Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Upande wa kushoto ukiwa unashuka chini kuelelekea fire kabla hujafika kituo Cha Mwendokasi Cha Msimbazi B unazama Kwa ndani Kuna bidhaa kibaoo Kwa bei Chee.Chimbo lipi kariakoo la kupata bidhaa za jumla za simu kama cover, screen protector, headphone, charger, na simu za bei ya jumla
Pia ukihitaji majeneza ya bei chee na ya kisasa kabisa nicheki fasta utaletewa ulipo (kwa wakazi wa Dodoma, Morogoro na Dar)Wapendwa week end inaendaje?
Wanasema kizuri kula na mwenzako....na nomeona niwashirikishe fursa hii adimu hasa kwa wale wanaofika kariakoo na kujikuta wanauziwa bei ghali kuliko hata huku mtaani...
[emoji117][emoji117][emoji117]
SOMA HAPO UKIPENDA SAWA USIPOPENDA PITA KIMYA
Ngoja nikupe machimbo eh best kizuri kula na mwenzio...Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule mnazi mmoja wengi wanaouza k.koo wanaenda kufata huko,
Viatu navyo vinapatikana huu mtaa wa Narung'ombe na congo pale nenda straight kwenye maduka ya wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini nop unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile visandles wanauza 2500/pc.
Cheni zama mchikichi katikati kuna mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki.
Magauni nayo ingia ndanindani kule congo na aggrey wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc.
Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro.
Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau?
Mapazia ya kukata jora Kama unaenda Posta upande wa chuo cha DIT na CBE, Ukishavuka ule ukuta kuna duka la mfanyabiashara ana asili ya india anauza bei nzuri na mara nyingi Jumamos anakua na bei ya SALE kwahyo unaweza kupata majora ya mapazia kwa bei chee na kila design.
NA UKITAKA DAGAA ZA KUKAANGA FRESH KABISA KUTOKA MWANZA YANI KUTOKA ZIWANI STRAIGHT KWA MLAJI UTAZIPATA KWA HUYU HAPA 0654688288
NATUMAIN MTAKUJA NA MACHIMBO MENGINE SEMENI HAPA. copy and paste
Ahsante Sana mkuu ila hizo tshert ukiingia ndani kule unakuta wengine wanaziuza Elfu 10 Kwa jumla sasa sijajua kama Zina tofauti na hizo wanazouza Elfu 7000 machinga na pia naomba kuelekezwa machinga complex IPo mtaa Gani na pia penye maduka ya vipodozi mfano dettol ya kuogea ya mtoto unakuta inauzwa 18000 Kwa dazen lakini ukija barabani huku unakuta wamepanga chini wanauza jero jero nazo sijajua pia kama ni feli au la ila zinafanana vile vile.
Hebu imagine mtu aje hapo eneo lako uliloajiriwa (kwa nyie waajiriwa)halafu amwambie bosi wako kwamba anajua chimbo la wafanyakazi wa bei rahisi kuliko alionao..utajisikiaje!Mi nayajua Machimbo ya kila bidhaa kariakoo..lkn siezi toa Code humu maana huenda nina wateja wangu humuhumu ninaowauzia..huyu mwamba aliyetoa mchongo humu inawezekana hana biashara.maana huwezi kumwaga mchongo wa kazi kiboya namna hii.
MkuuMi nayajua Machimbo ya kila bidhaa kariakoo..lkn siezi toa Code humu maana huenda nina wateja wangu humuhumu ninaowauzia..huyu mwamba aliyetoa mchongo humu inawezekana hana biashara.maana huwezi kumwaga mchongo wa kazi kiboya namna hii.
Roho ya kimasikini hii.Tz kuna raia milioni 60+ alafu mtu unakuwa na hofu ya kupoteza wateja kisa kuogopa kuchangia huu uzi wa jf??[emoji848][emoji848] Wakati hata waliousoma hawafiki 10kHebu imagine mtu aje hapo eneo lako uliloajiriwa (kwa nyie waajiriwa)halafu amwambie bosi wako kwamba anajua chimbo la wafanyakazi wa bei rahisi kuliko alionao..utajisikiaje!
Tajiri hakupi mchongo wa pesa hata siku moja..karagabaho.Roho ya kimasikini hii.Tz kuna raia milioni 60+ alafu mtu unakuwa na hofu ya kupoteza wateja kisa kuogopa kuchangia huu uzi wa jf??[emoji848][emoji848] Wakati hata waliousoma hawafiki 10k