Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

1. Ni mkopo wa USD 24 billion. Yaani nusu ya deni la taifa la sasa. Ukiongeza na riba yake ni zaidi ya hapo.
2. Bandari itamilikiwa na kuendeshwa na China kwa miaka 99.
3. Hawatalipa kodi yo yote ya TRA kwa kipindi chote hicho ila wanaweza kutupatia mrahaba watavyoona.
4. Wakwere wa Bagamoyo na watanzania wengine hawataruhusiwa kuingia maeneo hayo.
5. Itakuwa eneo la manoari za China (millitary base).
6. Mkataba wake utakuwa ni wa siri na hauruhusiwi kuonwa na wabunge au mtu mwingine ye yote yule isipokuwa Spika Ndungai tu.
7. Bidhaa zote kutoka China zitapitia bandari hii pekee ambazo zitasambazwa pia kwenye nchi jirani.
8. Hakuna mambo ya win win ila Tanzania itakuwa kama Uchina.
9....
10.....
Asee wajinga bado mpo wengi
 
Mkataba wa ununuzi wa ndege uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa Watanzania?

Mkataba wa bwawa la Nyerere uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa Watanzania?

Mkataba wa SGR (segments zote) uliuona? Ulijiridhisha ulikuwa na maslahi kwa Watanzania?

Usiwe bendera fuata mkumbo. Hii nchi mikataba haijawahi kuwa na ahueni. Mikataba yote huwa tunapigwa mjomba. Ishu huwa ni nani ananufaika na kupigwa kwetu, nakuhakikishia hata mikataba enzi za Jiwe ilikuwa tunapigwa mno!

Tuungane kudai katiba itakayotaka mikataba yote kuwekwa hadharani kabla haijasainiwa

NB
Sina maslahi na bandari ya Bagamoyo wala siungi mkono mkataba unless uwekwe wazi
Busara ikutume ufiche huu upumbavu wako. Miradi yote uliyoisema hapo juu tunaitekeleza wenyewe, labda kama unataka kuona mikataba ya ujenzi na wakandarasi waliopata tender.

Huu mradi wa Bagamoyo unakwenda kutekelezwa na wachina na watu wa oman. Swali ulililotakiwa kujiuliza, Sisi kama taifa tunakwenda kunufaikaje? Hoja zilizotolewa na Serikali iliyopita, lini zilishawahi kupatiwa majibu? Na kwanini wachina wanaung'ang'ania sana huu mradi kuliko hata sisi ambao tunaambiwa ndo wanufaika wakuu. Unahisi wanatupenda sana

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
This is your own judgement. I don't blame or praise anyone but I do blame people who have, by their will, betrayed their thinking capability. How can we equate everything to the poor thought of one foolish man. Let allow people to think. The nation is bigger than one of US. I stand with the nation not else.
I second you Sir[emoji108][emoji108]
 
Mtume Muhammad( SAW) alipata kusema kuwa
"IMEANGAMIA KAUMU ITAKAYOONGOZWA NA MWANAMKE"
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Mkuu tatizo siyo wachina, tatizo ni sisi wenyewe, miaka nenda miaka rudi viongozi wa CCM na serikali zake ndiyo wamekuwa wakiridhia mikataba hii, wakiweka maslahi yao mbele.

Mikataba yote huwa inabidi ipite kwa mwanasheria mkuu ili ichambuliwe kwa kina kisha irudishwe kwenye majadiliano hatimaje iridhiwe na bunge. Hilo halijawahi kufanyika kuanzia kwenye madini, gesi, mafuta, SGR, ndege, bwawa la Nyerere na sasa bandari ya Bagamoyo.
Tuwaulize ninyi CCM kulikuwa na uharaka gani wa kusaini mikataba 22 usiku bila ya kuangalia vipengele vyake vinasema nini?

