Maadhimisho na Kilele cha Usomaji Quran kufanyika Siku ya Pasaka ni Dharau na Uchokozi kwa Wakristo au ni Utaratibu tu?

Sioni dharau wala uchokozi wote. Ya waislamu yanamhusu vipi mkristo na kinyume chake? Hawaji kunibughudhi kanisani wala nyumbani kwangu na mimi siwaingilii msikitini au popote wanapofanya shughuli yao.
 
Acheni kila mtu aamini kile anacho kiamini, ningewaona mna akili iwapo mnge hamasisha kufungwa kwa mabaa na sehemu za starehe siku hiyo ili watu wasisherekee kwa kulewa na kufanya uzinzi kitu kinacho haribu dhana na maana nzima ya pasaka hiyo ndo maana ya kuiheshimisha pasaka na sio ngonjera zako hizo.
 
Umejibu vizuri sana kiungwana
 


Hiyo "busara" unayoitaka ni religious compromise, na kamwe haitawezekana kuwepo na compromise ya aina hiyo, kila dini inayo mafundisho na taratibu zake na haitakiwi iingiliwe na taratibu za dini nyingine, Wakristo mnayo Pasaka yenu na Waisilamu wanayo siku yao ya kusoma Qur'an na wao wenyewe wataamua ni siku gani Qur'an isomwe na nani awe ni mgeni rasmi, na kwa kufanya hivyo hawajavunja heshima ya kitu chochote.

Sasa hoja yenye mashiko ambayo ni Common kwa dini zote mbili ni swali hili; je Pasaka na Usomaji wa Qur'an unayofaida gani kwa WATU wote??? (Hizi dini ni kwa ajili ya watu wote, haya ni madai ya hizo dini).

Kama usomaji wa Qur'an ni kwa ajili ya watu WOTE basi hapo ndipo hiyo "Busara" ingetumika kupisha kwanza sikukuu ya Pasaka ipite na Waisilamu nao siku hiyo wapate nafasi ya kupata mafundisho ya kiimani kuhusu pasaka ili nao ikibidi siku moja wawe wakristo, hivyo pasaka ni mahubiri.

Ni jambo hilo hilo kwa Waisilamu kuhahirisha siku ya kisomo cha Qur'an ili kuwapa nafasi Wakristo kujumuika kupata Baraka za kisomo na hata ikibidi kama kuna mkristo atakayevutiwa na uisilamu basi anayo hiyari ya kusilimu.

Hiyo ndio logic na busara ya; kwanini Waisilamu Waahirishe siku ya kusoma Qur'an isiingiliane na sikukuu ya Pasaka kinyume na hiyo logic hukutaweza kamwe kuwepo compromise ya aina yoyote kwani dini hizi kimsingi kila moja ipo kivyake.

Cc: GENTAMYCINE
 
Mbona hakuna muingiliano wowote? Waislam watadeal na qur an na wakristo watadeal na pasaka. Mbona kwaresma na Ramadan vimeingiliana na hakuna shida yoyote
 
Exactly.
 
Ndio ukweli, hakuna ubaguzi kabisa. Nakumbuka tumesoma shule ya inaitwa Muslim school, lakini kulikuwa na waalimu wakristo, wengine ni masister, hawa walikuwa hata kuwachapa wanafunzi, hawawachapi, wanakaa na sisi wanafunzi waislamu kiuzuri kabisa.
 
Mbona hakuna muingiliano wowote? Waislam watadeal na qur an na wakristo watadeal na pasaka. Mbona kwaresma na Ramadan vimeingiliana na hakuna shida yoyote
Umemaliza mjadala,hoja zako ni za kisomi.
 
Hawa jamaa huwa siwaelewi kabisa, wakitokea hapo wanasema waislam wanapenda kulalamika Sasa sijui wanachokifanya hapa ni nini kama sio malalamiko tena yasiyo na msingi
 
Acha uchizi wenyewe wanakwambia mashindano wewe unasema ibada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…