Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Kuna siku mother alisafiri tukabaki na mshua ilikuwa hatari. Tukalilia wali, mshua akazama jikoni. Mhmm kitu kilivokuja mezani balaaa.

Haha hatari mkuu! Ila wali kwa sasa hausymbui kama una rice-cooker, kiukweli mimi wali wa kupikia kwenye jiko la gesi au mkaa siwezi ila kwenye rice-cooker ni rahisi sana
 
Nina imani mabachela tuko wengi sana humu.

Katika suala la kupika na kuosha vyombo huwa ni habari ingine. Vipi wewe mkuu ni msosi gani kuupika au kuuandaa huwa unakupa mawazo sana japo unaupenda. Na ukiula mahala unahisi umekosewa kupika sio kama ungeupika japo hujawahi kuutest geto.

Mimi bana WALI naupenda ila kuuandaa hadi utoke ni hatari sana. Halafu nikiwa nakula kitaa huwa mwepesi sana kuwalaumu wahudumu wali haujaiva au wamepika bokoboko au una mawe.

Wewe je msela wa geto nini kinasumbua jikoni?
Chapati na pilau. Nadhani hata nikipelekwa kozi ntafeli tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chapati na pilau. Nadhani hata nikipelekwa kozi ntafeli tu

Sent using Jamii Forums mobile app
86623f26fa91bdd88979d7c1da0168f4.jpg
 
Kuna vyakula vinatajwa humu kwakweli navitamani ila formula ya kuvipika ndo shida. Birian na makande? Makande mara ya mwisho kula ilikuwa shuleni hiyo advance.
 
Wali mbona easy siku hz kwa kutumia Ricekooker, hua naupika asubuhi nakula na chai jioni nautafutia mboga saafi
 
Kuosha vyombo ndio msala

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
Mods hiki kipengele cha chini cha kutambua mtoa mada katumia kifaa gani watu watakuja na mengi sana ila nimeipenda humuhumu tunajua uwezo wa mtu tukiangalia na simu aliyotumia
 
Back
Top Bottom