Kote ambako wachina wanalaumiwa mazingira ni hayo hayo. Mkataba unaandaliwa China, viongozi wanafanyiwa sherehe, wanapagawa mwisho wa siku wanasaini. Wananchi mnakuja shtuka mko utumwani na viongozi wenu wamestaafu kwa raha mustarehe.
Mungu atuepushe na balaa[emoji120]
 
Mtume Muhammad( SAW) alipata kusema kuwa
"IMEANGAMIA KAUMU ITAKAYOONGOZWA NA MWANAMKE"
Sidhani Kama alimaanisha unavyofikiri wewe. Tatizo mnaquote mistar robo kwenye misaaf na bible halafu mnapotosha. Siamini mtume alikua muumini wa mfumo dume. Mwanamke ni muhimu Sana hapa duniani. Hata mwanzo Mungu alipomuumba Adam aliona jinsi amepwaya , alishindwa maisha mpaka akaletewa Hawa.
 
Dhumuni la Mungu kumleta Hawa lilikuwa nini......??
 
Busara ikutume ufiche huu upumbavu wako. Miradi yote uliyoisema hapo juu tunaitekeleza wenyewe, labda kama unataka kuona mikataba ya ujenzi na wakandarasi waliopata tender.

Huu mradi wa Bagamoyo unakwenda kutekelezwa na wachina na watu wa oman. Swali ulililotakiwa kujiuliza, Sisi kama taifa tunakwenda kunufaikaje? Hoja zilizotolewa na Serikali iliyopita, lini zilishawahi kupatiwa majibu? Na kwanini wachina wanaung'ang'ania sana huu mradi kuliko hata sisi ambao tunaambiwa ndo wanufaika wakuu. Unahisi wanatupenda sana

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Wapi uliona mchina anang'ang'ania mradi??? Mchina ashaitwa Mozambique akafanye kama huu, ni JUKUMU LA Taifa letu kuwawahi wachina tukae nao chini tuyajenge, tusije tukapoteza hii fursa. Na ujue sio mchina tu ndo yupo kwenye huu mradi, Oman pia wapo. Acheni propaganda. Dubai ilianza hivi hivi. Mbona hamlalamiki kigogo busisi na chato airport??
 
Dhumuni la Mungu kumleta Hawa lilikuwa nini......??
Hawa aliletwa Ili amfungue akili Adam. Mwanamke Ana uwezo wa kufkiri, kuona mbali na kuelewa kuliko mwanaume. Akifikisha 50yrs akili yake inazid kukomaa. Wakati ya mwanaume inaanza kupungua. Mkuu nawakubali Wanawake Sana. Wana viungo vilaini lakini ubongo wao ni mgumu kuliko mwanaume.
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Tuambie kwanza, mradi wa Kiwanja cha ndege Chato umekusaidiaje wewe moja kwa moja.

Tulikuwa na Rais risasi fisadi uchwara.
 
Hiyo bandari Ingekuwa ni chato ingejengwa haraka sana!! Lakin kwasababu ni Bagamoyo utaambiwa wachina ni wabaya. Umejengwa uwanja wa ndege wa kimataifa chato sijui hata wa kazi gani, lakin hujalia wala kulalamika, zimenunuliwa ndege 11 za gharama ya trillion 1.2 ambazo zimepaki tu zinapigwa mvua na kuozeshwa na chumvi ya Dar, lakin wala hulii!! Tatizo mnachukulia maneno ya lile chizi kama torati, totally brain washed!! Poleni sana wanyonge
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Ujenzi wa bandari kama ni muhimu nadhani tunaweza kuutekeleza bila kuwatumia hao wachina na mikataba yao mibaya.
 
Ccm kuwaelewa yataka moyo sana, kikwete alitaka ijengwe magufuli akapinga, serikali iliyopo sasa kama inataka ijengwe, kivumbi kilimkuta spika yeye kila beat anatoa verse
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Mimi kwa upande wangu hilo la mradi huo kujengwa na Mchina halinipi shida, bali linalonipa shida ni uharaka wa kufufua mchakato wa kutaka kuanza tena ujenzi wa bandari hii ya Bagamoyo. Rais aliyetangulia alikwisha kutuambia ya kuwa kuna kasoro na mapungufu makubwa ndani ya mkataba wa ujenzi kiasi kwamba akafikia uamuzi wa kuachana nao.

