Machache yanayonifanya niamini uwepo wa Mungu: Hatari ya kuamini hakuna Mungu



Hiyo hadithi ya Pazi inakushika wewe mwenyewe, mimi katika suala la kiti cha enzi cha Mungu (throne) sikuzungumzia juu ya usahihi wa habari ya hicho kiti bali nimezungumzia juu ya falsafa ya kiti chenyewe na nikasema hicho kiti maana yake ni utukufu, power nk za Mungu na sio kiti halisia kama viti vya kukalia wanadamu, huo mfano wako wa jogoo na Pazi unaunga mkono hicho ninachokisema kwamba hadithi hiyo ni metaphor/parable na inahitaji tafsiri ili upate maana yake kama jinsi utahitaji tafsiri kupata maana ya kiti cha enzi cha Mungu, kiti cha enzi kwa kizungu ni (throne) na mfalme au mtawala akiondolewa katika ufalme au utawala wake neno linalotumika ni (dethroned) hivyo utaona kiti cha enzi (throne) HASA kinawakilisha utawala, utukufu nk, kwani kiuhalisia hakuna kiti cha kawaida kinachoweza kumbeba Mungu jinsi isivyokuwa kawaida Jogoo kumbeba mtu, nashukuru kuleta hiyo hadithi ya Pazi.🤣🤣.

Unataka maelezo yangu uyapate kutoka kwenye Qur'an!!!, je ukiyapata ndipo utaamini uwepo wa Mungu??!!. ----Katika Qur'an Wapinzani wa mtume (saw) walimwambia mtume kwamba hawatamuamini hadi apande mbinguni na awaletee kitabu kutoka huko ili wakisome na sio hii Qur'an, Mungu akamwambia awaambie; "Mtukufu ni mola wangu mimi siye ila ni mtu na mtume"., hivyo madai yako ya kutaka maelezo yote yatoke ndani ya Qur'an ni madai yale yale ya Wapinzani na hata kama madai hayo yangetekelezwa bado ungetafuta madai mengine mapya. Kifupi ni kwamba; "Laa yumasuhu illa mutaharuun" yaani huwezi kushika/kupata maana za ndani za Qur'an bila kujitakasa, kutakasika au kuomba utakaswe.

Kumbuka akili zetu ndio nyenzo alizotupatia Mungu na usijisikie interior kujifunza kitu kipya chenye faida kutoka kwa mtu mnayepingana kimawazo.
 
Universe ni kubwa na still inazidi kutanuka na inatanuka kwa spidi ya mwanga... aya mungu yukowapi kwenye hii universe yote? Kuna viumbe kwenye sayari nyingine yyte mbali na dunia? Kama wapo, ni kwenye sayari gani? Kama hawapo ni kwanini, kwanini huyo mungu kaumba universe yote hii na kaweka kife duniani tu?Nataka kuona dini ikijibu maswali haya..
 
Hapana bro, sijamaanisha kwamba sayansi ina project zinazolenga kumtafuta mungu. Bali kuna lile swali la "what's the origin of the universe?" Na hapa theory ya creation ILIKUA considered... ila kwa bahati mbaya tunazidi kupata sababu tu zaidi za kua hamna creator wa universe. Ndio maana sasaivi utasikia watu wanakwambia maandiko usiyachukulie literally [emoji23]
 
Ona sasa... eti space exploration ni waste of money! Hapana, hii ndo inasaidia kujua mahala tulipo katika universe kuelewa muundo wa universe, na hata kupata idea universe iliundwaje, since... well ...we can't trust your gods.

Na pia siunaelewa kua jua lita ingia stage ya red giant in a few billion yrs to come? Hizi exploration zinasaidia kutafuta mbadala wa kuamisha colonization kwenye sayari ingine. Mdg mdg miaka maelfu ijayo huenda sayari habitable ikapatikana. Maybe or maybe not...
 
Subiri kidogo

"The heavens, We have built them with power. And verily, We are expanding it" Qur'an (51:47) {579-632}

Then Hubble in 1920s discovered that the universe is expanding
Kwahiyo heavens=universe? Anhaa sawa...
 
Sasa huoni kwamba kuna wakati vitu kama hasira, malipizi ya visasi, chuki vinaweza kumfanya mwanadamu afikirie kuua ila hapohapo unakuta kinachomfanya asifanye hivyo ikawa woga wa kuingia matatizoni, Ila anyway kama ungekuta woga hautakiwi basi kwenye maandiko pasingekuwa na maneno kama "Ole wao" Haya umesema kuna kuheshimu na sio kuogopa Rais ni cheo cha kuheshimika hivyo basi kama tunapaswa kukiheshimu na heshima inafanya tushindwe kufanya baya juu yake basi ni kwanini anawekewa ulinzi.... Sasa ukitaka ujue tofauti ya heshima na woga kajaribu kumsogelea kiholela.... Huwezi kusema unaheshimu kitu bila kuogopa kuvunja heshima.
 
Uzi wako umeniongezea kasi ya kumuamini Mungu katika changamoto ninazopitia kwamba kama aliweza kuumba hayo yote basi anaweza kutatua mapito yangu.
 
Kuna mambo ambayo hujayaelewa sijui ni kwa bahati mbaya au kusudi.

Kwanza mfano wa Pazi na jogoo niliuweka kuonesha uwezekano wa kujadili stori fulani kama ilivyoandikwa pasipo kukubaliana na uhalisia wake.

Ukiniambia Pazi alibebwa na kuku jike nitakupinga kwasababu umepotosha stori ya mwandishi. Kukupinga huko hakuna maana kwamba nakubaliana na uhalisia wa stori hiyo.

Nataka nijue hiyo falsafa ya kiti umeitoa ndani ya kitabu au ni interpretation yako tu?

Kuuliza kama ukinipa maelezo kutoka ndani ya kitabu yanayoelezea maana ya kiti cha enzi kwa jinsi ulivyodai wewe inakuwa hauna tofauti na mtu anayesema Pazi alibebwa na kuku jike nikamuomba anioneshe hayo maneno ndani ya kitabu afu ye akasema kwani nikikuonesha ndio utaamini kuwa Pazi aliwahi kubebwa kichwa chini miguu na kuku?
 
Ngoja tujadili kwa namna ambayo we unataka

Kama woga ndio unaosababisha watu washindwe kufanya mabaya, mbona bado kuna mabaya?

impact ya huo uwoga iko wapi?

Unazungumzia mwanadamu kufikiria kuua halafu akaja kughairi kwa kuogopa Mungu atamuadhibu wakati vitabu vya dini vimesimulia namna mitume wenu walivyokuwa wakifanya mauaji bila woga

Na sio tu kwamba mtu ndio anafanya mabaya kwa kuhemkwa kushindwa kuzuia hisia zake, hata Mungu katajwa kufanya mauaji kwa wasio na hatia na ameshindwa kuzuia hisia zake.

Nakupa mfano wa ile hadithi ya Pharao na Mussa ambapo ili kumfanya Pharao awaruhusu waisrael waondoke ilibidi apigwe mapigo kumi

Hayo mapigo kumi hayakumlenga yeye, yalilenga watu wengine wasio kuwa na hatia.

Mungu alitoa agizo la kila nyumba kupaka damu ya kondoo juu ya milango yao na usiku roho mtakatifu alipita ku scan kila nyumba.

Nyumba ambayo haikupakwa damu juu ya milango yao iliadhibiwa kwa kuuwawa mtoto wa kwanza wa kiume.

Huyo mtoto wa kwanza wa kiume hajahusika kwa namna yeyote na dhambi ya pharao lakini pharao kaachwa, akaenda kuadhibiwa mwingine.

