Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

mabikra wapo, tuongee vizuri na wagikulu wise
Kwa hawa waliopita vyuoni mtalaumu wagikūlū wenu bure tu 😂

Baching'wa na masisūngū ambika na mbika. Abangī balībatolwa ūgūmachuo gabo mpaga bafunya na nda! 🚮

-771953229.jpg
 
1. Muheshimu MUNGU.
2.Watunze wazazi.
3. Kuwa moderate katika imani.
4. Milki Ardhi na mashamba.
5. Fanya kazi kwa bidii.
6. Jihadhari na wanawake. Kwao kuna uzima na mauti.
7.Tafuta elimu kila siku.
8. Tafuta elimu mahsusi kuhusu mambo ya hisa na mitaji.
 
78 yrs here speaking. Nitaandika kwa kirefu kidogo na kwa uwazi. Kama kijana mmoja atasaidika basi itakuwa poa sana!

Iko hivi. Kama unataka utoboe huku 65+ hakikisha una furaha, huna wivu wa ******* na usijilinganishe na mtu. Vinginevyo utaRIP mapema tu kwa kushambuliwa na moyo wako mwenyewe au harusi huko juu ubongoni. Unaipataje furaha? Nao liseni vere keafuli:

➡️➡️ 1. Linda sana afya yako. Asikudanganye mtu: Afya yako ndo kila kitu. Under 35 unaweza kujiona mwamba lakini hiki ndicho kipindi cha kuepuka presha, kisukari, matatizo ya moyo, baadhi ya saratani na magonjwa mengine mengi yasiyo ya kuambukiza huko mbele ya safari. Kati ya majuto makuu niliyonayo ni kunywa pombe sana na kuponda raha kupitiliza ukiwemo ulaji wa hovyo huko nyuma. Japo nimeweza ku-reverse karibu kila kitu kilichokuwa kimeanza kwenda mrama (pre-diabetic, BP, acute sleep apnea, obesity....) na kuwa sawa lakini imenigharimu sana (muda na mengineyo).

Kijana under 35:
  • Punguza au acha kabisa pombe
  • Kamwe usivute sigara wala kutumia ugoro
  • Ogopa sana sukari
  • Angalia usinenepe na kuwa futufutu.
  • Punguza caffeine (energy drink).
  • Angalia mlo wako
  • Anza kuangalia sukari, BP na lehemu.
  • Usitumie boosters za nguvu za kiume
  • Hakikisha hupati UKIMWI 📌📌📌
  • Mazoezi na lishe bora vitakupa uzee safi
  • Anza kujali afya ya ngozi yako ili kuepuka kuchakaa mapema (nione kama unahitaji msaada katika hili)
  • Ukijisikia hauko sawa nenda hospitali.
  • Tumia common sense kwenye kila kitu.
Kumbuka: Hiki ndicho kipindi cha kuweka misingi ya afya njema ukifika huku 45+. Na bila kuwa na afya njema huwezi kufurahia maisha. Kwa kifupi hakikisha huandai mazingira ya kuja kupata BP, kisukari na ishu zingine sugu huku mbele ya safari.

➡️➡️ 2. Uchumi: Hata kama hutakuja kuwa tajiri wa kupigiwa mfano lakini hakikisha una uwezo wa kupata mahitaji yako ya msingi bila kusumbua watu. Ukiumwa ujitibu. Ule cho chote unachotaka. Uende po pote unapotaka na ufanye cho chote unachotaka bila kutegemea misaada ya watoto wako, ndugu, jamaa, marafiki na wasamaria wema. Under 35 ndiyo kipindi kizuri cha kuanza kuweka misingi sahihi ya kuja kuwa na uzee wenye neema na mibaraka. Ukikichezea kipindi hiki, huku mbele kuna majuto makubwa yanakusubiri kmmk!

➡️➡️3. Kua kihisia - Emotional Intelligence (EI). Usipokuwa na emotional intelligence kubwa maisha yatakuendesha maana kila kitu kwako ni crisis ushapaniki presha iko juu unataka kufa. Hii itakusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuchukulia mabaya yanayokutokea (zikiwemo hekaheka za mapenzi) kama sehemu muhimu ya maisha maana maisha bila hekaheka na amsha amsha yanaboa kishenzi 👋. Usipokuwa na emotional intelligence (EI) kubwa utaishi maisha ya wasiwasi, hasira, stress, nuksi na kuudhi watu; na utakuwa mgumu sana kupendeka.

