Pre GE2025 Maandamano ya CHADEMA kuanzia Mbezi Mwisho na Buguruni hadi Ofisi za UN

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Maandamano ya Jumatano, Januari 2024, yataanza Saa 3:00 asubuhi. Yatahusisha njia mbili kuanzia Mbezi Mwisho (Stand) na Buguruni, na yataishia Ofisi za UN, barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam.

Nakala za barua za taarifa ya Maandamano haya zimepelekwa kwa makamanda wote wa Polisi Wilaya, pamoja na Mkuu wa kanda ya Polisi Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, kumalizia maandamano ofisi za UN ni kwa sababu UN inao wajibu na nafasi ya kuchukua hatua kwa kadri itakavyoona inafaa.

Kuhusu suala la mjadala, Mnyika amesema tayari walifanya mdahalo na CCM kwa mwaka mzima na haoni mantiki ya kuendelea kupoteza muda zaidi hivyo wakutane barabarani.

Mnyika amefafanua pia majibu ya maswali ya CHADEMA yanapaswa kutolewa na viongozi wakubwa kama, amewaasa wananchi kutokukubali kuhamishwa kwenye hoja.

Pia, ameelezea kuwa CHADEMA ni chama kinachoamini katika kubana matumizi na kuwa na Serikali ndogo, hoja aliyoitoa kuhusu idadi ya wabunge wawili (Me na Ke) kila jimbo imetoka kwenye Rasimu ya Warioba ambayo ukiisoma utagundua kuwa idadi ya wabunge itapungua kwa kuwa watatokea kwenye Halmashauri za Wilaya (wabunge 278 tu) badala ya Sera ya sasa ya Majimbo ambapo kuna wabunge zaidi ya 370.

Your browser is not able to display this video.

===

Pia soma: CHADEMA yatangaza Maandamano Kupinga Miswada ya Sheria za Uchaguzi iliyowasilishwa Bungeni
 
Acheni kutuharibia Tanzania yetu nyie CDM. Kama mnataka andamabeni peke yenu. Waacheni waTanzania waendeshe shughuli zao za kiuchumi. Nyie ni sisimizi tu wala hamuwezi kubadili kitu kwenye mambo ya nchi hii. Kama hamna shughuli semeni tuwaonyeshe fursa.
 
Watapitia barabarani au wataandamana porini.

Barabara zipo Kwa ajili ya shughuli za Kiuchumi sio maandamano.

Halafu barabara zote wamechagua ni zenye shughuli nyingi za Kiuchumi za magari si sahihi kabisa kusimamisha shughuli za Kiuchumi barabara kuu kama hizo kupisha maandamano.
 

Tanzania ilishaharibiwa siku nyingi. Na sasa wameanza kuiuza kwa Waarabu.

Maandamano ni ya Amani maCCM mnaogopa nini? Kama hamtaki maandamano na mezani hamtaki, mnataka nini?
 
Waonyesheni hizo barua wananchi maana hao mliowapelekea watakana mara tatu kabla jogoo hqlijawika na watawapiga hivyo ushahidi mzuri ni kuwahusisha wananchi cha kuongeza familia za viongozi wote wawe mstari wa mbele!
 
Sasa wewe mfu uliitwa kuandamana?
Tuliza hicho kiyolea uchafu chako
 
Ila kupisha viongozi majizi wapite kwenye njia hizo ni sawa!
 
Ila kwakweli nchi yetu kupata mageuzi bado sana, wananchi wenyewe wanafuata upepo tu kwa hili la kubana matumizi chadema wapo sawa nawaunga mkono, ila hao wananchi wanaotetewa wanafurahia chadema apigwe dah
 
Vipi mkuuu umekunywa chai lkn?
 
Bumunda kaa kimya wanaume wainyooshe nchi!
 
Kwani umelazimishwa kuandamana?Acha uoga,haya ni maandamano ya amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…