M wekeza ni bonge la uwekezaji kutoka Vodacom kwa watu wenye mpunga wa maana

M wekeza ni bonge la uwekezaji kutoka Vodacom kwa watu wenye mpunga wa maana

Toa basi ramani bro na sisi tuangalie namna,ila usije kuwa umetumwa na voda unatutangazia biashara kiaina hapa.
 
Mkuu hii huduma ya Vodacom m wekeza unaweka pesa halafu gawio linakua linatoka Kila mwezi tarehe Moja yaani ukiweka mpunga wa maana kazi Yako inakua kuandaliwa maziwa na wife huku wewe ukiichapa
Weka numbers Kuna watu wametoka kufuliwa Lb
 
Wakuu hii huduma ya Vodacom m wekeza ni bonge la uwekezaji aisee yaani nimetia pesa huko Sasa hivi nafanya kazi ya kuamka na Taulo huku nikinywa maziwa pesa yangu ikiniletea faida halafu uzuri wanaweka pesa. Tarehe 1 tu mwanzoni mwa mwezi mungu anipe nini mimi

Weka mfano iwapo mdau wa JF akaweka 3,000,000, Je atarajie faida ya TZS ngapi kwa kila mwezi?
- Hapo utrakuwa umesaidia wengi.
 
Jamaa Muongo huyu.
M wekeza ni 13%, uwekezaji wa mwaka.
milioni kumi kwa mwaka utapata faida 1.3ml
Sawa na 108000 kwa mwezi na huwezi toa hela mpka mwaka upinduke. Hawatoi kwa mwezi.

Sasa huyu kuku kawekeza bei gani apikiwe maziwa na taulo
Yumkini ndiyo maana akiulizwa maswali anakuwa mkali?

Eti maziwa na taulo huyo Bahakresa na ukwasi wake hakai kibarazani asubuhi kunywa chai anakunywa amesimama ili kuwahi mishe ndiyo M-pesa waje kumpa mtu faida ya kubweteka?
 
Wewe hutaki watu tunufaike na huo mfuko au mijitu mieusi bhana kwahiyo unataka tuwe masikini kama wewe milele pambana na Hali Yako
Sasa mzee si utoe elimu umeweka kiasi gani unapata kiasi gani baada ya muda gani kwani kuna atakayekuja kukukaba ndugu?

Mnufaike wewe na nani sasa kama siyo sisi ulio-share nasi hii ishu,basi ilikuwa haina haja kupandisha uzi hapa kutupagawisha wakati ulijua ulitaka unufaike wewe na wa nyumbani kwako.
 
Ngoja niitafute laini ya Vodacom
Kawaulize Vodacom Sina mda wa kuweka mifano
Kwa majibu haya mkuu wala usijisumbue!

Huyu ni wale wasajili line katumwa aje humu kupandisha soko la uuzaji wa line za voda,siioni mantiki mtu anashindwa vipi ku-share details chache tu kama kaweka bei gani kwa muda gani na kapata faida bei gani?
 
Huyu kaweka laki mbili na anapata 26k per year, sasa kaja jf kakuta watu wanapiga hesabu za milioni 50 mara milioni 100, wengine milioni 250 ...

Akaona eheee ishakua noma, kesi ishakua ngumu hii, kumbe huku ni kwa matajiri na hesabu wanazijua,. Ndio chanzo cha kulala mbele na kua mkali.
 
Hasira za nini siweki detail zangu hata usemaje
 
Kwa majibu haya mkuu wala usijisumbue!

Huyu ni wale wasajili line katumwa aje humu kupandisha soko la uuzaji wa line za voda,siioni mantiki mtu anashindwa vipi ku-share details chache tu kama kaweka bei gani kwa muda gani na kapata faida bei gani?
Uzuri Vodacom kampuni inayojulikana zaidi duniani yaani sio tanzania tu hivyo Kila siku wateja wapya wanasajili laini hivyo Mimi siwezi kuongeza Wala kupunguza chochote kikubwa nimeshasema Sasa hivi ni mwendo wa kunywa maziwa kibarazani kwangu huku wife akikarangiza vinono daily
 
Hasira za nini siweki detail zangu hata usemaje
Hakuna anaetaka detail kijana, kua muelewa, kama umeamua kushare fursa dadavua ni kiwango gani chafaa mtu kuwekeza.

Faida ikoje, awe makini na kipi na kipi aepuke kabisa, pesa unatoaje nk.

Ukifata details vodacom, watakupa details ili uweke hela, hawatakipa risks associated na huo uwekezaji.

Ndio maana wadau wanatamani kusikia kutoka kwako wewe ulieweka mzigo na kudai umepata faida unaeeza kua na ukweli bila upendeleo.
Sio details zako weka mifano.
 
Uzuri Vodacom kampuni inayojulikana zaidi duniani yaani sio tanzania tu hivyo Kila siku wateja wapya wanasajili laini hivyo Mimi siwezi kuongeza Wala kupunguza chochote kikubwa nimeshasema Sasa hivi ni mwendo wa kunywa maziwa kibarazani kwangu huku wife akikarangiza vinono daily
Huna jambo bwana wewe amka kwenye huo usingizi mzito uliokushika ingia mtaani tafuta vibarua ufanye upate hela ya kula acha kujifariji ujinga!
 
Huna jambo bwana wewe amka kwenye huo usingizi mzito uliokushika ingia mtaani tafuta vibarua ufanye upate hela ya kula acha kujifariji ujinga!
We umepagawa sio bure mtu humjui unasema anajifariji hahahaha unatatizo la afya ya akili🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom