Siyo Rasilimali za asili pekee unazomiliki ndio zinakufanya uwe tajiri.bali inahitaji akili ,pesa, teknolojia,maarifa na ujuzi wa watu wako unaotokana na kupata Elimu bora na ya viwango vikubwa.
Embu fikiria hata kama una gesi asilia lakini huna pesa, wataalamu wenye ujuzi na uzoefu, teknolojia na mengine mengi ni vipi utavuma gesi hiyo?
Hiyo ndio sababu ya viongozi wenye Akili kubwa ,maarifa na maono makubwa aina ya Daktari Samia Suluhu Hasssan hutumia akili kutafuta pesa kwa njia mbalimbali kama ya mikopo nafuu kabisa isiyo na athari wala maumivu kwa walipakodi na mali na utajiri wa Taifa letu.
Lakini pia kuna masuala ya ubia kati ya serikali na Secta binafsi kama ambavyo hufanyika hapa Nchini na njia nyingine mbalimbali zinazokubalika na zenye maslahi kwa Taifa letu.
Angalia hata Mheshimiwa Paul Kagame yeye na Nchi yake wanadaiwa shilingi ngapi kutoka mataifa ya nje,taasisi za kifedha na mashirika mbalimbali ya kifedha kutoka maeneo mbalimbali Duniani?