Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

Kosa la kwanza ni hili, kujimithilisha na wengine ama kuweka uhalisia fulani kwa ujumla.

Kila mtu ana formula na wakati wake wa kutoka. Kwa vile vijana wa kibongo bongo 99 hawatoboi kabla ya umri fulani inaweza ikawa wewe 100 ndio ukatoboa.

Maisha hayana formula moja kwa kila mtu. Kila mtu anatoka kwa channel yake, majaaliwa yake, juhudi zake na wakati wake.
Sahihi kbsa mkuu
 
3.ukimaliza na hayo hapo juu tafuta familia ya mke mmoja,aliye bikiria.
Ni pimbi tu ,ataenda kutoa mahali kwa mwanamke aliyekwisha tumika na wenzake,Binti amepigwa blowjob za kutosha hostel huko, wewe unaenda kumpigia magoti,acha huu ufala
Naona hii ya kuoa mabikra nayo inataka kuwa kama movement fulani hivi. Vijana sasa hamtaki kuoa mabinti waliokuwa wameolewa kwa ndoa bubu kwa miaka mitatu huko vyuoni; na mimba wakatoa? Kama mtaoa graduates, hao mabikra mtawapata wapi sasa? Hamjidanganyi tu? 😳
 
1) usichelewe kuanza kugegeda, mwenzenu nilianza na mia 25 katika ushamba wa mbususu ndio nikapata hiv
2) tafuta hela kwa nguvu zote na hakiisha hela hiyo unatumia kula mbususu
3) wanawake wote ni kenge na ni chombo cha starehe.
ukiwa na pesa wee just confuse them (wachanganye). Ukikosa watamukwepa kama ukoma.
4) mwanamke ni kenge asiekuwa na upendo wala shukran. Weka ndani at ur own peril.
5) usiache mwanamke kwa sababu amechepuka. Huo utoto hamna mwanamke mzuri asiechepuka. Muhimu anakupa mbususu na ikiwezekana mkaribishe huyo njemba nyingine mgonge 3some. There is something u will learn, ego aside plz.
6) kuajiriwa ni ungese ila fanya juu chini ukiajiriwa boss wako awe mzungu au mjapan. Hawa ndio waajiri wa kweli. Mwafrica muhindi mwarabu tunafanya kazi kwa sababu ya umaskini.
Hapo no.5 umetisha Sana mkuu ila ni upotoshaji WA kiwango cha juu sana
 
Mpendwa Mdogo wangu yafuatayo nimeona katika maisha yangu mpaka umri huu na huu ni ushauri wangu,kwa sababu mimi ni mwanaume nitakuambia ya kiume na kama baba mwenye watoto.

1.Maisha ni jinsi unavyo yachukulia, ukitaka yawe mepesi rahisisha mahitaji yako au ongeza kipato chako.
ukiwa kijana ukiyarahisisha kwa kuwa na viwango vya chini utalala sehemu rahisi unatakula rahisi,utasafiri kirahisi,utakojoa sehem rahisi(Elewa neno kukojoa) ila havitakua na ubora.
Ukiyarahisisha kwa kuongeza kipato ni kinyume chake,uta fanya vyote kwa gharama kiasi ila mara nyingi vitakua na ubora.(Elewa mara nyingi)

2.Ukioa utakua chanzo cha furaha ya mwenza wako au huzuni, wanawake wanahitaji muda na matunzo lakini pia hakikisho la kesho yake na watoto wake (Kama mtajaariwa watoto)
Furaha yako itatokana na maisha yako unavyotaka yawe sio mkeo

3.Kumbuka ibada,kwa imani yako( sali,jumuika na watu mtukuze muumba wako to sadaka) kwenye nyumba za ibada.

3.Ishi vizuri na watu, waheshimu wakubwa na wadogo,usiwe mwepesi kudharau watu hasa wazee mara nyingi shida huturudisha au kutupeleka kwa watu tulio wadharau.

4.Jiimarishe, uwe bora zaidi ya jana, fikiri tofauti zaidi ya jana, panga malengo zaidi ya mwaka jana

5.Kuwa mtu wa kiasi,Kunywa kiasi,cheka kiasi,Pumzika kiasi,jumuika kiasi,kuwa nanhuruma kiasi. Kula kiasi zungumza kiasi,uww na marafiki kiasi

6.Ngono ni Anguko la vijana wengi,Tafuta mwanamke mmoja unae mmudu,anaesikia,Ishi hapo,wanaume wengi wanamaliza hela kuchungulia sana wanawake.

7.Nunua Ardhi, hata kama ni nje ya mji,sio lazima Dar,hapo hapo ulipo kuna nje ya mji,ardhi inakua thamani kila siku.

8.Wapende wazazi wako,watoto wako na mkeo ukijaliwa,wahudumie

Legacy.
I love this 💯
 
78 yrs here speaking. Nitaandika kwa kirefu kidogo na kwa uwazi. Kama kijana mmoja atasaidika basi itakuwa poa sana!

