Tetesi: Machache aliyonieleza mfanyakazi wa TPA yana ukweli?

1. Budget zote za uendeshaji, manunuzi na nyinginezo katika taasisi za serikali hipangwa na kupitishwa katika bunge la bajeti. Amekadiriaje kuwa kuanzia wakati huo pesa haitakuwepo na ukizingatia shirika halihitaji ruzuku kujiendesha kwamba bandari inafungwa?

2. Ni ngumu sana kwa DPE kuwa ingeanza shughuli mwaka huu hata kama kila kitu kingekua smooth. Handling and passing over activities za bandari sio kama kuuziana dalaala kuwa ukiuziana leo basi kesho utaanzakuamsha asbuhi kubeba abiria. Atupe timeframe iliyosema DPW angeanza kazi October.

3. Hili fuatilia mwenyewe utaujua ukweli. Kama wafanyakazi wa bandari ni mafisadi na wezi ama hao unaoita viongozi ndio mafisadi wa bandari utapata jibu.

4. Mkuu kuwa na bandari pekee sio kigezo cha mtu kupitishia mizigo katika bandari yako na ndio maana kuna masuala mengi ya kibiashara yanayoamua watu wapitie kwako. Hii ni debate tena kubwa tu na sio kwa tuhuma ndogo ama slight accusations kama hizi.

Mkuu kila mtu amekua akiongea lake kuhusu bandari na kama ilivyo kawaida ya majungu kila anayelipata analifanya ku'amplify hivyo kupoteza uhalisia wa mpika majungu wa mwanzo na wa mwisho.

Katika hili suala watu tunapaswa kusoma sanaaaa na kuchimba sana maandiko ya wataalamu katika PORT BUSINESS ili tuuelewe ukweli lakini kama kawaida yetu sisi watanzania ni wavivu kusoma na tunapenda kusimuliwa zaidi kuliko kusoma na siwezi kushangaa kukuta mtu anapondea ile IGA lakini ukimuuliza kama umesoma mkataba husika kwa niliokutana nao ni 80% hawakuusoma waliishia kupata clips na kusimuliwa.

Tunapaswa kutumia akili yetu kwanza kabla hatujatoka nje kutafuta msaada lakini tutafute uhalisia kwa neutral party tunaweza kuokota lolote
 
Itakua kweli. Hao wenye mirija bandarini ndio wameona bora waiuze kabisa. Na ndio wasiyotaka usimamizi imara ili waweze kuendeleza unyonyaji wao. Rais na serikali yake wawajibike sio kutaka kuwapa dubai kutwaa bandari za nchi yetu. Vinginevyo 2025 tuibwage ccm chini.
 
mimi natamani wanipe niendeshe banandari.

nahisi point ya 3 ina ka ukweli fulani. Tanzania tuna matajiri wengi why wasipewe tenda hii kwa mkataba mzuri ?
Watawala hawana imani na ninyi raia
 
Kidoogo naanza kupata nuru
 
Bandari ni mto w pesa usiokauka, serikali iwape..
 
Kakoko Ana mafaili mengi Sana Siku akiyamwaga panachafuka.
 
Mkuu tuweke records sawa. Wakati Samia anaingia madarakani hadi hivi sasa hakuna major changes alizofanya zaidi ya kutowaongeza muda TICTS na ameamua kutoa room ya uwekezaji kwa mwingine na sehemu nyingine ya bandari ili kuboresha utendaji zaidi na faida zaidi na wanadai kuwa hali ya kipato kwa serikali tokea pale bandarini imeongezeka(naweza kurekebishwa).

Kwani kuna mfumo gani mwingine alioubadili nijifanyie updates hapa
 
Naunga mkono

Kana kwamba hao wezi sijui sio waaminifu wameteuliwa na serikali ya chama kingine.
 
Kungekuwa na mifumo imara rais asingehangaika na maziara ya kustukiza ya mchongo!
 
Kwann tusinunue management ya kuendesha shughuli zetu za uchumi toka nje na kuipa full mamlaka.
Hata Kama watalipwa mishahara mikubwa kuliko kubinafsisha
 
Bila kujali ulilotaka kuweka hapa, rekebisha hapo namba tatu, kama viongozi ndio wanakula hapo, hiyo DP World watakulaje wakiwaleta? Rekebisha hapo tafadhali.
 
Bila kujali ulilotaka kuweka hapa, rekebisha hapo namba tatu, kama viongozi ndio wanakula hapo, hiyo DP World watakulaje wakiwaleta? Rekebisha hapo tafadhali.
Mkuu
DPW ni upande mmoja na hao wahuni ni kamilisho la upande huo.

Elewa concept
 
Hayati John Joseph Pombe Magufuri akiwa kama baba wa taifa 🇹🇿 wa pili baada ya wa kwanza Julius nyerere...,.....

Hao wawili wasinge kabidhi sovereign state yetu kwa kijikampuni kitakataka Cha DP WORLD in MWABUKUSI voice.,........
 
Hayati John Joseph Pombe Magufuri akiwa kama baba wa taifa 🇹🇿 wa pili baada ya wa kwanza Julius nyerere...,.....

Hao wawili wasinge kabidhi sovereign state yetu kwa kijikampuni kitakataka Cha DP WORLD in MWABUKUSI voice.,........
Tujikumbushe sababu na dhima ya kutoipa CCM kura hapo 2025
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…