Lucas Mwashambwa toa maoni yako kuhusu kauli ya Rais Paul Kagame

Huyo @ephen na mumewe wote vichwa maji.
Nahisi bado hawajaelewa kinachozungumzwa.
Kagame hajazungumzia kukopa ama madeni bali kazungumzia kuomba.
Mwambie apimie Kagame kasafiri mara ngapi toka mwaka uingie kwenda kuomba fedha za miradi kama alivyofanya Samia?
 

Kama ni mtihani, hapo Mwashambwa umejitahidi. Umepata 70%.

Jibu sahihi hapo ni moja tu, na umeliweka kwenye majibu yako. Ungepata 100% ila umeharibu kwa kuongeza mengine yasiyo sahihi.

Rasilimali kubwa inayoweza kukufanya umudu mazingira yako iwe kiuchumi, kitekinolojia, kielimu na hata maarifa, ni AKILI. Siyo mikia ya fisi, siyo madini, gesi, mito na maziwa yenye maji mazuri, mafuta au ardhi nzuri ya kilimo. Ila ukiwa na AKILI, halafu ukajaaliwa kuwa na rasilimali asilia, hakika unapaa kimaendeleo. Ukiwa huna akili, ukajaaliwa kuwa na mito mingi, utaanza kulalamika na kuona mito ni kero kwa sababu huna uwezo wa kujenga madaraja. Utaanza kulalamikia mawe yenye madini ni kero kwa sababu milima ya mawe inakufanya ushindwe kutengeneza barabara nzuri, utalalamikia uwepo wa wanyama pori kwa sababu wanakula mbuzi wako na wanaua wananchi, kwa vile tu wananchi wako, hawana makazi bora na salama.

Switzerland hawana rasilimali asilia karibia zote lakini viongozi wa Afrika wanashindana kwenda kuhifadhi pesa huko, na Waswiz wanatumia pesa hiyo kuwakopesha wananchi wao na wawekezaji mbalimbali wa kimataifa na kujipatia faida kubwa.

Jibu ni moja tu bwana Mwashamba, utajiri mkubwa katika Ulimwengu huu upo kichwani. Na huo utajiri wa kichwani, viongozi wengi wa Afrika wameukosa.
 
Mtoa ujumbe mwenyewe huyo anamadeni kibao sana Nchini kwake. Muulizeni kwanini alikopa na kuomba msaada?

Soma vizuri comment yake. Inaonekana umekimbilia kujibu bila kuelewa alichokiandika.

Anasema kuwa kama nchi ni tajiri wa rasilimali asilia, halafu kiongozi wake anakuwa ombaomba, basi ana shida kichwani.

Rwanda siyo nchi tajiri katika mali asilia. Huu ujumbe ni kwa viongozi wa mataifa tajiri ya mali asilia tu.

Katika orodha ya nchi 15 zenye rasilimali nyingi asilia Afrika, bahati mbaya Tanzania haimo. Labda ndiyo maana viongozi wetu kila siku wapo kuomba misaada.
 
Kumbe una akili nyingi sana ukituliaga vizuri chini na kuandika. Bonge moja la Comment . Nimefurahi sana majibu na andiko lako hili. Japo huwa tunakwaruzana mara kwa mara ila leo umenikosha na wala sina nyongeza .Huu ndio upinzani naoupenda mimi. Upinzani wa hoja.ambao mtu akiandika hoja kama ulivyofanya wewe mpaka mwingine unaona aibu kupinga ukweli huo.

Safi sana.kichwa chako kipo vizuri sana na upo vizuri sana kichwani.leo Umeniongezea kitu kichwani mwangu na ni comment moja bora sana niliyoipenda kwa kweli . Tuwe tunafanya hivi kila siku .
 
Huyu mama 24/7 ni kiguu na njia, hatulii, akitulia ujue amekuja kupika deal jingine la kuuza nchi, anarud tena kuzurura. Yan awamu hii tuna sales and marketing officer pale magogoni.

Ujumbe wa kagame roho imeniuma mmi kama ndio mkuu wa nchi vile
 
Acha dharau zako wewe. Mimi nimepiga shule sana na nilikuwa kinara wa kuongea kizunguu kwenye mijadala shuleni mpaka wanafunzi wanashangilia kwa kelele za shangwe huku wanabubujikwa na machozi ya furaha.
Hakuna lugha ya kizungu huku duniani. Alichoongea hapo ni Kingereza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…