Iko hivi. Kama unataka utoboe huku 65+ hakikisha una furaha, huna wivu wa ******* na usijilinganishe na mtu. Vinginevyo utaRIP mapema tu kwa kushambuliwa na moyo wako mwenyewe au harusi huko juu ubongoni. Unaipataje furaha? Nao liseni vere keafuli:

➡️➡️ 1. Linda sana afya yako. Asikudanganye mtu: Afya yako ndo kila kitu. Under 35 unaweza kujiona mwamba lakini hiki ndicho kipindi cha kuepuka presha, kisukari, matatizo ya moyo, baadhi ya saratani na magonjwa mengine mengi yasiyo ya kuambukiza huko mbele ya safari. Kati ya majuto makuu niliyonayo ni kunywa pombe sana na kuponda raha kupitiliza ukiwemo ulaji wa hovyo huko nyuma. Japo nimeweza ku-reverse karibu kila kitu kilichokuwa kimeanza kwenda mrama (pre-diabetic, BP, acute sleep apnea, obesity....) na kuwa sawa lakini imenigharimu sana (muda na mengineyo).

Kijana under 35:
  • Punguza au acha kabisa pombe
  • Kamwe usivute sigara wala kutumia ugoro
  • Ogopa sana sukari
  • Angalia usinenepe na kuwa futufutu.
  • Punguza caffeine (energy drink).
  • Angalia mlo wako
  • Anza kuangalia sukari, BP na lehemu.
  • Usitumie boosters za nguvu za kiume
  • Hakikisha hupati UKIMWI 📌📌📌
  • Mazoezi na lishe bora vitakupa uzee safi
  • Anza kujali afya ya ngozi yako ili kuepuka kuchakaa mapema (nione kama unahitaji msaada katika hili)
  • Ukijisikia hauko sawa nenda hospitali.
  • Tumia common sense kwenye kila kitu.
Kumbuka: Hiki ndicho kipindi cha kuweka misingi ya afya njema ukifika huku 45+. Na bila kuwa na afya njema huwezi kufurahia maisha. Kwa kifupi hakikisha huandai mazingira ya kuja kupata BP, kisukari na ishu zingine sugu huku mbele ya safari.

➡️➡️ 2. Uchumi: Hata kama hutakuja kuwa tajiri wa kupigiwa mfano lakini hakikisha una uwezo wa kupata mahitaji yako ya msingi bila kusumbua watu. Ukiumwa ujitibu. Ule cho chote unachotaka. Uende po pote unapotaka na ufanye cho chote unachotaka bila kutegemea misaada ya watoto wako, ndugu, jamaa, marafiki na wasamaria wema. Under 35 ndiyo kipindi kizuri cha kuanza kuweka misingi sahihi ya kuja kuwa na uzee wenye neema na mibaraka. Ukikichezea kipindi hiki, huku mbele kuna majuto makubwa yanakusubiri kmmk!

➡️➡️3. Kua kihisia - Emotional Intelligence (EI). Usipokuwa na emotional intelligence kubwa maisha yatakuendesha maana kila kitu kwako ni crisis ushapaniki presha iko juu unataka kufa. Hii itakusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuchukulia mabaya yanayokutokea (zikiwemo hekaheka za mapenzi) kama sehemu muhimu ya maisha maana maisha bila hekaheka na amsha amsha yanaboa kishenzi 👋. Usipokuwa na emotional intelligence (EI) kubwa utaishi maisha ya wasiwasi, hasira, stress, nuksi na kuudhi watu; na utakuwa mgumu sana kupendeka.

