Machimbo mazuri ya kupata bidhaa mbalimbali Kariakoo kwa bei nafuu
Unatafuta bidhaa bei nafuu na jumla Kariakoo? Hapa nakupa machimbo bure ufanye biashara,

Save hiii post kwanza itakusaidia baadae.

Maduka ya jumla kwa vitambaa vya Masofa, yanapitakana mtaa wa kipata, anza na kipata na msimbazi mpaka kipata na swahili yapo ya kutosha.
_
Vifaa vya umeme nenda Mtaa wa Narung'ombe.
_
Spear za pikipiki Nenda mtaa wa swahili na k/koo hapo kuna maduka mengi.
_
Mtaa wa congo na narung'ombe underground ya Tanzanite kule chini kuna mtaa mzima unaingia unatembea chini kwa chini kuna t-shirts za bei nafuu.
_
Vifaa vya plastiki Nenda Duka la cello kariakoo .
_
Make up _ kituo cha mwendokasi ukiachana na huu upande ilipo msimbazi polisi ule mwingine unaingia ndanindani.
_
Kwa nguo za ndani (chupi) ukimaliza kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, kwenye upande wa vitu vya make up kuna mtaa mmoja unaingia yapo maduka mengi dozen za cotton Ni Bei nafuu.
_
Rasta bei ya jumla ziko upande wa pili wa kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, mtaa yanapopaki magari ya makumbusho gerezani yanayopitia Sinza.
_
vitambaa vya vijora ni Msimbazi Kwa nyuma.

Chimbo la dawa muhimu za binadamu kwa kariakooo linapatikana mtaa wa Kipata na nyamwezi street.
_
Bidhaa za simu, cover, charger, housing Kwa bei Chee ziko Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani
_
Vifaa vya ujenzi ni Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata.

Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )

Shati ni mtaa wa Agrey/congo au mchikichi/Congo

Mashine mbalimbali kama za miwa, kusaga nk nenda Mtaa wa SIDO

Narudia Vitenge ni pale mnazi mmoja ile njia ya kuingia posta. Wale wahindi watakuuzia vitenge vizuri bei nafuu. (ukipata connection ya Uganda utatisha)

Maduka ya wachina wanaouza viatu vya kike ni mtaa wa congo.

Vipi kuhusu cosmetics mkuu na manukato
 
Vipi kuhusu cosmetics mkuu na manukato

Ukifika Big bon vuka upande wa pili unaotazamana na Big Bon wa barabara kubwa ya mwendokasi na upite kichochoro chochote kuingia huo upande huo kuelekea Magharibi utaanza kuyaona maduka na utatokea upande barabara wa Daladala za kwenda SINZA Makumbusho,( zamani mbezi). Utaona Maduka yapo pande zote za barabara
 
Safi sana.

Jamaa wa MNAZI MMOJA wapo siriasi na kazi ni kitambo sana biashara yao ndio ile ile.
 
Pia kuna Chimbo la Ubuyu wa vimto na Ladha nyingine. N pale kwa Magomeni kanisani njia ya kwenda Tandale.
 
Back
Top Bottom