Maafisa usafirishaji hii tabia yenu ya kujifanya hamna chenchi iacheni

Maafisa usafirishaji hii tabia yenu ya kujifanya hamna chenchi iacheni

hao wasomi walipotosha, ilikuwa ni kujipendekeza kisiasa kwa wahuni hao wakawaita ni maofisa wakati ni wahuni tu wa kijiweni
Ni maafisa mkuu, hayo majina mengine ni ya kuwatofautisha kulingana na vyombo vyao
 
Ni maafisa mkuu, hayo majina mengine ni ya kuwatofautisha kulingana na vyombo vyao
sasa tukianza kuwaita wahuni wa kijeweni ni maofisa basi itabidi na wengine tuwape hadhi na heshima hiyo. Dada poa na jamii zao zote za biashara ya ngono tutawaita maofisa biashara ya ngono, maofisa kubeti, church/masjid officers, ofisa umachinga, maofisa wajasiria mali hali kadhalika kwa mtindo huo tutakuwa na wakurugenzi wao katika vijewe vyao
 
Kwani sifa za kuwa ofisa ni zipi mkuu
 
TUKUPE CHENCHI HALAFU SISI TIPU TUTAPATA WAPI?
tipu zipo tu na mnazipata sana msifosi kuzipata kuna muda abiria tuna bajeti ngumu ikipelea hata 500 ni changamoto. Kwa mfano mimi huwa napenda kutoka na hela ikiwa nimeshaipigia hesabu yote ya mizunguko yote ya siku kwahyo nikipunguza inanigharimu.
 
Mi huwa nawaambia kabla sijapanda ili kama hana aombe kwa wenzie au sheli.
 
Habari wakuu.

Kuna tabia nimeiona kwa hawa maafisa usafirishaji hasa bodaboda na bajaji, ndani ya wiki 2 nimetumia sana usafiri wao ukifika mwisho wa safari ukampa hela inayohitaji kurudi chenchi hasa tsh 500 & 1000 wengi wanasema hawana ila ukiwakazia watafute chenchi utaona kaingia mfukoni na kukupa chenchi kamili. Huu ni usumbufu na kupotezeana muda.

Na wengine sio wastaarabu kabisa, mtu anakukasirikia kabisa, chenchi hana yeye alafu anakuwakia. Jukumu la kutafuta chenchi sio la abiria, jukumu la abiria ni kuhakikisha amelipia huduma basi.

Hii tabia sio nzuri, sijui wanaona hicho kiasi cha pesa ni kidogo sana, kwa wanaotumia usafiri huo kwa zaidi ya mara 5 kwa siku ni hasara. Badilikeni hela ngumu.

NAWASILISHA.
Sasa unabembeleza nini jikatae na hela yote uone kama hatatoa chenchi
 
Mkuu mda mwingine waachie tu hata ya maji., ni wapambanaji,,,, ! Mm kuliko kumpa lofa hela yangu aliekaa tu kijiweni eti niungie lijero, bora nimpe mpambanaji anaejiongeza !
Wewe waachie ****** pesa za tabu uwaachie kwani kanibeba bure
 
Aisee👿
Huo ndio ukweli. Katika dunia ya sasa, mara nyingi wanaofanikiwa zaidi ni wale walio na uthabiti wa moyo, hasa katika kusimamia rasilimali. Pia wenye roho za kuto kutoa toa rasilimali ikiwamo pesa!

Ukiwa na huruma kupita kiasi bila kuwa makini, unaweza kujikuta ukiachwa nyuma. Sasa wewe kila anaekulilia ushamgea hela!!! Eboo wewe kufanikiwa kifedha ni usahau.

Utafutaji wa mali leo umejaa ushindani mkali—ambapo unyonyaji hufanyika bila kujali utu.

Kumbuka ubepari ni mfumo unaoficha ukatili wake nyuma ya upatikanaji wa mali, ndiyo sababu nchi za magharibi zina ukwasi wa kutosha na mali pia na ndizo zinatawala dunia kimaamuzi!!!.

Tafuta hela ila kumbuka utafutaji wa hela na utu havikai pamoja.

​

Back
Top Bottom