Mungu anayekuambia ole wako ufanye jambo fulani halafu yeye ambaye tunategemea kumuona kama mfano unamuona analifanya jambo hilo unafikiri inaleta picha gani?
 


Mimi nimeongelea kiti cha enzi cha Mungu na wala sijaongelea kiti cha enzi cha Scars au jini nk, ningalikuwa nimeongelea kiti kingine kinyume na hicho basi ulikuwa unayo haki ya kutoa mfano wa hadithi ya Jogoo na kuku tembe na Pazi kwa maana hiyo huo mfano wako ni irrelevant katika case hii.

Kwa upande mwingine Ulipotoa huo mfano wa Pazi na jogoo ndipo na mimi nika take advantage wa kuhusisha mfano huo na kiti cha enzi cha Mungu kwamba habari zote hizo mbili zimekaa kimafumbo kwani haiingii akilini Kwamba ipo siku jogoo atamning'iniza mtu kichwa chini miguu juu halikadhali haitatokea Mungu aketi kwenye kiti au sofa akinywa soda akiangalia TV kama binadamu afanyavyo, hivyo ukisoma maandiko ni lazima uyapime kwani maandiko mengine ni tamathali za semi (figure of speech).

Umeshikilia tu nikuonyeshe ni wapi nimepata hiyo interpretation, nataka ujue kwamba aya za Qur'an (kwa mujibu wa Qur'an) zimegawanyika katika makundi mawili; ayat Muhakamat na ayat Mutashabihat, hizo za kwanza zinakupa maana ya moja kwa moja na hizo za pili zinakupa maana ya iliyojificha, aya ya Kiti cha enzi ni kundi la pili (mutashabihat) ambayo inahitaji ufafanuzi ili Kuelewa maana zake za ndani, kama nilivyokueleza Qur'an inasema; "laa yumasuhu illa almutaharuun", yaani mtu hashiki/hataelewa maana za ndani za Qur'an kama huyupo tohara kiroho, sasa wewe unapinga kuwepo kwa Mungu kwa Kibri je huyo Mungu anaweza atakase roho yako ili ujue undani wa maneno yake wakati umeweka kibri kama uzio !??--- ondoa hicho kibri na jaribu kunyenyekea na hapo Mungu atajitokeza kwako Miraculously.
 
Kuna point unai miss hapo, mfano wa Pazi nimeutoa kuonesha jinsi mtu anavyo weza kuingia mjadla kujadili stori yeyote bila kukubaliana na uhalisia wa stori hiyo.

Hapo nilikuwa nai refute hoja yako iliyokuwa unadai sipaswi kukosoa madai yako uliyoyatoa kinyume na ilivyoandikwa kwasbabu tu siamini Mungu yupo

Mkuu hiyo ya kusema tohara ya kiroho wote tunakubaliana ni propaganda za kidini zinazotumika kuzuia ukosolewaji na watu waliokinyume na dini husika

Hata wewe huwezi kuupinga ukristo maana nao wameweka defense ya namna hiyo kuwa kabla ya yote unatakiwa umpokee roho mtakatifu

Roho mtakatifu huanza kwa kumkiri Yesu kuwa bwana na mokozi wa maisha yako.

Ikifuatiwa na kubatizwa kwa ajili ya kuruhusu huyo Roho mtakatifu akuingie

Wanakuambia ukiwa na Roho mtakatifu huwezi ukaona dosari kwenye biblia, kama umeona dosari tafsiri yake ni kwamba hauna roho mtakatifu

Sasa mpaka hapo ukisema ufuate kanuni hiyo utaweza?
 


Mkuu, mimi points zako zote nizipata labda mimi naongea kwa falsafa ya juu sana kiadi kwamba unashindwa kunipata.

