Machimbo mazuri ya kupata bidhaa mbalimbali Kariakoo kwa bei nafuu
Anaehitaji mtaa wanaouza sabufa Aina zote za jumla mafenii nyuma ya jengo la msimbazi.
 
Na machimbo ya( PPE's),
Yaani vitu hivi yako wapi kwa hapo kariakoo mkuu....??

gloves,
helmet,
Overall
Ear plug
Dust mask
Safety glass,
Safety boots
Cutting disc
Drill machine
Welding shield,
Angle grinders
Air compressors
safety harness belt,


Vifaa vya usalama na kazi mahala pa kazi kama Workshops na Mining areas vinauzwa wapi kwa hapo kariakoo mkuu???
Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata
 
Wap naweza pata viatu aina hii
IMG-20210525-WA0003.jpg
 
Hayo maduka yapo karibia na maeneo gani
Hayo maduka yapo karibia na maeneo gani
Mambo vipi mkuu, kuna duka la wahindi nalifahamu lipo posta Dar, nilishawahi kununua hapo T-shirts za cotton ambazo ni nzito. Wanauza Tshirt kwa jumla. Tshirt za round collar, sh 6000 kuanzia 10, ukichukua 100 bei 5500. Pia wanauza za form 6 ila bei yake sikumbuki. Kuna bidhaa zingine wanauza. Ninaweza kukupeleka. Kwa maelekezo zaidi nitumie msg PM.
 
Ahsante Sana mkuu ila hizo tshert ukiingia ndani kule unakuta wengine wanaziuza Elfu 10 Kwa jumla sasa sijajua kama Zina tofauti na hizo wanazouza Elfu 7000 machinga na pia naomba kuelekezwa machinga complex IPo mtaa Gani na pia penye maduka ya vipodozi mfano dettol ya kuogea ya mtoto unakuta inauzwa 18000 Kwa dazen lakini ukija barabani huku unakuta wamepanga chini wanauza jero jero nazo sijajua pia kama ni feli au la ila zinafanana vile vile.
Kaka zile feki ama zimekaa Sana madukani (ubora umeisha ama umepungua)..japo unaweza bahatika ukapata kitu quality!!Kuna wahuni wengi Sana Sasa hivi wanafyetua bidhaa majumbani mwao na kufanya packaging ukiletewa sokoni huchomoki
 
Unatafuta bidhaa bei nafuu na jumla Kariakoo? Hapa nakupa machimbo bure ufanye biashara,

Save hiii post kwanza itakusaidia baadae.

Kwa nguo za ndani (chupi) ukimaliza kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, kwenye upande wa vitu vya make up kuna mtaa mmoja unaingia yapo maduka mengi dozen za cotton Ni Bei nafuu.

Make up _ kituo cha mwendokasi ukiachana na huu upande ilipo msimbazi polisi ule mwingine unaingia ndanindani.

Maduka ya jumla kwa vitambaa vya Masofa, yanapitakana mtaa wa kipata, anza na kipata na msimbazi mpaka kipata na swahili yapo ya kutosha.

Vifaa vya umeme nenda Mtaa wa Narung'ombe.

Spear za pikipiki Nenda mtaa wa swahili na k/koo hapo kuna maduka mengi.

Mtaa wa congo na narung'ombe underground ya Tanzanite kule chini kuna mtaa mzima unaingia unatembea chini kwa chini kuna t-shirts za bei nafuu.

Vifaa vya plastiki Nenda Duka la cello kariakoo .

Rasta bei ya jumla ziko upande wa pili wa kituo cha mwendokasi kinachoangaliana na msimbazi police, mtaa yanapopaki magari ya makumbusho gerezani yanayopitia Sinza.

vitambaa vya vijora ni Msimbazi Kwa nyuma.

Chimbo la dawa muhimu za binadamu kwa kariakooo linapatikana mtaa wa Kipata na nyamwezi street.

Bidhaa za simu, cover, charger, housing Kwa bei Chee ziko Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani

Vifaa vya ujenzi ni Mtaa wa livingstone kuna Duka Linaitwa Bahdela bei poa vyote utapata.

Vifaa vya stationaries ni mtaa wa Kipata ( maduka ya wasomali ndo bei nzuri )

Shati ni mtaa wa Agrey/congo au mchikichi/Congo

Mashine mbalimbali kama za miwa, kusaga nk nenda Mtaa wa SIDO

Narudia Vitenge ni pale mnazi mmoja ile njia ya kuingia posta. Wale wahindi watakuuzia vitenge vizuri bei nafuu. (ukipata connection ya Uganda utatisha)

Maduka ya wachina wanaouza viatu vya kike ni mtaa wa congo.
 
Back
Top Bottom