Machimbo mazuri ya kupata bidhaa mbalimbali Kariakoo kwa bei nafuu
Nipe chimbo la mashati original au t shrts ,mfano wa heat gear fabrics au nike dri fit.
Sitaki midosho ambayo ukifua mara moja inapauka
 
Asante kwa uzi mzuri, na kwa rim papers bei rahisi napata wapi kkoo hapo. Tunaruhusiwa ku share kwa anaejua please.
Ngoja wa steshenary akuje ila asipokuja hadi kesho ntakupa mrejesho coz nina mtu anadili na ishu hizo
 
Mimi naomba kujua tu yafuatayo je ni chimbo Gani wanauza t-shirt za Form 6 zile ambazo machinga wanauza Elfu 7? Pia naomba kujua kariakoo shimoni ni wapi na ni chimbo Gani wanauza zile sendles za kimasai Kwa jumla pamoja na sabuni za kuogea.
 
Tisheti Form 6 nenda mtaa wa Agrey na Congo utazipata. Kariakoo shimoni pamefungwa kwa sasa(Ndo lilipokuwa soko lililoungua) sandoz za kimasai kwa bei nzuri Nenda Machinga Complex kule ndo kuna viwanda vidgo vidogo zaid ya 200 wanakuuzia hata pea 1 na bei zao ni njema. Sabuni mtaa wa Msimbazi A&B karibu na vituo vya mwendo kasi kote kuna maduka ya vipodozi bila shaka utazipata huko
 
Ahsante Sana mkuu ila hizo tshert ukiingia ndani kule unakuta wengine wanaziuza Elfu 10 Kwa jumla sasa sijajua kama Zina tofauti na hizo wanazouza Elfu 7000 machinga na pia naomba kuelekezwa machinga complex IPo mtaa Gani na pia penye maduka ya vipodozi mfano dettol ya kuogea ya mtoto unakuta inauzwa 18000 Kwa dazen lakini ukija barabani huku unakuta wamepanga chini wanauza jero jero nazo sijajua pia kama ni feli au la ila zinafanana vile vile.
 
Safi sana mkuu! Ila ukiweka na contact zao hapa ungekuwa umetuvusha sana maana katika biashara mawasiliano ndio mpango mzima!
 
Na machimbo ya( PPE's),
Yaani vitu hivi yako wapi kwa hapo kariakoo mkuu....??

gloves,
helmet,
Overall
Ear plug
Dust mask
Safety glass,
Safety boots
Cutting disc
Drill machine
Welding shield,
Angle grinders
Air compressors
safety harness belt,

Vifaa vya usalama na kazi mahala pa kazi kama Workshops na Mining areas vinauzwa wapi kwa hapo kariakoo mkuu???
Mtaa wa lindi
 
Ahsante Sana mkuu ila hizo tshert ukiingia ndani kule unakuta wengine wanaziuza Elfu 10 Kwa jumla sasa sijajua kama Zina tofauti na hizo wanazouza Elfu 7000
Machinga complex ni karume pale👇
machinga na pia naomba kuelekezwa machinga complex
Nenda maduka ya vipodozi kaulizie utapata taarifa vizuri zaidi,kuwa makini usije kuwauliza madalali watakuingiza chaka,maana wao watakuambia subiri Kwa hapa nikakuulizie kisha abakuletea bidhaa ameweka na chake cha juu

Maduka ya vipodozi mengi yapo usawa wa kituo cha mwendo Kasi cha msimbazi upande wa kushoto km unaelekea fire au ulizia big bon wapi kisha ukifika pale uliza Kwa watengeneza simu mule barabarani wqtakuelekeza maduka yalipo maana yapo Kwa ndani kidogo ..narudia tena usithubutu kuongea na watu wenye dalili ya kukuonyesha madalali/ watu wa Kati...ingia mwenyewe dukani
IPo mtaa Gani na pia penye maduka ya vipodozi mfano dettol ya kuogea ya mtoto unakuta inauzwa 18000 Kwa dazen lakini ukija barabani huku unakuta wamepanga chini wanauza jero jero nazo sijajua pia kama ni feli au la ila zinafanana vile vile.
 
Me nataka kujua chimbo la mapazia na mikoba ila nko mkoan
Mbona mleta mada ameelezea vizuri yanakopatikana.soma tena Kwa umakini

Labda changamoto niliyoioana ni watu wa mikoani kutojua majina ya mitaa na hata akiambiwa bidhaa Fulani inapatikana let say mtaa wa Lindi au shauri moyo ni kujua location ya huo mtaa Ila smartphone zipo mkuu
 
Machinga complex ni karume pale[emoji116]

Nenda maduka ya vipodozi kaulizie utapata taarifa vizuri zaidi,kuwa makini usije kuwauliza madalali watakuingiza chaka,maana wao watakuambia subiri Kwa hapa nikakuulizie kisha abakuletea bidhaa ameweka na chake cha juu

Maduka ya vipodozi mengi yapo usawa wa kituo cha mwendo Kasi cha msimbazi upande wa kushoto km unaelekea fire au ulizia big bon wapi kisha ukifika pale uliza Kwa watengeneza simu mule barabarani wqtakuelekeza maduka yalipo maana yapo Kwa ndani kidogo ..narudia tena usithubutu kuongea na watu wenye dalili ya kukuonyesha madalali/ watu wa Kati...ingia mwenyewe dukani
Ahsante Sana hayo maduka ya vipodozi nayajua Sana tu
 
Back
Top Bottom