Unapataje EI kubwa?
  • Kuwa na utulivu wa kiroho
  • Kupenda kujifunza mambo mapya
  • Kukubali kubadilika kulingana na wakati
  • Kusoma vitabu
  • Kutokujilinganisha na watu wengine
  • Kutambua kwamba kila mtu unayekutana naye ana matatizo anayopambana nayo; na pengine makubwa kuliko uliyonayo.
  • Kutokulalamika na kulaumu wengine.
  • Kutambua kwamba maisha yako ni jukumu lako 100%; na kwamba hakuna mtu aliyezaliwa ili aje akupe maisha mazuri (labda wazazi wako - kama bado wapo na bado uko under 18).
  • Kuwa mtu mwema; na kusaidia wengine.
  • Jenga familia/mahusiano yenye upendo
  • Jifunze kusamehe.
  • Jitambue na kujithamini; na usitake kupendwa na kila mtu
  • Kutambua kwamba mwisho wa yote kuna kifo kinakusubiri; na hizi hekaheka zote zitakoma.
Nadhani kwa sasa haya yanatosha. Tabia yangu ya kupenda kujifunza mambo na kuangalia watu katika upande chanya hivi karibuni ilinikutanisha na rafiki wa kipekee sana maishani mwangu. Polepole na kwa uvumilivu mkubwa pamoja na maumivu rafiki yangu huyu aliweza kunionyesha kwamba sikuwa sawa katika hilo eneo la emotional intelligence. Japo sikujua lakini kumbe nilikuwa ni mmoja wa wale watu wenye hasira za haraka haraka tu. Watu ambao jambo dogo tu wameshakasirika halafu baadaye wakipoa wanaanza kujuta (They hurt themselves more by trying to hurt others). Safari ya miaka mitatu hivi na rafiki yangu huyu kutoka kwa Mungu hatimaye imenitoa huko mpaka wanangu na wajukuu zangu wanasema "umekuwaje wewe?". Kusema kweli nimekuwa calm sana na siyo yule mtu wa kuona mlima kwenye kila tatizo hata kama tatizo lenyewe lina kimo cha kichuguu...and looking back sasa ninaweza kuona ni kwa nini hata baadhi ya mahusiano yangu huko nyuma hayakufanikiwa kwa sababu mimi sikuwepo kwenye mahusiano yale kwa jinsi mtu mwenye upendo wa kweli anavyopaswa kuwa. High emotional Intelligence inakupa uwezo wa kuliangalia jambo katika upana wake na kupima outcomes na consequences zake mbalimbali kabla hujaamua kulitolea uamuzi. Tena unafanya hivyo kwa hekima na busara. Matokeo yake ni amani ya kweli, utulivu wa fikra na mkong'osio wa roho na mwili. Total tranquility!

Asante sana rafiki yangu uliyejitolea miaka yako mitatu kusafiri nami na kutumia taaluma yako ya saikolojia ili kuhakikisha kuwa nimekuwa mtu mpya - baba bora kwa wanangu, rafiki wa kupigiwa mfano, binadamu mvumilivu, mtu anayejitambua, kiumbe anayependeka na.....

Huwa una maneno transformational na yenye baraka sana na kukiri kuwa, umejifunza kitu kipya na kubadilishwa katika umri wako. Inaonesha kuwa hakuna kuchelewa katika kubadilika, what matters ni mabadiliko

Kingine mkuu, naamini kuwa huru kifedha yani kuweza kujimudu kimaisha inaepusha mambo mengi ikiwemo fedheha, dharau na manung'uniko yanayosababishwa na ukali wa maisha lakini pia kutokuthaminika kwa watu.

I'm almost a half of your age na naweza kiri katika kipindi cha miaka nane hiki.. Nimejifunza mengi ambayo umeyasema lakini pia yamenibadilisha kiasi cha kuanza kujipenda na kujithamini mimi kwanza. Kujiweka first priority na kuwa commited kwangu kwa sababu kiuhalisia kila mtu atakuacha kwenye point moja ya maisha kwa hiyo ukitegemea wengine au ukajitolea kwa wengine kiasi cha kujipuuza wewe kwanza ili uwanyooshee wengine mapito yao. Meza ikipinduka si ajabu ukajikuta upo peke yako

No call, no friends, no nothing.. Na hata kama wapo watakaokuja baadhi Ila nao wataondoka tu lakini Mungu akijaalia unaweza pata hata mmoja wa kusimama nawe. Na hapo life linakufunulia watu wakuwa nao ukiwa katika ubora wako

Wengine ibaki story na kuangalia usefulness yao maana wengi hutumia urafiki ili kukutumia but when you say no.. Ndio utaziona rangi zao halisi. Kwa hiyo wasio marafiki unaangalia common ground. Kama hakuna wabakie watu wa salamu tu
 
Maisha kila mtu ana tafsiri yake haziwezi fanana kwa mtu mmoja mmoja.
Kuwa karibu na Ibada kutoka na imani yako.

