Ma brother wa miaka 35+ hebu tupeni wadogo zenu, ushauri wowote wa kuhusu maisha

Tafuta guru , mentor, tafuta connection kwenye industry yeyote nenda dedicated muda wako fanya kwa bidii..miaka miwili mitatu copy idea anzisha chako hata kwa udogo jipe Long term plan na short term plan KAZAA

Kama una kipaji talent fulani tafuta upenyo tobo lipo Kama MIMI NISINGE KUA NAFANYA HICHI NACHO KIFANYA BASI KWENYE MGUU WANGU WA KUSHOTO MUNGU ALIWEKA KIPAJI CHA AJABU CHA KUSAKATA KABUMBU.

Mimi kwa enzi zetu nili udharau mpira wa miguu by then ulikua haulipi Kama Sasa ☺️

Kama vipi fuata ushauri wa PM wahitimu wa degree waende veta kua na bidii ya Maisha mwombe MUNGU akujalie afya na nguvu.. EVERYTHING IS POSSIBLE UNDER THE SUN.
 
Dah ona Sasa ume kuja kujibu ujinga wako, we mwenyewe chawa
Gentleman,
nimetoa ushauri wa bure kabisa,
na ni kwa neema na baraka alizonijalia Mungu,

Mimi nimepewa kipawa hicho bure na Mungu, nami sina hiyana nimeona hakuna haja ya kuwatoza chochote wananchi wangu ambao wengi ndio kwanza mnajitafuta tena katika hali ya unyonge sana kiuchumi,

niwatie moyo tu na kuendelea kuwashauri kwamba
kujikwamua kutoka kwenye unyonge wa kiuchumi mnaoupitia ni lazima, sio hiyari kufanya maamuzi magumu na kuchukua hatua ya kusonga mbele bila mbambamba
 
1: Kamwe usimuamini mwanamke kuhusu uchumi na afya ya akili inategemeana ukizingatia hili

2:Epuka makundi ikibidi uishi kama upo kwenye kisiwa hata kivuli chako usikiamini ila usijiweke wazi maana shetani wa mtu ni mtu

3: Mungu yupo ridhika na maisha usiwake tamaa, jikubali , msiigize maisha hakika ishi maisha yako

4: Hakuna mtu atakuwekea hela ya bure mfukoni au kukupa chakula cha bure pambana jipatia hata kidogo chochote kitu halali

5: Usikope kumbuka ukikopa unakua mtumwa wa anaekudai amini kwenye haba na haba hujaza kibaba ishi kwa kudunduliza

6: Usichelewe kuoa na ukioa ishi na mkeo kama dada wa kazi ila usimuonyeshe maana watoto atakao kuzalia ndiyo ndugu zako halali na wakati mwingine watatumika kukuangamiza

7: Kamwe usieleweke kwa mtu yeyote yule na siku zote usiwe mjuaji kua mtu wa kujifunza kila siku. Pia kua mwepesi wa kusikia lakini mzito wa kutoa majibu / ushahidi

8: Maisha ya mwanaume ya uzeeni ni ya tabu sana jenga maisha yako ya uzeeni sasa hata kama utakufa kesho ili uje kua hadithi nzuri
 
Age is nothing but a number

Hustle
Work hard & smart
Spread positive Energy

Love money but spend it wisely
Health is wealth don't ruin ur health , mantain physical exercises , balance diet .

Enjoy, because life is about balance.
Cha kuongezea hapo kwenye
"love money but spend it wisely"
Cheza na mshahara, ila usicheze na kaziπŸ™
 
Jipende kabla ya kupenda mtu. (Mfano: Usimpeleke Mtu kfc kama hujawahi kwenda. Usimpe mtu hela yako. Usimkopeshe mtu hela kama unajua akikudhurimu hiyo hela itakuuma.

Rudi nyumbani saa kumi na mbili na usitoke nje tena kama kazi zako si za usiku. Kama za Usiku rudi nyumbani mapema.

Usichangie harusi yoyote. Ukitaka kumpa mpenzi wako hela, hakikisha unamtumia mzazi wako hela sawa na uliyotoa kwa mpenzi wako.

