Maandamano makubwa ya kudai maji Dar es Salaam

Katika zunguuka yangu vijiweni Dar es salaam, Wananchi wanahasira kali sana juu ya ukosefu wa maji Jijini.

Wananchi wanasema Maji wakati mwingine yanakosekana kwa wiki nzima.

Kinachowakera zaidi ni kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa sana kununua maji na hivyo kufanya maisha yao kuwa magumu maradufu.

Wananchi wanasema, Wameivumilia serikali kwenye mambo mengi sana ikiwemo kuvuruga uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2019, Kuvuruga uchaguzi mkuu, Kuwatoza tozo kubwa, Ukatili wa kisiasa, Kuendesha zoezi la wamachinga kihuni. Sasa wanasema hili suala la Maji limewafika shingoni hali ni mbaya.

Inadaiwa Wananchi wanazungumza uwezekano wa kufanya maandamano makubwa ya kudai maji nchini.

Wananchi wanakumbushia kuwa kwenye rasimu ya Warioba MAJI ILIKUWA NI HAKI YA MSINGI ya mwananchi, wanasema kuwa kukataa katiba mpya maana yake ni kukataa wananchi wasipate hayo maji.

Katika mazungumzo yao, wananchi wanasema wanahitaji majibu ya suala la maji haraka sana la sivyo watatoka barabarani na ndoo za maji na magudulia ikiwa ni ishara ya kuonyesha kudai maji!

Wazazi wanalalamika watoto wanaenda shule bila kuoga, Watu wanalalamika wanashindwa kujisitiri chooni vyema sababu ya maji. Watu wanahoji hii nchi ni nchi ya namna gani?

Wakati huo wanahoji, Inakuwaje serikali inatumia matrilioni ya hela kununua ndege halafu inashindwa kujenga miundo mbinu bora ya maji kwa ajili ya jiji la watu milioni 8?

Haya mdogomdogo tutafika. Serikali ijiabdae kwa majibu, Mabomu ya machozi, virungu na bunduki havitoweza kuzuia watu wenye kiu!
Kama maji hakuna wanywe bia, unaleta porojo wakati watu wengi siku zote wanategemea visima binafsi.
 
Ole wenu narudia ole wenu!
Wana daslam Naona mnacheza na moto Kwa kuleta chokochoko na vile maji hakuna mtaungua bila vipoozeo!
(In kamanda mroto voices)
😁😁😁😁
Hata mroto angependa nguvu kazi ya taifa wapate maji kuliko kunuka mtaani.
 
hayo ni maneno tu..hakuna atakayetoka barabarani

tulianza na tozo, mara umeme na sasa maji

hamna lolote, ni makelele tu yanapigwa
 
Hivi we unaweza kuandamana wewe? Hao viongozi wanao itishaga maandamano wenyewe ikifika siku ya kuandamana wanatoroka nchini
 
Katika zunguuka yangu vijiweni Dar es salaam, Wananchi wanahasira kali sana juu ya ukosefu wa maji Jijini.

Wananchi wanasema Maji wakati mwingine yanakosekana kwa wiki nzima.

Kinachowakera zaidi ni kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa sana kununua maji na hivyo kufanya maisha yao kuwa magumu maradufu.

Wananchi wanasema, Wameivumilia serikali kwenye mambo mengi sana ikiwemo kuvuruga uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2019, Kuvuruga uchaguzi mkuu, Kuwatoza tozo kubwa, Ukatili wa kisiasa, Kuendesha zoezi la wamachinga kihuni. Sasa wanasema hili suala la Maji limewafika shingoni hali ni mbaya.

Inadaiwa Wananchi wanazungumza uwezekano wa kufanya maandamano makubwa ya kudai maji nchini.

Wananchi wanakumbushia kuwa kwenye rasimu ya Warioba MAJI ILIKUWA NI HAKI YA MSINGI ya mwananchi, wanasema kuwa kukataa katiba mpya maana yake ni kukataa wananchi wasipate hayo maji.

Katika mazungumzo yao, wananchi wanasema wanahitaji majibu ya suala la maji haraka sana la sivyo watatoka barabarani na ndoo za maji na magudulia ikiwa ni ishara ya kuonyesha kudai maji!

Wazazi wanalalamika watoto wanaenda shule bila kuoga, Watu wanalalamika wanashindwa kujisitiri chooni vyema sababu ya maji. Watu wanahoji hii nchi ni nchi ya namna gani?

Wakati huo wanahoji, Inakuwaje serikali inatumia matrilioni ya hela kununua ndege halafu inashindwa kujenga miundo mbinu bora ya maji kwa ajili ya jiji la watu milioni 8?

Haya mdogomdogo tutafika. Serikali ijiabdae kwa majibu, Mabomu ya machozi, virungu na bunduki havitoweza kuzuia watu wenye kiu!
Wakiandamana uje unitag,
 
Unazungumzia Watanzania sisi au "wa kufikirika"?

Unadhani kuna mtu ataenda kuandamana akiona FFU wenye mitutu na maji ya kuwasha na wajeda wakiwa barabarani "wanafanya usafi"? Labda Tz ingine !!

Hayo Maji wanayotumia kujaza kwenye Magari ya kuwasha bora wangeyatumia kuwapa wananchi.
 