Unapataje EI kubwa?
  • Kuwa na utulivu wa kiroho
  • Kupenda kujifunza mambo mapya
  • Kukubali kubadilika kulingana na wakati
  • Kusoma vitabu
  • Kutokujilinganisha na watu wengine
  • Kutambua kwamba kila mtu unayekutana naye ana matatizo anayopambana nayo; na pengine makubwa kuliko uliyonayo.
  • Kutokulalamika na kulaumu wengine.
  • Kutambua kwamba maisha yako ni jukumu lako 100%; na kwamba hakuna mtu aliyezaliwa ili aje akupe maisha mazuri (labda wazazi wako - kama bado wapo na bado uko under 18).
  • Kuwa mtu mwema; na kusaidia wengine.
  • Jenga familia/mahusiano yenye upendo
  • Jifunze kusamehe.
  • Jitambue na kujithamini; na usitake kupendwa na kila mtu
  • Kutambua kwamba mwisho wa yote kuna kifo kinakusubiri; na hizi hekaheka zote zitakoma.
Nadhani kwa sasa haya yanatosha. Tabia yangu ya kupenda kujifunza mambo na kuangalia watu katika upande chanya hivi karibuni ilinikutanisha na rafiki wa kipekee sana maishani mwangu. Polepole na kwa uvumilivu mkubwa pamoja na maumivu rafiki yangu huyu aliweza kunionyesha kwamba sikuwa sawa katika hilo eneo la emotional intelligence. Japo sikujua lakini kumbe nilikuwa ni mmoja wa wale watu wenye hasira za haraka haraka tu. Watu ambao jambo dogo tu wameshakasirika halafu baadaye wakipoa wanaanza kujuta (They hurt themselves more by trying to hurt others). Safari ya miaka mitatu hivi na rafiki yangu huyu kutoka kwa Mungu hatimaye imenitoa huko mpaka wanangu na wajukuu zangu wanasema "umekuwaje wewe?". Kusema kweli nimekuwa calm sana na siyo yule mtu wa kuona mlima kwenye kila tatizo hata kama tatizo lenyewe lina kimo cha kichuguu...and looking back sasa ninaweza kuona ni kwa nini hata baadhi ya mahusiano yangu huko nyuma hayakufanikiwa kwa sababu mimi sikuwepo kwenye mahusiano yale kwa jinsi mtu mwenye upendo wa kweli anavyopaswa kuwa. High emotional Intelligence inakupa uwezo wa kuliangalia jambo katika upana wake na kupima outcomes na consequences zake mbalimbali kabla hujaamua kulitolea uamuzi. Tena unafanya hivyo kwa hekima na busara. Matokeo yake ni amani ya kweli, utulivu wa fikra na mkong'osio wa roho na mwili. Total tranquility!

Asante sana rafiki yangu uliyejitolea miaka yako mitatu kusafiri nami na kutumia taaluma yako ya saikolojia ili kuhakikisha kuwa nimekuwa mtu mpya - baba bora kwa wanangu, rafiki wa kupigiwa mfano, binadamu mvumilivu, mtu anayejitambua, kiumbe anayependeka na.....
Mkuu shukrani kwa madini haya.

Suala la kutunza ngozi inakuwaje sasa hapo, tunalimalia vp?

Tunaombaa muongozo wako.
 
1.kitu cha muhimu kutafuta ni afya Bora,physica,psychological,social
2.Kitu Cha pili cha kutafutq ni maarifa sahihi kuhusu kutafuta pesa,yaani hata kama umeajiriwa serikalini usiende kusoma kuwatishia wenzako,nenda kusoma ili uongeze income,opportunity etc
3.ukimaliza na hayo hapo juu tafuta familia ya mke mmoja,aliye bikiria.
Ni pimbi tu ,ataenda kutoa mahali kwa mwanamke aliyekwisha tumika na wenzake,Binti amepigwa blowjob za kutosha hostel huko, wewe unaenda kumpigia magoti,acha huu ufala
4.Uwekezaji,hata ulipwe milioni 20,ama ufanya biashara update faida ya milioni 100,kama hauwekezi kwenye Bonds,real estate,Stocks,Kuna siku utakuja kua masikini tena ombaomba mkubwa sana
5.ukifanikiwa kupata watoto walee ili waje wapambane na Dunia,na sio uwalee kwa kuwarahisishia changamoto za Dunia
Ukifanya hayo hapo kabla haujafika 35 utaweza kutatua 95% ya matatizo ambayo vijana na wazee huyapata
Eti Binti amepigwa blowjob za kutosha hostel huko, wewe unaenda kumpigia magoti,acha huu ufala😂😂😂🙌🙌🙌
 
Hapo no.5 umetisha Sana mkuu ila ni upotoshaji WA kiwango cha juu sana
Najua binadamu hasa wanaume hatupendi wanawake zetu kugo gwa ila ukweli ni kwamba wanagongwa sana tuuu. Sasa the choice is urs to accept reality or live in denial.
 
1) usichelewe kuanza kugegeda, mwenzenu nilianza na mia 25 katika ushamba wa mbususu ndio nikapata hiv
2) tafuta hela kwa nguvu zote na hakiisha hela hiyo unatumia kula mbususu
3) wanawake wote ni kenge na ni chombo cha starehe.
ukiwa na pesa wee just confuse them (wachanganye). Ukikosa watamukwepa kama ukoma.
4) mwanamke ni kenge asiekuwa na upendo wala shukran. Weka ndani at ur own peril.
5) usiache mwanamke kwa sababu amechepuka. Huo utoto hamna mwanamke mzuri asiechepuka. Muhimu anakupa mbususu na ikiwezekana mkaribishe huyo njemba nyingine mgonge 3some. There is something u will learn, ego aside plz.
6) kuajiriwa ni ungese ila fanya juu chini ukiajiriwa boss wako awe mzungu au mjapan. Hawa ndio waajiri wa kweli. Mwafrica muhindi mwarabu tunafanya kazi kwa sababu ya umaskini.
mweee, nime chukua namba 6 tu 😂😂
 
Back
Top Bottom