Famya yote ila mtoto wako ndo ndugu yako.

Usiache kufanya ibada kulingana na imani yako.

Ishi maisha yako bila kujali watu watasema nini. Muhimu usiige maisha ya mtu mwingine.

Kumbuka: Adui yako ni yule wa karibu yako. Hakikisha siri za maisha yako zinabaki kuwa zako.

Mwisho kaa ukijua Mwanamke ni pasua kichwa. Ishi naye kwa akili ukijua hivyo. Sio akikukera kidogo unaanza kulialia. Ni kawaida yao kukera kuudhi na wakipata nafasi nzuri wanadhuru. Mia
 
Siyo 35+ ila ushauri wangu:

1. KATAA NDOA

2. Jifunze kuhusu pesa (financial literacy)

3. Tengeneza mahusiano yenye tija na maana, kwenye circle yako wakuzunguke watu wa maana kabisa. Iwe mapenzi, urafiki au kazi.

4. Ilinde afya yako ya akili na mwili kuliko kitu chochote kile, hapo ndiyo points 3 zilipo.

5. Kuwa mvumilivu. Hakuna mafanikio ya kulala masikini na kuamka tajiri.

6. Jifunze zaidi: ongeza ujuzi, safiri nje ya mipaka kuijua Dunia, watu, na tamaduni zao.

7. Experiences over Possession.
 
Yan baba mkwe, unaniambia niendelee kupiga nyere* na huu umri wangu miaka 35 kweli
 
Miaka 35 unaona mingi kwakuwa mnakula na kulala bure kwa shemeji, siku mkianza kujitegemea mtajua 35 ni namba tu !
 
Sasa mkuu, wakati huu unafanya nini? Haja unamalizaje?
Maana yake usiingie kwenye committed relationship, yaani ile kubeba wajibu wa baba au mume kwenye mahusiano. Kaa kijanja janja yaani ile kula kimasihara, one night stand, ile demu akokiletea mizinga unaipangua kidiplomasia na mambo kama hayo
 
Mkipata vihela baada ya kumpiga muhindi huo ushauri wenyewe huwa mnauzingatia sasa.
 
1. Jali afya yako sana.
a) Tumia zana kwa kila tendo.
b) Usitumie bangi, sigara, au mihadarati
c) Tunza afya ya akili kwa kujiweka mbali
na mtu au chochote cha kukuvuruga
d) Usipige nyeto
e) Fanya mazoezi uwe fit

2. Fanya kazi yoyote ya halali kwa nguvu zako zote na maarifa yako yote.

3. Tunza kibunda chako kwa kuwekeza zaidi.

4. Kama unasoma soma kwa bidii zote. GPA kubwa ni muhimu.

5. Kama kuna uwezekano wa kuoa bila kuleta changamoto yoyote ya kiuchumi OA. KUOA MAPEMA NI BORA ZAIDI KULIKO KUCHELEWA.

6. Fuata njia zako mwenyewe. Usiangalie watu wengine wanavyofanya.

7. Waheshimu watu wote bila kujali rika, elimu, hadhi, utajiri, umaskini au lolote lile.

8. Jizuie kupanda bodaboda kadiri uwezavyo.

9. Sio muhimu sana ila jitahidi uwe na Passport pamoja na kadi ya uanachama CCM.

10. Wakosee watu wote ila chunga sana kutowakosea wazazi wako (baba na mama). Ikitokea umeteleza haraka sana waombe msamaha.

11. Kaa mbali na CHADEMA. Watakupora kibunda chako kupitia michango yao ya kipuuzi.
 
Uzi wameitwa mabroo, wewe mama umefata nini hapa.
 
Maana yake usiingie kwenye committed relationship, yaani ile kubeba wajibu wa baba au mume kwenye mahusiano. Kaa kijanja janja yaani ile kula kimasihara, one night stand, ile demu akokiletea mizinga unaipangua kidiplomasia na mambo kama hayo
I got your point sipo mbali kwenye kula kimasihara! Message za vizinga. Huwa najibu tu okay Ila waga sitekelezi maombi yao mfano Huyu
 

Attachments

  • Screenshot_20250319_183336.jpg
    213.8 KB · Views: 36
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…