Machimbo mazuri ya kupata bidhaa mbalimbali Kariakoo kwa bei nafuu
Wapi nitapata chimbo la barber shop chir kwa bei ya mtanzania wa Hali ya chini? Msaada plz kwa anaejua

Ukifika mataa ya fire ya kwanza kutokea Ubungo
Pale njia panda ya kwenda muhimbili, ingia kulia utaona duka kubwa Lina Vitu Vya barber shop , ukitaka Mtumba utasogea mbele kidogo
 
Screenshot_20230622-090842.png
bei ya jumla ya hizo yebo wakuu na zinapo patikana kwa kariakoo.
Screenshot_20230622-091113.png
 
Naomba msaada wa vifaa vya solar kama chaja za kobe za sola na taa za sola
 

Attachments

  • IMG_20230822_190906.jpg
    IMG_20230822_190906.jpg
    175.6 KB · Views: 15
NANUNUA,NAFUNGA NA KUSAFIRISHA BIDHAA KUTOKA KARIAKOO KWENDA MIKOA YOTE TANZANIA NA NCHI JIRANI.

HUDUMA ZA ZIADA
📌Nafuata,nafunga na kusafirisha bidhaa iliyokwisha kununuliwa Kariakoo kupitia mitandao kama fb na insta.
📌Nafanya ukaguzi na kuhakiki ubora wa bidhaa uliyonunua kariakoo kupitia mitandao kama fb na insta.
📌Nafanya malipo ya bidhaa uliyonunua kariakoo kupitia mitandao kama fb na insta baada ya kuhakiki na kukagua ubora wa bidhaa.
📌Nakusanya bidhaa,nazifunga kwa pamoja kisha nasafirisha kama mzigo mmoja kutoka kariakoo kwenda mikoa yote Tanzania na nchi jirani.

SIMU:0745645035 (PIGA/SMS/WHATSAPP)
 
Habari! Nahitaji kujua chimbo la chupa hizi kwa bei ya jumla k koo.asante
 

Attachments

  • Screenshot_20231107_140407_Gallery.jpg
    Screenshot_20231107_140407_Gallery.jpg
    74.5 KB · Views: 32
Wapendwa week end inaendaje?
Wanasema kizuri kula na mwenzako....na nomeona niwashirikishe fursa hii adimu hasa kwa wale wanaofika kariakoo na kujikuta wanauziwa bei ghali kuliko hata huku mtaani...
[emoji117][emoji117][emoji117]
SOMA HAPO UKIPENDA SAWA USIPOPENDA PITA KIMYA

Ngoja nikupe machimbo eh best kizuri kula na mwenzio...Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule mnazi mmoja wengi wanaouza k.koo wanaenda kufata huko,

Viatu navyo vinapatikana huu mtaa wa Narung'ombe na congo pale nenda straight kwenye maduka ya wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini nop unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile visandles wanauza 2500/pc.

Cheni zama mchikichi katikati kuna mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki.

Magauni nayo ingia ndanindani kule congo na aggrey wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc.

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro.

Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau?

Mapazia ya kukata jora Kama unaenda Posta upande wa chuo cha DIT na CBE, Ukishavuka ule ukuta kuna duka la mfanyabiashara ana asili ya india anauza bei nzuri na mara nyingi Jumamos anakua na bei ya SALE kwahyo unaweza kupata majora ya mapazia kwa bei chee na kila design.

NA UKITAKA DAGAA ZA KUKAANGA FRESH KABISA KUTOKA MWANZA YANI KUTOKA ZIWANI STRAIGHT KWA MLAJI UTAZIPATA KWA HUYU HAPA 0654688288

NATUMAIN MTAKUJA NA MACHIMBO MENGINE SEMENI HAPA. copy and paste
Mabegi ya Wanafunzi chimbo lake liko wapi?
January hii hapa
 
Habari! Nahitaji kujua chimbo la chupa hizi kwa bei ya jumla k koo.asante
Nenda pale mtaa vyombo mtaa wa aggrey ..pale maduka yanapoanzia karibu na mtaa wa sikukuu..nenda duka la tatu kutoka duka la wachina kuna mdada anauza , mkono wa kushoto , huyo jumla ndio anaanzania angalau piece 3 . Hizo chupa ziko 4 in 1 pale anauza jumla 15,000
 
Nenda pale mtaa vyombo mtaa wa aggrey ..pale maduka yanapoanzia karibu na mtaa wa sikukuu..nenda duka kama la nne hivi kutoka duka la wachina kuna mdada anauza , mkono wa kushoto , huyo jumla ndio anaanzania angalau piece 3 . Hizo chupa ziko 3 in 1 pale anauza jumla 15,000
Shukraani ndugu.nitafanya ivyo
 
Back
Top Bottom