Luhaga Mpina awekewe ulinzi iwapo kweli tuna maana ya kupiga vita ufisadi!

Luhaga Mpina awekewe ulinzi iwapo kweli tuna maana ya kupiga vita ufisadi!

Huez piga vita ufisadi wakat naww ni mshirika wa mfumo wa mafisadi!! Mzalendo Assad alitolewa mbio na akakosa kaz kisa kuhoji pesa ambayo matumizi yake hayajulikan!! Uzalendo Nchi baado san!!
Kama ni mzalendo si mmrudishe nyie si ndo kila kitu mmeshika dolla kama mna mmic sana si mumteue
 
Hapana nachosema ni kwamba huyo shida sio kupambana na ufisadi Bali anataka uwaziri akishaupata atakana maneno yake yote.

Nasema hivi maana huko nyuma tuliwahi support kina Bashe ila walipopata uwaziri wote mmeona majibu Yao ya kejeli kwa shida za wananchi maskini.

Mfano huyu Mpina hakuunga mkono katiba mpya enzi za Jiwe ila Kwa Sasa eti ndio amegundua ni ya muhimu kama sio unafiki ni Nini?
Katika historia ya nchi yetu najaribu kukumbuka waziri yeyote aliyewahi "kupambana" dhidi ya ilichokisimamia serikali aliyokuwemo, simpati!. Naomba usinipe mfano wa Oscar Kambona.

Pengine wewe unao mfano mzuri unistue kuhusu hili.

Binafsi, mimi sitajali sana kama mtu aliyewahi kuwa serikalini, lakini kutokana na fungate zinazowafunga mdomo wakiwa huko, halafu wanapotoka wakawa ni watu wanaopigania maslahi mapana ya jamii; hata kama ni kwa kuigiza, mimi nitaungana naye. Na hasa, kama mtu huyo hana historia mbaya ya ushiriki katika maovu akiwa huko serikalini; nitampa heshima yake stahiki.

Sijui hapa kama Mpina anagombea u-waziri. Litakuwa ni jambo la kushangaza sana kama anategemea kupewa uwaziri kwa kuwasema watu hao hao wanaosababisha hayo anayoyapinga.

Hapana. Kwenye hili wewe na mimi tumesimama mbali sana kiasi kwamba hata tupigiane kelele vipi tutaweza kusikilizana juu yake.

Katika wote waliopo humo CCM, sasa hivi ni sauti ya Mpina pekee inayosikika ikiwa tofauti na wengine wote. Sasa sijui kama huko CCM hawapo wanaoutamani uwaziri hata kuliko Luhaga Mpina!
 
Naomba mwny link ya video akiwa anayasema haya,napenda sana kumuona Mpina akiwa anatema cheche na reactions za wanaosemwa pia
 
Tutumie tena fedha ya nchi kifisadi kumlinda mtu mmoja anayejipigania yeye kisiasa?! Ajiondoe kwanza kwenye chama cha kifisadi.
Kwanza kwa kupiga zake kelele ameokoa shilingi ngapi hadi sasa?! Kuna kiasi chochote cha pesa kimerudishwa Na Hao mafisadi baada ya kelele zake?
Yeye katimiza wajibu kuhoji na kukufahamisha ww mwananchi, kuhusu hatua inabid uchukue ww mwananchi kataa wapigaji kwny kura ama watandike mabomu tu wafie mbali
 
Utasemaje ukijua kwamba yeye ndiye dereva wa hayo mafisadi?
Ndiyo maana nimeshauri akamatwe nikijuwa wazi naye anahusika hapa. Haiwezekani waziri wake aibie taifa yeye asijuwe. Mama akamatwe tu.
 
Sema chini ya mama ufisadi unaibuliwa.

Huyo mpina angeyajuwa hayo ys ufisadi bila mama kuruhusu report za CAG zisasambuliwe bungeni?

Mmesahau bwana yule alivyolitumia bunge kumminya CAG?
Mamaa! Tupeane kadi leo, nami nakulaga plau aisee!
 
Nipo Mkuu, sikukuu vipi aisee, kadi wapi kiongozi, Mimi pia ni mtaalam wa kula plau aisee
Karibu, Mimi nipo Sangamwalugesha karibu na Nzuginaminzi! Elekea njia inayokwenda kisarawe ukifika mwanarumango ulizia kwa MzeewaShy !
 
Karibu, Mimi nipo Sangamwalugesha karibu na Nzuginaminzi! Elekea njia inayokwenda kisarawe ukifika mwanarumango ulizia kwa MzeewaShy !
Kwa hiyo maji ya kunywa na kunawa nakuja nayo kabisa?

Nzuginaminzi?
 
Watu waliojiapiza maisha yao, kufa au kupona, kuuwa ama kuuwawa, ni mafisadi!

Ikiwa kweli mnamaanisha kupambana na watu hao hatari, anapotokea mtu mmoja kujitoa mhanga kuwataja hadharani watu hatari kama how, Sisi ambao tuko nyuma ya vita hiyo, jambo moja tu tunapaswa kufanya,

Ni kumuunga mkono mtu huyo na kuhakikisha maisha yake yako salama!

Mpina awekewe ulinzi, la sivyo tutakuwa tumekubali kwamba, pesa zinazokuwa zikiibwa na mafisadi, kwa upande mmoja na sisi tu wamoja wao!

Mpina anasaidia sana kubainisha kwa uwazi bila kuogopa kuwataja mafisadi hao

Lakini kwa upande mwingine, anahatarisha mno maisha yake!

Kundi la mafisadi ni watu wenye umoja na wako tayari kufanya chochote juu ya mtu yeyote!

Watu kama Mpina, kwa mfumo wetu ulivyo mbovu, hapaswi kuteuliwa kuwa waziri, anapaswa awe na nafasi hii hii aliyopo ili kuwakaanga mafisadi, maana akiwa upande wa serikali, hawezi kuchangia wala kuibua uozo wowote wa serikali kwa sababu yeye anakuwa mtetezi wa serikali
Sukuma Gang anzisheni chama chenu awe mwenyekiti
 
Mkuu, inauma sana aisee, halafu hakuna hata kuwajibishwa kwa hayo majizi
We mshamba hata ripot ya CAG Hujui maana yake? Unataka watu wawajibishwe kabla ya kujibu hoja za mkaguzi? Mnawaita watu majina mabaya kwa kuhisi tu? Subirin wajibu hoJ ndo hatua zichukuliwe. Inauma sana hata kodi unalipa wewe
 
Back
Top Bottom