Macho yangu yanaona kama yako? CCM mnaenda kuanguka na anguko lenu ni kubwa sana

Wewe huna tofauti na hao mnawaita manabii feki kina Gwajima..

Kwanza serikali haiwafukuzi inawapanga watakaokaidi lazima waone moto nchi lazima iwe na utaratibu.

Pili hao ni wachache sana huko mijini ukilinganisha na maelfu ya WaTzn ,tena wengi wako Dar,Mwanza basi kwingine hata hawana impacts ndio maana hujasikia kelele kutoka maeneo mengine.

Kwa hiyo unajilisha upepo, tatizo lilikuzwa na mwendazake lakini hatuwezi endelea hivyo likakua zaidi.

Rais kwa sasa anahangaika kurejesha uchumi wa kabla ya Magu kipindi cha JK ,pesa ilikuwepo na watu walipenda kujiajiri na biashara zilikuwa zinatoka
 
Kilichofanyika kwa Wamachinga Dar ni Maafa. Lakini kwanini Makala alirudi na anaeleweka. Haya kabadilika na wakati
 
Kila mtu anatafuta riziki lakini utafutaji huu ni lazima uwe na utaratibu, siyo uwe hovyo hovyo na unaoathiri watu wengine.

Ni ujinga kuruhusu ukiukwaji wa taratibu na sheria, eti kwa sababu ya kupata kura. Serikali ikazanie kutengeneza mazingira yatakayosaidia tuwe na wazalishaji wengi, na siyo wachuuzi. Ni uzalishaji ndio utakaotengeneza ajira, kuongeza mapato ya nchi, utaongeza fedha za kigeni, na kuondoa umaskini. Serikali iwapate super intelligent brains watakaoisaidia kimawazo na kimbinu, namna tutakavyopunguza machinga, na kuongeza wazalishaji.

Mleta mada, ameleta hoja za kipuuzi kabisa. Wapuuzi kama mleta mada kuna siku vibaka wakiwa wengi, wakizuiwa kuwapora watu, atasema waachwe, wakiondolewa CCM itakosa kura.
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Wamachinga wanakuathiri vipi wewe? Hauingizi kipato? Watoto wako hawasomi? Chuki na ubinafsi vikizidi ni chanzo cha kuvunjika amani. Jiulize machinga wasikie hayo maneno yako inakuwaje?

Kesho zikianza roba za mbao na matairi kutobolewa na misumari utataka serikali ikusaidie.
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Uko sahihi ila ila athali zao kukosa sehemu muafaka watu hao ni kuingiza jeshi mtaani usilojua namna ya kulidhibiti serikali wao ni chanzo cha tatizo wanapaswa walitataue kwa busara kuliko njia wanazotumia maana ni kama uporaji unamtoa mtu.barabarani huku na mtaji wake umemaliza wengi tunaopinga machinga ni kwa vile sisi tunafanya kazi maofisini na kutoona taabu zitawakuta na maamuzi watayochukua baada ya mitaji yao kukata
 
Tulia dawa ikuingie we chawa wa mwendazake
 
Anguko kuu la CCM itakuwa ni Independence ya pili kwa Tanzania na Watu wake.
 
Inaangushwa na nani?
 
Lia lia kama kawaida yetu, tukiwaambia tuandike katiba mpya hamtaki, ujinga na upumbavu tu umetawala ndo maana ccm inawageuza inavyotaka
 
Kwa upinzani upi sasa

Mbona mna macho yanayoona upande mmoja
 
😂kuna watu hawatakuelewa hapa wataishia kukutukana, ngoja waje wazalendo
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Sawa machinga ni kero kwajamii yako wewe unayekosa parking ukienda kariakoo, je huyu mtu unaweza kumuhudumia yeye na familia yake kuanzia kula kulala kuvaa na matibabu pindi atakapovunjiwa banda lake au biashara yake nyumbani kwako? Kama wabunge wenu wanasema wahitimu wajiajiri wasitegemee kuajiriwa. Unataka wafanye nini?
Kisa tu wewe upo kwenye system inayokupendelea , usije ona wenzako wanao taabika kwenye jua kali na mvua kuwa hawana haki yakula mema ya nchi hii .
 
Hao wamachinga ni raia wa nchi gani? Kama ni Watz hamna kitu kitatokea, mark my words...
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Machinga ni baba, ni mama, ni babu, ni bibi, ni mke, ni mume, ni mtoto! Dkt Magufuli aliposema msiwabuguzi alimaanisha tutafute njia inayowapa pia unafuu chinga. Tusiwabague wala kuwaona wabaya.
 
CCM inawaogopa wamachinga; Machinga leo ana uwezo wa kupanga biashara yake mbele ya nyumba yako na huthubutu kumgusa!!

Machinga walishagundua weakness ya CCM - sasa Kariako halipitiki - huku mtaani nako njia zote ni meza na matenga matupu !!

CCM oyeeeeee
Machinga oyeeeeeeee
Jiji la Dar es salaam oyeeeee

kazi iendeleee...!!
 
Umeongea nonsense kabisa

Pathetic fool
 
Ni jambo jema kabisa machinga kuondolewa maeneo hayo, Mh rais watafutie eneo nje ya mji.
 
Kwenye hili la Wamachinga nitasimama na serikali yetu. HAIWEZEKANI WAMACHINGA WASAMBAA NA KUFANYA BIASHARA KILA MAHALI..tena tulichelewa sana kufanya uamuzi juu ya hili. BARABARA ZOTE ZA MIJI ZIMEJAA VIBANDA NA HAMANA KULIPA KODI. big NO to Machingas
Tatizo haohao waliruhusu hii hali eti wanaweza kuiondoa?haiwezekani wamefika mwisho panahitajika wengine wanaoweza kufikiri tofauti na hao vinginevyo itakuwa ni vurugu na hakuna kitacho kaa sawa kama mnabisha shauri yenu
 
Hujanielewa, nimesema, wapewe catalog/ setup ( kwa lugha nyepesi naweza kusema muundo) na serikali kwamba hii ndio standard, wao sasa wakatengeneze za kwao, ila ziwe nafuu na zakupendezesha mji.
Unaongelea nchi gani? Huyo mmachinga wa kumpa kiwango atengeneze ni wa hapa! Na akishatengeneza aliweke wapi zaidi ya katikati ya barabara.
Wengi wa hao wamachinga wanalala kwenye mabanda yao.
 
Reactions: Ame
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…