1. Uaminifu
2. Juhudi
3. Ukweli
4. Respect ( HESHIMU muda, watu, kazi, pesa, Matumizi, vitendea kazi, eneo la kazi, nk)
 
Usitegemee pesa ya kula ambayo haipo mfukoni kwako kama cash utakuja kulala na njaa kimasihara..

Pesa haitafutwi inawekewa mtego alafu unatulia zako, sisi ambao tulikosea kuweka mtego Wacha tuendelee kuzitafuta
Ushauli makini sana! Shukrani kwako
 
Ma brother wa kuanzia 35+ najua nyinyi tayari ni watu wazima na mme pitia mengi kwenye haya maisha.

Hebu tupeni ushauri wowote iwe kwa uzoefu au Kama angalizo litakalo tufaa wadogo zenu.

Iwe kiuchumi, mahusiano, elimu, au vyovyote itakavyo kuwa poa.

I mean no malice to nobody.
View attachment 3276424
Pombe na uzinzi vinafelisha vijana sana, yaani ukizeeka hutakiona hata kimoja kwenye maisha yako. Weka akiba utaiona baadae. Uzinzi na pombe hutaviona.
 
Huwa una maneno transformational na yenye baraka sana na kukiri kuwa, umejifunza kitu kipya na kubadilishwa katika umri wako. Inaonesha kuwa hakuna kuchelewa katika kubadilika, what matters ni mabadiliko

Kingine mkuu, naamini kuwa huru kifedha yani kuweza kujimudu kimaisha inaepusha mambo mengi ikiwemo fedheha, dharau na manung'uniko yanayosababishwa na ukali wa maisha lakini pia kutokuthaminika kwa watu.

I'm almost a half of your age na naweza kiri katika kipindi cha miaka nane hiki.. Nimejifunza mengi ambayo umeyasema lakini pia yamenibadilisha kiasi cha kuanza kujipenda na kujithamini mimi kwanza. Kujiweka first priority na kuwa commited kwangu kwa sababu kiuhalisia kila mtu atakuacha kwenye point moja ya maisha kwa hiyo ukitegemea wengine au ukajitolea kwa wengine kiasi cha kujipuuza wewe kwanza ili uwanyooshee wengine mapito yao. Meza ikipinduka si ajabu ukajikuta upo peke yako

No call, no friends, no nothing.. Na hata kama wapo watakaokuja baadhi Ila nao wataondoka tu lakini Mungu akijaalia unaweza pata hata mmoja wa kusimama nawe. Na hapo life linakufunulia watu wakuwa nao ukiwa katika ubora wako

Wengine ibaki story na kuangalia usefulness yao maana wengi hutumia urafiki ili kukutumia but when you say no.. Ndio utaziona rangi zao halisi. Kwa hiyo wasio marafiki unaangalia common ground. Kama hakuna wabakie watu wa salamu tu
Sina cha kuongezea mdogo wangu maana, kama ilivyo kawaida yako, umetema madini tupu! Wewe ni mmoja kati ya watu ambao huwa naamini kuwa una emotional intelligence kubwa sana; na ni mtu unayependa kujisomea. Comments zako ninazokutana nazo huwa zina kitu hai ndanimwe na huwa najifunza mengi.

Umeongea mambo ya msingi sana na natumaini kuwa hawa madogo wa under 35 watajifunza kitu. Ndiyo. Wanaume tuna tabia ya kujisahau sana na ku-prioritize watu wengine. Halafu wakati ukifika tunabaki peke yetu; na matokeo yake ndiyo haya ya kufa mapema tunayoyaona. Kwangu mimi miaka mitatu hii imenifunza mambo mengi ambayo huko nyuma nilikuwa nayachukulia poa.

Tuendelee kujifunza. Tuendelee kubadilika. Tuendelee kujiboresha. Maisha yanatutaka tufanye hivyo. Kwa faida yetu, wale tuwapendao na binadamu wenzetu! 🙏🏿
 
Huwa una maneno transformational na yenye baraka sana na kukiri kuwa, umejifunza kitu kipya na kubadilishwa katika umri wako. Inaonesha kuwa hakuna kuchelewa katika kubadilika, what matters ni mabadiliko

Kingine mkuu, naamini kuwa huru kifedha yani kuweza kujimudu kimaisha inaepusha mambo mengi ikiwemo fedheha, dharau na manung'uniko yanayosababishwa na ukali wa maisha lakini pia kutokuthaminika kwa watu.

