Maafisa usafirishaji hii tabia yenu ya kujifanya hamna chenchi iacheni

Maafisa usafirishaji hii tabia yenu ya kujifanya hamna chenchi iacheni

Kumbe ndo tabia yao! Kuna mmoja nili bolt juzi sema nilimsimamisha dk kadhaa maan aliwahi kufika, tulivyofika akasema dada bado mia 5 hapa sina nitakutumia kwenye account yako nikamwambia tu haina haja.
Ndio tabia zao kwasasa jaribu kufuatilia itatokea tena kama hivyo.
 
baada ya kujua hilo kama natumia boda kabla sijatoka kituoni ananipa chenji yangu kabisa alafu tunaanza safari ili tukifika asije akaanza siasa
Hapo utakuwa umemuweza, wengine wanaishia kulalamika kuwa ungemtaarifu mapema kama huna ela ya chenji ili apite sheli.
 
Mkuu mda mwingine waachie tu hata ya maji., ni wapambanaji,,,, ! Mm kuliko kumpa lofa hela yangu aliekaa tu kijiweni eti niungie lijero, bora nimpe mpambanaji anaejiongeza !
Mimi huwa nawaachia wale wanaokubali bei kwenye ku bargain. Anasema buku 6 namwambia 5. Huyu akikubali lazima nimuachie hiyo buku ama buku 2 kbs.

Nawapenda sana wapambanaji wasiotaka pesa iwapite. Lkn wale mabrazamen unakuta wanawasikizia wengine huwa wanakoma.

Kuna siku wakanimaindi broo unakomaa kupunguza afu umifika mwisho unatoa hadi zaidi.

Mie huwajibu nalipa fadhira kwa yule anayekuwa tayari kusasidia. Ili wajifunze muda mwingine kusaidia hata wale wenye nauli pungufu, maana hujui anapitia shida gani.

Mbona mademu huwa mnawafuata bure tu, ama mnawapeleka kisa tu demu wako ama unamfukuzia.
 
Back
Top Bottom