Hivi we unaweza kuandamana wewe? Hao viongozi wanao itishaga maandamano wenyewe ikifika siku ya kuandamana wanatoroka nchini
Kwenye mambo ya msingi usiangalie fulani na fulani wameandamana au la. Jiangalie wewe kama wewe, Jambo likikugusa andamana, ila kama unaona ni upuuzi basi acha
 
Andamana sasa au nisikupangie muda wako wa kwenda kuandamana?
 
🤣 🤣 🤣 Watanzania sisi? wakuandamana? Sisi tunajuwa kuunga mkono juhudi tu.
 
Wako sahihi kabisa. Huwezi kutumia zaidi ya trilioni moja kuendelea kununua ndege wakati basic needs za watu wako zimekushinda kutimiza. Hii ni dharau.
Kweli serikali inatakiwa kuwa transparency kwa mambo inayofanya!

Order za ndege za miaka nenda rudi zimekuja kuhusianishwa na mgao wa maji wa leo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika zunguuka yangu vijiweni Dar es salaam, Wananchi wanahasira kali sana juu ya ukosefu wa maji Jijini.

Wananchi wanasema Maji wakati mwingine yanakosekana kwa wiki nzima.

Kinachowakera zaidi ni kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa sana kununua maji na hivyo kufanya maisha yao kuwa magumu maradufu.

Wananchi wanasema, Wameivumilia serikali kwenye mambo mengi sana ikiwemo kuvuruga uchaguzi serikali za mitaa mwaka 2019, Kuvuruga uchaguzi mkuu, Kuwatoza tozo kubwa, Ukatili wa kisiasa, Kuendesha zoezi la wamachinga kihuni. Sasa wanasema hili suala la Maji limewafika shingoni hali ni mbaya.

Inadaiwa Wananchi wanazungumza uwezekano wa kufanya maandamano makubwa ya kudai maji nchini.

Wananchi wanakumbushia kuwa kwenye rasimu ya Warioba MAJI ILIKUWA NI HAKI YA MSINGI ya mwananchi, wanasema kuwa kukataa katiba mpya maana yake ni kukataa wananchi wasipate hayo maji.

Katika mazungumzo yao, wananchi wanasema wanahitaji majibu ya suala la maji haraka sana la sivyo watatoka barabarani na ndoo za maji na magudulia ikiwa ni ishara ya kuonyesha kudai maji!

Wazazi wanalalamika watoto wanaenda shule bila kuoga, Watu wanalalamika wanashindwa kujisitiri chooni vyema sababu ya maji. Watu wanahoji hii nchi ni nchi ya namna gani?

Wakati huo wanahoji, Inakuwaje serikali inatumia matrilioni ya hela kununua ndege halafu inashindwa kujenga miundo mbinu bora ya maji kwa ajili ya jiji la watu milioni 8?

Haya mdogomdogo tutafika. Serikali ijiabdae kwa majibu, Mabomu ya machozi, virungu na bunduki havitoweza kuzuia watu wenye kiu!
Hivi kwanini hakuna viongozi viona mbali kiasi cha kujenga "dam" katika mto Ruvu kama "reserve" ya maji na kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa vyanzo cha maji Dar?

Miundo mbinu ya namna hiyo imejengwa mahali ambapo hapana uhakika wa mtiririko wa maji kwa mwaka mzima na wakafaulu.

Dar miaka nenda rudi kutegemea maji tiririka ya mto na mabadiliko haya ya tabia nchi ni majanga.

viona mbali hawana nafasi kupata uongozi Bongo.

upigaji, ujanja ujanja, uhuni na yule Mh Kishimba anasema Utoro oyee!
 
Hoja ilikuwa hivi
Maendeleo ya watu
Maendeleo ya vitu

Nani alikuwa sahihi
 
Mbadilike Wenyewe Kwa Kujali mambo ya Msingi Maji Kila mtu atunze Chanzo
Na wewe ubadilike. Tozo udai wananchi halafu lawama ya ukosefu wa maji uwape wananchi. Kazi ya serikari ni nini?. Wizara ya maji na taasisi zote zinafanya nini.
 
Eti hizi ndizo akili za Chadema!! Chama kimeishiwa mikakati mpaka kinatia huruma. Haya itisha maandamano hayo tuone kama utapata hata watu 10.
Shida ya wananchi mnawachukulia Chadema sio watanzania. Mtu ametoa wazo la ukosefu wa maji, wewe badala ya kuangalia tatizo linalosemwa unaangalia chadema. Mna hasira na chadema mpaka mnakufuru. Asilimia 95 ya madiwani wabunge na wenyeviti wa mtaa ni CCM , lakini kutatua mgao wa maji na umeme wameshindwa. Halafu wewe unakuja hapa unaisema chadema kwa lipi na mwenye mamlaka unamwacha.

Mnaenda kununua ndenge kwa trilioni, wakati mji mkuu wa kibiashara hauna maji pamoja na tozo wanazochukua. Achana na chadema shughulika na mambo yako. Kama chadema inatia huruma achana nayo , baki na ccm inayokutoza tozo na maji inakupa kwa mgao. Furahia na ushangilie. Leave chadema alone hujui kimepitia mangapi. Makamu mwrnyekiti alipigwa risasi, ikawa haitoshi wamemshtaki mwenyekitk kwa ugaidi and then unajifanya huoni unawatukana. Ulaaniwe milele na milele.
 
Back
Top Bottom