I'm almost a half of your age na naweza kiri katika kipindi cha miaka nane hiki.. Nimejifunza mengi ambayo umeyasema lakini pia yamenibadilisha kiasi cha kuanza kujipenda na kujithamini mimi kwanza. Kujiweka first priority na kuwa commited kwangu kwa sababu kiuhalisia kila mtu atakuacha kwenye point moja ya maisha kwa hiyo ukitegemea wengine au ukajitolea kwa wengine kiasi cha kujipuuza wewe kwanza ili uwanyooshee wengine mapito yao. Meza ikipinduka si ajabu ukajikuta upo peke yako

No call, no friends, no nothing.. Na hata kama wapo watakaokuja baadhi Ila nao wataondoka tu lakini Mungu akijaalia unaweza pata hata mmoja wa kusimama nawe. Na hapo life linakufunulia watu wakuwa nao ukiwa katika ubora wako

Wengine ibaki story na kuangalia usefulness yao maana wengi hutumia urafiki ili kukutumia but when you say no.. Ndio utaziona rangi zao halisi. Kwa hiyo wasio marafiki unaangalia common ground. Kama hakuna wabakie watu wa salamu tu
humu nime Soma ushauri deep kama wa watu 3-4, wewe ukiwa mmoja wao.
 
Pombe na uzinzi vinafelisha vijana sana, yaani ukizeeka hutakiona hata kimoja kwenye maisha yako. Weka akiba utaiona baadae. Uzinzi na pombe hutaviona.
bahati nzuri au mbaya mimi sija wahi tumia pombe, sigara, bangi na wala sio mzinzi mkuu.

it's just a choice ninayo jivunia, Asante kwa ukumbusho mzuri.
 
78 yrs here speaking. Nitaandika kwa kirefu kidogo na kwa uwazi. Kama kijana mmoja atasaidika basi itakuwa poa sana!

Iko hivi. Kama unataka utoboe huku 65+ hakikisha una furaha, huna wivu wa ******* na usijilinganishe na mtu. Vinginevyo utaRIP mapema tu kwa kushambuliwa na moyo wako mwenyewe au harusi huko juu ubongoni. Unaipataje furaha? Nao liseni vere keafuli:

➡️➡️ 1. Linda sana afya yako. Asikudanganye mtu: Afya yako ndo kila kitu. Under 35 unaweza kujiona mwamba lakini hiki ndicho kipindi cha kuepuka presha, kisukari, matatizo ya moyo, baadhi ya saratani na magonjwa mengine mengi yasiyo ya kuambukiza huko mbele ya safari. Kati ya majuto makuu niliyonayo ni kunywa pombe sana na kuponda raha kupitiliza ukiwemo ulaji wa hovyo huko nyuma. Japo nimeweza ku-reverse karibu kila kitu kilichokuwa kimeanza kwenda mrama (pre-diabetic, BP, acute sleep apnea, obesity....) na kuwa sawa lakini imenigharimu sana (muda na mengineyo).

Kijana under 35:
  • Punguza au acha kabisa pombe
  • Kamwe usivute sigara wala kutumia ugoro
  • Ogopa sana sukari
  • Angalia usinenepe na kuwa futufutu.
  • Punguza caffeine (energy drink).
  • Angalia mlo wako
  • Anza kuangalia sukari, BP na lehemu.
  • Usitumie boosters za nguvu za kiume
  • Hakikisha hupati UKIMWI 📌📌📌
  • Mazoezi na lishe bora vitakupa uzee safi
  • Anza kujali afya ya ngozi yako ili kuepuka kuchakaa mapema (nione kama unahitaji msaada katika hili)
  • Ukijisikia hauko sawa nenda hospitali.
  • Tumia common sense kwenye kila kitu.
Kumbuka: Hiki ndicho kipindi cha kuweka misingi ya afya njema ukifika huku 45+. Na bila kuwa na afya njema huwezi kufurahia maisha. Kwa kifupi hakikisha huandai mazingira ya kuja kupata BP, kisukari na ishu zingine sugu huku mbele ya safari.

