja tu bwana Mwashamba, utajiri mkubwa katika Ulimwengu huu upo kichwani. Na huo utajiri wa kichwani, viongozi wengi wa Afrika wameukosa.
Awezi kuja hapa labda apite kimyakimya."If the owners of the natural resources go around begging, then you should know there's something wrong with their minds”
View attachment 3009379
Mimi huwa sikimbii hoja ndugu yangu na ndio maana nimejibu kwa hoja nzito sana na za kutetemesha.Awezi kuja hapa labda apite kimyakimya.
Huo upuuzi ndio hoja?Mimi huwa sikimbii hoja ndugu yangu na ndio maana nimejibu kwa hoja nzito sana na za kutetemesha.
Acha ujinga wako . unafikiri ni matangazo ya mpira hayo hadi aanze kutangaza?Huo upuuzi ndio hoja?
Kwani ameshindwa kutangaza tu kwamba tuna gas,miti,madini na wateja wakaja mpaka azurure?
Hakuna lugha ya kizungu huku duniani. Alichoongea hapo ni Kingereza!Acha dharau zako wewe. Mimi nimepiga shule sana na nilikuwa kinara wa kuongea kizunguu kwenye mijadala shuleni mpaka wanafunzi wanashangilia kwa kelele za shangwe huku wanabubujikwa na machozi ya furaha.