Gazeti la mwananchi lilishaandika makala juu yako wewe Luhanga Mpina mbona hujakanusha mpaka Leo kuhusu hizo ekari ulizopora Morogoro Katika kijiji cha dala
Mwezi February mwaka 2021 tarehe 24 taarifa zako zilimfikia Katibu mkuu wa wakati huo Dkt Bashiru na kuchapwa kwenye gazeti la mwananchi tarehe hiyo
Luhaga Mpina anza kutoa boriti kwenye jicho lako kwanza halafu njoo Utoe vibanzi kwenye macho ya wenzako
Uchafu uliofanya ukiwa Waziri wa mifugo unajulikana, Wewe na Rushwa ni Pete na chanda,
Zakayo kwenye biblia alikuwa mtoza ushuru na mtu tajiri wa kupitiliza, Alipoamua kubadilika na kuigeukia injili aliomba msamaha na kuwarudishia wadeni wake wote, Zakayo kwa wale aliowatoza kwa makusudi aliwarudishia mara mbili na wale wote aliowadhulumu Mali zao aliwalipa mara mbili
Luhanga Mpina wakati wa JPM wananchi wa Morogoro uliwapora ekari zaidi ya elfu moja na mpaka sasa Wanalalamika kuhusu maeneo yao
Luhanga Mpina ulichukua rushwa kwa wavuvi wakubwa ambao walipindisha sheria na kuendelea kuvua kwa nyavu zisizo na viwango kama za wavuvi wadogo lakini kwa wavuvi wadogo uliwachomea nyavu zao
Malalamiko ya wavuvi wadogo yalipelekwa mpaka kwa bosi wako kuwa unawachomea wao nyavu wakati wavuvi wakubwa unapokea rushwa na wanaendelea kuvua
Kama kweli wewe ni mzalendo rudisha hizo ekari zaidi ya elfu moja Mkoa wa Morogoro, Pia rudisha pesa zote ulizochukua kwa wavuvi wakubwa baada ya hapo nami nitaunga kambi yako ya mapambano
Tuache unafiki na tuweke siasa pembeni Luhaga Mpina ni moja ya watu walioogopwa enzi za utawala wa awamu ya tano kwa kuwa karibu na Mwenyekiti wa ccm Taifa
Kama Leo ameanzisha mapambano awarudishe watu wa Morogoro ekari alizojitwalia kinguvu nasi tumuunge mkono
Tutakuwa ni nchi ya ajabu mtu aina ya Sabaya au Makonda akajitokeza kwenye mapambano ya haki za binadamu huku wao wakiwa binafsi hawajawaomba msamaha waathirika kwa mambo waliyowatendea.
Kwa hisani ya
seedfarm