Cha kushangaza leo yapata miezi mitatu toka aondoke madarakani, viongozi walewale ambao waliokuwa katika safu yake ya uongozi, ambao walikuwa sambamba naye katika uamuzi huo, sasa nao wamebadili uamuzi. Eti wanadai alipotoshwa! Alipotoshwa na nani wakati wao wenyewe ndio walikuwa ni wasaidizi na washauri wake wakuu?

Viongozi hawa kwa nini walikubali gharama kubwa ya TZS 350Bn itumike katika upanuzi wa gati zilizopo katika bandari ya Dar es Salaam? Gati namba 1 ambayo ilihusisha kuongeza eneo la kupakia na kupakua mizigo pamoja na kuongeza kina cha maji mpaka mita 14.5 na kazi kama hiyo kwenye Gati Namba 2 mpaka 4.

Kama gharama kubwa zimekwisha kutumika kwa ujenzi wa gati, wala pasipo kuangalia "pay back period" yake, tunaanza tena uharaka wa kukimbilia mradi mwingine mkubwa ambao utakwenda kuiathiri kabisa bandari ya Dar es Salaam.

Mkataba huu wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uwekwe wazi ili wananchi wapate kuyaona mazuri na mabaya yaliyomo ndani mwake. Viongozi kupata dhamana ya kutuongoza siyo kuwa wamepewa uhalali wa kutekeleza maslahi yao binafsi ama ya kikundi fulani cha watu, bali ni kujali maslahi mapana ya taifa.
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.
Unajua huo mkataba au mnashikiwa akili tu.
 
Wewe ulikuwa segerea nn wkt wanasema vifungu vilivyomo kwenye mkataba? Kama huyo mama yenu ni mkweli na mwenye kutaka mema kwa watu wake apeleke Bungeni huo Mkataba ukachambuliwe
Hahahaa, sasa kule bungeni kumejaa babu tale watupu unategemea nini?
 
Hata Dubai wangeugomea uwekezaji wa matrilion ya dola miaka hiyo leo hii nchi yao isingekuwa HUB ya dunia kwa usafiri wa anga na mahotel ya kifahari.

Watanzania msiogope uwekezaji...hiyo ni roho ya kimaskini.
Hakika
 
Ajabu yenyewe watu wanaolilia kupandishiwa mishahara, kujengewa barabara, kupewa ulinzi, watoto zao waende shule nzuri, serikali ikidhi wafanyakazi sector ya afya na vifaa tiba vya kileo.

Kutaja mambo machache ambayo hakuna mwekezaji atakufanyia kwa hela yake ni jukumu la serikali pekee; ndio watu hao hao wanaopiga kelele serikali iingie mikataba itakayopteza mapato chungu mzima kwa miaka kibao na kukosa hayo mahitaji wanayolilia kuwafikia haraka.

Mchina umeambiwa anarudisha hela yake ndani ya miaka 10 kwa makadirio ya juu ya mapato na kwa makadirio ya chini miaka 15; serikali wamewapa miaka 30 ya kuvuna. Mchina hataki anataka apewe 99 years.

Mchina anataka industrial park iwe sehemu ya mkataba wa bandari; serikali imemwambia hapana ajenge hivyo viwanda viwe vyake mwenyewe na sehemu wamempa bure serikali ivyo viwanja imeshavilipia fidia.

Isipokuwa huo uwekezaji wa viwanda uwe kama wa wawekezaji wengine wa kigeni kama kuna benefits zozote watazipata huko huko wizara ya viwanda kama wenzao hakina Dangote; lakini TPA aina interest na viwanda vya mchina.

Mie nadhani kuna wakati tukubali tu hii nchi walalahoi siku tukichoka ndio tutaikomboa; kwa sasa kama mkate unaenda kinywani vitu vingine kubali tu yaishe. Maana wale wanaopiganiwa ndio wanazi wakubwa wakushangilia ujinga.

That reminds me of Spike Lee classic movie “She is gotta have it” ndio watanzania kuna wasaa unaona waachwe tu yawakute.
 
Back
Top Bottom