Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Lowasa alisema mradi haufai.

Magufuli alisema ni mjinga pekee atakaye saini mkataba na akauvunja.

Kwanini rais Samia hauweki mkataba wazi tuusome wote.
Atakuwa ndio yule kichaa anayeweza sign huo mkataba
 
Wazee tumekwisha rasmi. End of the game.

Bado ardhi tu, tubaki kuwa watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe.

China inalalamikiwa kote Duniani Kwa kufanya miradi inayowaumiza wazawa, sasa zamu yetu imefika rasmi.

Walau kwa hili, Magufuli tutamkumbuka mno. Hii bandari ina maslahi makubwa sana kwa Wachina kuliko watz.

Hapa ni pdf guy akijaribu kutazama umuhimu wa Bahari kwa sisi watz. Nimemuelewa sana huyu jamaa.

Hapa pia kuna video ya Magufuli akijaribu kuweka dondoo ya nini kilichomo kwenye Mkataba wa Bandari ya Wachina (Bagamoyo).

Kuna uzi pia Lowassa akisema huu mkataba atauvunjilia mbali huko.

Huenda watanzania Mungu amewakataa hapa Duniani na hata Mbinguni. Endeleeni kumuuliza Mungu Kwa upole na unyenyekevu mkubwa sana.

Kwenye Madini tumepotezwa. Hayati JK Nyerere aliwahi kusema Madini tusichimbe hadi tuwe na uwezo wa kuhakikisha yanatunufaisha, hatukusikia na sasa kila mtu anajua kinachoendelea kwenye madini.

Gesi imepigiwa kelele nyingi haijawahi kutokea lakini kila mtu anajua kinachoendelea na gesi kwa wananchi wa kawaida. Ndio ardhi yetu inaondoka hivyo wazee.

Hizi ni nyakati za kujikabidhi mbele za Mungu kila mmoja kwa imani yake. Tumekwisha, muda si mrefu hili litabainika. Hakuna ajira, watu hawana hela, maisha magumu hakuna matumaini tena.

Mungu uturehemu.
Tangu lini China kawa adui wa Tanzania au CCM? Sio hawa wachina ambao balozi wao wanahudhuria vikao vya chama?

Sio Magufuli aliyekuwa anatumbia kuwa wazungu ni mabeberu? Lini aliwahi kusema wachina ni mabeberu?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Asee wajinga bado mpo wengi
Wewe mwelevu tuelimishe basi sisi wajinga. Au utasema hayo niliyoyaorodhesha yako kwa mjibu wa sheria yetu ya Export Processing Zones Act (EPZ act).
 
Kwa hili Mama Samia naomba tafakari upya, tena Mungu akuongoze sana
Acha kumshirikisha Mungu kwenye vitu vya kipuuzi hujui chochote kuhusu bandari ya bagamoyo umelishwa matango pori na mwendazake unabwabwaja kama fala humu
 
Hivi mkuu unafahamu malengo hasa makubwa ya hiyo bandari?kwani mnalishwa matango poli tu na kuyamumunya !!bandari ya bagamoyo shughuri zake wala haitahusiana kabisa na bandari nyingine, kama mi meli mikubwa tena mikubwa kweli ya kuanzia mita 400 urefu, yanatoa bidhaa china kwa ajiri ya masoko ya afrika na sehemu nyingine, yanaileta hapo bagamoyo, kuanzia hapo ina bebwa na meli za kawaida na kuipeleka sehemu hizo, na bidhaa nyingine zitakuwa zinatengenezwa hapo.sasa kwa shughuri hizi hizi bnadari zetu nyingine zitakufa vipi?!!
Haa hayo ndo mnadanganywa eti meli za mita 400 nani amekuambia ndo tu zitakazokuja hapo
 
Mbona huu mradi hata kipofu hawezi kutia saini yake.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mchezo unaanza hivi.......

Bidhaa nyingi zinazoagizwa nje ya nchi zinatoka China na wabia wakuu wa kuagiza bidhaa hizi wanatoka china

Halafu wachina wawe na bandari yao, hivi unategemea hizo bidhaa zitashushwa kwenye bandari ipi?

Wachina watajenga bandari yenye hadhi na yenye uwezo mkubwa wa kuhudumia mizigo mingi kwa wakati mmoja tofauti na hizi bandari zetu nyingine hivyo kupelekea wateja wengi wa mizigo kushusha mizigo yao kwenye hiyo bandari

Mchezo utaisha hivi.....[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Hakuna mfanyabiashara atakae taka kushusha mizigo kwenye hii bandari ya dar yenye mizengwe mingi

Hili litagharimu taifa kwa miaka mingi Sana

Mama oyeeeee.......
Ndo ukweli huo na automatic bandari ya dar itakufa natural death , na jira za ndugu zetu zitapotea maana bandari bagamoyo itakuwa Kama ni guazou ndogo , serikali wataweza kutia mguu hapo
 
Sikuwahi kudhani Tanzania tuna uhaba wa Port mpk tuwauzie wachina Bagamoyo tumekarabati Bandari ya Dsm na Bandari zingine kwa gharama kubwa kabisa lakini leo tunakwenda kuziua bandari zote

Namuona Yuda ila sijui alimsaliti mwenzie kwa vipande 30 vya fedha au kwa ahadi ya kupewa kitu!!
Wapiga dili wamesharudi kwa speed....
muda utasema
 
Acha kumshirikisha Mungu kwenye vitu vya kipuuzi hujui chochote kuhusu bandari ya bagamoyo umelishwa matango pori na mwendazake unabwabwaja kama fala humu
Sawa. Najua umetanguliza mbele matusi kwa kuwa ndio hazina yako.

Mm acha nitangulize hekima na busara Kwa sababu ndio hazina yangu, yaani kila mmoja ana hazina yake hapa, na kila mtu hutoa alichonacho. Yaani km una harufu mbaya unatoa harufu mbaya na kama una harufu nzuri basi unatoa harufu nzuri. Sayansi na hesabu ya maisha ipo hvyo siku zote
 
Sikuwahi kudhani Tanzania tuna uhaba wa Port mpk tuwauzie wachina Bagamoyo tumekarabati Bandari ya Dsm na Bandari zingine kwa gharama kubwa kabisa lakini leo tunakwenda kuziua bandari zote

Namuona Yuda ila sijui alimsaliti mwenzie kwa vipande 30 vya fedha au kwa ahadi ya kupewa kitu!!

Hili sidhani kama lina baraka ya watanzania walio wengi. Kuna watu wameamua kufanya hili jambo bila kujari watanzania wanaliona vipi. Litaleta manjonzi na lawama. Liangaliwe upya
 
Sikuwahi kudhani Tanzania tuna uhaba wa Port mpk tuwauzie wachina Bagamoyo tumekarabati Bandari ya Dsm na Bandari zingine kwa gharama kubwa kabisa lakini leo tunakwenda kuziua bandari zote

Namuona Yuda ila sijui alimsaliti mwenzie kwa vipande 30 vya fedha au kwa ahadi ya kupewa kitu!!
Acha kukifanya una uchungu wakati ulikuwa unashangilia Kijiji cha Chato kujengwa kuwa jiji
 
Huwez ukawa na akili timamu kuja hadharan kumkumbuka mwendazake,kuondoka kwake na kuja kwa mama it's a blessing in disguise,kazin iendelee
 
Back
Top Bottom