Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Nimekupangia wapi nakukumbusha hii ni forum lazima ujibiwe pona yako ni usicomment kabisa
Hapa umenifurahisha sana aisee. Imebidi nicheke. Eti pona yangu ni kuto-comment.
Huu ni uzi wako na bila shaka ulipouweka ulitegemea mawazo tofauti tofauti. Sasa tusipo-comment uzi si utadoda?
Unapokomaa kuwa hiyo style yako ya ulezi na kufukuza mabinti home ndiyo sahihi, si ndo kupangiana kwenyewe huko? [emoji16]
Mimi simlelei mtoto kwa vitisho namlelea asiogope maisha pale anapokutana na changamoto atumie akili na mbinu azikibali awe wa kike au wakiume
Sio kila changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wake kuzikabili anakimbilia kwangu hapana, anakuja kwangu mpaka nijiridhishe amerun-out of option simlelei mtoto kimayai au kwa vitisho namlelea aweze kutumia akili yake effectively sababu matatizo tumeumbiwa wanadamu
Kila mzazi bila shaka anamtakia mema na mafanikio mtoto wake. Na kila mzazi anapambana sana katika malezi yake ili kuutimiza huu wajibu mtakatifu aliojivika. Je, kuna njia moja ya kufikia jukumu hilo? Hapo ndipo tunapotofautiana. Kila mzazi anapambana kivyake...kwa mafanikio tofauti tofauti....
Na hoja yako mama (kama kichwa cha uzi wako kinavyosema) ni kwamba binti aliyefikisha umri wa kuolewa inabidi afukuzwe nyumbani. Na hapa ndipo tunapingana sana - pengine kuanzia katika kiwango cha kifalsafa tu.
Kwangu mimi thamani na upendo kwa binti yangu havina gharama, bei, matakwa wala mikatale. Ni ile wanaitaga priceless!
Na siamini kwamba eti ni lazima aolewe ndiyo malezi yangu mema kwake yajidhihirishe. Kwamba asipoolewa eti ndiyo nimefeli. Kwamba asipoolewa thamani yake kwangu inashuka mpaka nifikie hata kumfukuza. Nimfukuze aende wapi? Akatafute hao wanaume wa kumuoa kwa nguvu? Hao waoaji wenyewe wako wapi?
Wa kwangu huyu nimeshamwambia. Priority yake maishani iwe ni kuishi maisha yenye furaha. Afanye kitu anachokipenda. Kinachompa ridhiko. Kuanzia kazi na mengineyo. Bila presha kabisa. Huku akijua kuwa babake ni supporter wake nambari wani. Akiamua kuolewa ni sawa. Asipoamua kuolewa pia ni sawa. Cha muhimu tu awe na uwezo wa kuendesha maisha yake bila kutegemea watu lakini hapa kwa baba yake ni kwake pia na anaweza kurudi wakati wo wote akitaka. Na chumba chake kipo vile vile kama alivyokiacha....
Hii nimeipenda maana nadhani imemwondolea mzigo mabegani mwake. Usiwaone hivi. Mabinti hawa wana presha kubwa sana vichwani mwao. Jamii inawategemea waolewe kabla hawajavuka 30 wakati hata statistically tu hili haliwezekani maana wao ni wengi kuliko wanaume. Ukijumlisha na hizi changamoto zingine zinazokikabili hiki kizazi chao (wavulana kutotaka kuoa ili kukwepa majukumu, ushoga, wanaume legelege, sijui ukosefu wa nguvu za kiume...), ni wazi kwamba si mabinti wote wataolewa hata kama wakifikia umri wa kuolewa na wanatamani kuolewa. Na kuwanyanyapaa mpaka kuwafukuza majumbani sidhani kama ni suluhisho.
Hakuna kitu kinachompa mwanamke thamani kama kuwa na uhuru wake wa kiuchumi. Ule uwezo wa kuendesha maisha yake bila kumtegemea mwanaume wala mzazi wake. Nadhani juhudi zetu kama wazazi tungezielekeza huko badala ya kuwaongezea presha kwamba ni lazima waolewe wakifikia umri fulani; na wasipoolewa basi tunafikia hata kuwafukuza majumbani mwetu.
Huyu wangu amepambana mwenyewe amepata ma-scholarships yake huko anafanya Pre-Med. Ndoto yake ni kuwa pediatric cardiologist maana anapenda watoto sana. Na mpaka ninapoandika hapa anafanya kazi nzuri tu inayompatia mahitaji yake yote. Anajiamini. Ana mwanga katika maisha yake. Akiamua kuolewa sasa au baadaye ni sawa. Akiamua kutoolewa sasa na hata baadaye napo ni sawa. Akiamua kukaa nyumbani sasa na hata hapo baadaye napo ni sawa.
Bila presha yo yote...
Upendo wa baba [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji3590][emoji3590][emoji3590]