➡️➡️ 2. Uchumi: Hata kama hutakuja kuwa tajiri wa kupigiwa mfano lakini hakikisha una uwezo wa kupata mahitaji yako ya msingi bila kusumbua watu. Ukiumwa ujitibu. Ule cho chote unachotaka. Uende po pote unapotaka na ufanye cho chote unachotaka bila kutegemea misaada ya watoto wako, ndugu, jamaa, marafiki na wasamaria wema. Under 35 ndiyo kipindi kizuri cha kuanza kuweka misingi sahihi ya kuja kuwa na uzee wenye neema na mibaraka. Ukikichezea kipindi hiki, huku mbele kuna majuto makubwa yanakusubiri kmmk!

➡️➡️3. Kua kihisia - Emotional Intelligence (EI). Usipokuwa na emotional intelligence kubwa maisha yatakuendesha maana kila kitu kwako ni crisis ushapaniki presha iko juu unataka kufa. Hii itakusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuchukulia mabaya yanayokutokea (zikiwemo hekaheka za mapenzi) kama sehemu muhimu ya maisha maana maisha bila hekaheka na amsha amsha yanaboa kishenzi 👋. Usipokuwa na emotional intelligence (EI) kubwa utaishi maisha ya wasiwasi, hasira, stress, nuksi na kuudhi watu; na utakuwa mgumu sana kupendeka.

Unapataje EI kubwa?
  • Kuwa na utulivu wa kiroho
  • Kupenda kujifunza mambo mapya
  • Kukubali kubadilika kulingana na wakati
  • Kusoma vitabu
  • Kutokujilinganisha na watu wengine
  • Kutambua kwamba kila mtu unayekutana naye ana matatizo anayopambana nayo; na pengine makubwa kuliko uliyonayo.
  • Kutokulalamika na kulaumu wengine.
  • Kutambua kwamba maisha yako ni jukumu lako 100%; na kwamba hakuna mtu aliyezaliwa ili aje akupe maisha mazuri (labda wazazi wako - kama bado wapo na bado uko under 18).
  • Kuwa mtu mwema; na kusaidia wengine.
  • Jenga familia/mahusiano yenye upendo
  • Jifunze kusamehe.
  • Jitambue na kujithamini; na usitake kupendwa na kila mtu
  • Kutambua kwamba mwisho wa yote kuna kifo kinakusubiri; na hizi hekaheka zote zitakoma.
Nadhani kwa sasa haya yanatosha. Tabia yangu ya kupenda kujifunza mambo na kuangalia watu katika upande chanya hivi karibuni ilinikutanisha na rafiki wa kipekee sana maishani mwangu. Polepole na kwa uvumilivu mkubwa pamoja na maumivu rafiki yangu huyu aliweza kunionyesha kwamba sikuwa sawa katika hilo eneo la emotional intelligence. Japo sikujua lakini kumbe nilikuwa ni mmoja wa wale watu wenye hasira za haraka haraka tu. Watu ambao jambo dogo tu wameshakasirika halafu baadaye wakipoa wanaanza kujuta (They hurt themselves more by trying to hurt others). Safari ya miaka mitatu hivi na rafiki yangu huyu kutoka kwa Mungu hatimaye imenitoa huko mpaka wanangu na wajukuu zangu wanasema "umekuwaje wewe?". Kusema kweli nimekuwa calm sana na siyo yule mtu wa kuona mlima kwenye kila tatizo hata kama tatizo lenyewe lina kimo cha kichuguu...and looking back sasa ninaweza kuona ni kwa nini hata baadhi ya mahusiano yangu huko nyuma hayakufanikiwa kwa sababu mimi sikuwepo kwenye mahusiano yale kwa jinsi mtu mwenye upendo wa kweli anavyopaswa kuwa. High emotional Intelligence inakupa uwezo wa kuliangalia jambo katika upana wake na kupima outcomes na consequences zake mbalimbali kabla hujaamua kulitolea uamuzi. Tena unafanya hivyo kwa hekima na busara. Matokeo yake ni amani ya kweli, utulivu wa fikra na mkong'osio wa roho na mwili. Total tranquility!

Asante sana rafiki yangu uliyejitolea miaka yako mitatu kusafiri nami na kutumia taaluma yako ya saikolojia ili kuhakikisha kuwa nimekuwa mtu mpya - baba bora kwa wanangu, rafiki wa kupigiwa mfano, binadamu mvumilivu, mtu anayejitambua, kiumbe anayependeka na.....
Maneno mazito kabisa kwa watu wenye iq zao ,asante
 
Amkeni,njoni chadema kwa wingi,tuwanyooshe Hawa wezi ccm.full stop
 
Inasikitisha kuona wenye umri tajwa au na zaidi hawayachukulii maanani haya mashauri
 
Back
Top Bottom