Mabenki yaanza kukusanya Tozo za Serikali kwenye miamala wanayofanya wateja

Mabenki yaanza kukusanya Tozo za Serikali kwenye miamala wanayofanya wateja

Yakusanye tu. Ikiwezekana Rudisheni hata Kodi ya Kichwa ile inaweza wasaidia watu kujielewa.
 
Watu wameanza kuletewa meseji kwenye simu kuhusu tozo wanazotozwa pindi wakifanya miamala ya kibenki.

Naona serikali imeamua sasa kutwaa fedha za wananchi kupitia tozo.

Sasa kinachofanyika, wananchi wanailipa serikali kodi za kawaida kama vile VAT n.k, halafu inakuja on top of that inakwangua pesa za watu kwa jina la tozo
Kwa kwenli tozo ni kama unyang'anyi wa wazi.

Mfano wa meseji ambao watu wanapata ni

Ndugu Mteja, tunakusanya tozo ya serikali kwenye akaunti yako kwa miamala ya tarehe 8 Sep 2021 mpaka 6 Oct 2021. Unaweza hakiki kupitia taarifa ya akaunti.

Pia, soma=▷Tozo zatinga kwenye mabenki, kuanza kukusanywa Septemba 8, 2021
Si ushukuru hata uwazi upo unapewa na taarifa,mbona makampuni ya simu na mabenki yalikuwa yanaiba pesa,mb nk bila taarifa?
 
Magu alikusanya pesa toka kwa matajiri, tulimsema sana. Mama amewaacha matajiri wanakula ubwabwa kwa mrija, masikini ishakuwa zamu yetu.

Futseke zao hovyo kabisa.
Matajiri gani Tanzania? Biashara zote za matajiri zilishasimamishwa na kufungwa. Wameshawakamua wote na damu zote. Sasa ni kila mtu akamuliwe. CCM Oyee!!!
 
Tuko na ma Hadi 2035 ,tozo hajengei nyumba yake bali anajengea mahitaji ya Watanzania.

Ukiangalia kila sekta Saizi imepewa pesa mara 2 au zaidi ya hapo awali kuyekeleza maendeleo.Lipa kodi kuwa mzalendo.
Hayo Maamuzi ni ya wananchi
 
Hayo Maamuzi ni ya wananchi
Unadhani hizo tozo zinaenda kutumia mbinguni? Zinatumika kwa wananchi.Mnalialia.umeme kukatika unadhani serikali itoe mavi kufanya ukarabati miundombinu umeme uje?

Maji ni tatizo kila sehemu serikali itoe kamasi ndio zitaleta maji? Lipa kodi upate huduma
 
Pana haja ya kufuata accounts statements na kulianzisha ikithibitika.

Miamala tuliachana nayo si kwa kupenda 😁😁.

Kama na huku tena hapo itakuwa ni kutafutana uchawi!
Muwe mnafuatilia kauli za serikali,walisema watakusanya pesa kwenye miamala yote ya kifedha kwenye simu na mabenki
 
Ni hatare, shakatwa tayar zote wamwkwangua
Na walivyo wapuuzi wankikata basi wakutumie poa ujumbe kuwa wamekata kiasi kadhaa ila wanataka uingie kuomba taarifa ili wakukate tena[emoji2297]
 
Hizi kodi za mshikamano mimi nataka mama aziongeze kila sehemu, hawa watu wakikamuliwa vizuri kwenye chaguzi akili zitaanza kuamka!
Kodi za kukatwa buku 2 hadi buku 25 tena unafanya muamala mara 1 au 2 kwa mwezi hazina maumivu kwa hiyo tuko na Mama hadi 2035
 
Hapo kati nimegonga miamala mingi balaa. Yani hapa nasiki kama utumbo unajinyongorota vile[emoji20][emoji20][emoji20]

NMB hawa, sijui benki nyinginezo kukoje huko
Yaani nimepitia miamala nilofanya kwa kipindi hicho walichosema walahi tumbo la kuhara limenishika. Naogopa hata kuiona statement[emoji2297]
 
Huo ni wizi on day light.
Mtalia Lia Kisha mtatulia kama awali lakini sasa matokeo yanaonekana,nyie watu wa mjini hamuwezi elewa haya.

Hata vifurushi Tzn bei ni chini serikali iongeze kodi huku tulingane na Nchi jirani.

Maana mtu anaweka buku Halotel anapata GB 1/week ya kuja kukejeri serikali huku mitandaoni,ingekuwa
 
Sah..wafanyakazi tutakufa taratibu sana kwa stress😒😒😒🤒🤒. Maana huwezi kusema unachukua mshahara cash dirishani🥺😭
Mama amepunguza kodi,mwakani anaongeza salary,ajira hazikauki utumishi portal unaweza omba.

Mama sio size yenu,Kuna majengo mengi ya vituo vya afya yamejengwa na yanaendelea kujengwa lazima pesa ipatikane Ili waajiriwe wakatie huduma.Lipa kodi kuwa mzalendo
 
Back
Top Bottom