Ni hivi; Wewe unadai kwamba kiti cha enzi cha Mungu ni kiti halisia au unataka kuamini kwa mujibu wa hiyo habari kwamba kiti hicho ni halisia na hapo unapingana na mimi ninaposema kwamba kiti hicho ni metaphor, sasa unawezaje kujadili kitu cha mtu ambaye hayupo???---- eti nianze kujadili simu ya mtu anayeitwa Scars wakati mtu mwenyewe hajulikani wala siamini Kwamba aliwahi kuishi!!!, hekima inasema hivi; kwanza tuthibitishe huyo Scars yupo au aliwahi kuishi na halafu ndipo tujadili habari ya simu yake, mbaya zaidi unashadidia kwamba kiti hicho ni HALISI kana kwamba umeingia ndani ya fikra za mleta hadithi (katika Qur'an ni Mungu mwenyewe) au kana kwamba umewahi kukiona hicho kiti!!, hutaki kusikia kwamba sio aya zote za Qur'an zinayo direct interpretation na mojawapo ni hiyo ya kiti cha enzi.

Ulipotoa mfano wa Jogoo na Pazi kwa kutoa hoja kwamba hukubaliani kwamba Jogoo anaweza kumning'iniza mtu kidhahiri lakini unayo haki ya kujadili kitu hicho japokuwa hukiamini na mimi pia naungana na wewe siamini kama jambo hilo linaweza kutendeka kidhahiri na ndio maana mimi nimetumia fursa hiyo kukuambia kuwa suala hilo na suala la kiti cha enzi cha Mungu ni metaphors yatupasa tujifunze kama tamathali za semi, kwani katika hiyo hadithi ya pazi na jogoo hakukuwa na fundisho?? au ilikuwa ni hadithi tu bila lessons and morals??-- na ndivyo hivyohivyo kwenye kiti cha enzi tunapata lessons and morals.
 
Prolly it is really beyond my grasp, can't deny that

Ni kweli nadai kiti cha enzi ni halisia kama ilivyoelezwa kwenye kitabu na sio code name.

Lakini hili nalijadili katika muktadha wa maandiko namna yalivyo andikwa na sio swala la mimi kukubaliana na hadithi hiyo.

Hata wewe unaweza kujadili habari za biblia ambazo hukubaliani nazo kwa kupoint vifungu vya biblia lakini haimaanishi kwamba unakubaliana nayo.

Kwasababu sio mara moja Mungu ameelezewa kwenge hivi vitabu akiwa na sifa zinazomtambulisha kuwa yupo physically

Kitabu chenu kimeandika Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake, ukiangalia hicho hicho kitaja kimetaja muonekano wa Mungu, Mungu huyu ana macho, anasikia, ana mdomo, hadi jinsia yake inafahamika, kuna maelezo mengi yanayopambanua muonekano wake yanayothibitisha kuwa ana mwili.

Na ndio maana napotaka utetee hoja yako uweke maneno yaliyoandikwa kwenye kitabu hicho yanayokanusha na sio kuweka mawazo yako
 


Kama Qur'an isingeandika baadhi ya aya zake katika muundo wa tamathali hiyo Qur'an nadhani ingekuwa na uzito wa zaidi ya tani kumi.

Thamathali makes a person use his/her mental power thus exercises his brain apart from gaining desired lessons.
 
Mungu ni Roho na shetani pia ni roho lakini uonekana kupitia matendo ya wanadamu. Mwanadamu anaweza akawa shetani au MUNGU. Neno mtu means Mungu you ndani ya mtu, ubinanadamu means uwepo wa Mungu. Shetani ni mtu mwenye matendo yasiyo ya kiutu
 
Kama Qur'an isingeandika baadhi ya aya zake katika muundo wa tamathali hiyo Qur'an nadhani ingekuwa na uzito wa zaidi ya tani kumi.

Thamathali makes a person use his/her mental power thus exercises his brain apart from gaining desired lessons.
Kila dini ina kauli mbiu kama hiyo
 
ebu tufupishe suala, Kwahiyo wewe unamuogopa Mungu au Umuogopi? Au huamini pia kama kuna Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…