Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Kama wataondoa hayo mapungufu makubwa basi utakuwa ni mradi mzuri sana kwa watanzania.

Hakika Tunahitaji sana huu mradi isipokuwa usiwe na hasara kwa watanzania.

Usiwe wa kinyonyaji.

Usijeleta hasara na majuto .
 
Nakumbuka bungeni wakati ule ulipopelekwa kama Zimamoto wapinzani walitaka utolewe muda wa kutosha kuupitia kwa kina na kujadili .

Ikafanyika hila ilipelekea wakasusa na kutolewa ukumbini.

Wakadhihakiwa sana na wabunge wa CCM .

Sasa awamu ilofuata wananchi tukaambiwa mradi wa bagamoyo haufai hata kidogo.

Sasa tuamini kinanani?

Mbona bunge wakati ule walipitisha kwa Zimamoto style?
 
Haya mambo nyie mnayatoa wapi mbona wengne hatujauona huo mkataba? Kwa nn hawataki kutupatia mbona sauti za akna Nappe na Makamba wanamteta malaika zilitolewa?
 
Mboyi utapata tabu sana!! Bagamoyo ni muhimu sana kuliko utumbo wako ulioandika hapa wewe PUSH GANG.........Kazi iendelee Mikumi tena kwa Mh SSH.
 
Wewe kwa ujinga wako unajua hiyo miradi yote umeitekeleza mwenyewe? Huna haya kuwaza hivi? Eti tunaitekeleza wenyewe, pimbi sana wewe.

Bwawa la umeme la Nyerere umetoa hela zako na unajenga na suma JKT?

Hizo ndege ulizonunua kwa cash ulitumia hela ulizodhulumu kwenye korosho? Au ni kodi uliyokata waalimu kwenye mishahara. Unajua deni la Taifa limefika ngapi sasa hivi?

Kuna siku mkataba wowote wa mradi mkubwa uliwahi kuwekwa hadharani au hata kupelekwa bungeni kujadiliwa? Hujiulizi ni kwanini?

Anyways, jumapili njema usinipotezee mudi yangu ya weekend bure.
 
Hiyo ni hujuma, ililetwa awamu ya 4. Bingo kubwa walichuma kuidhinisha mradi huo. Vizazi vijavyo vitalia sana.
 
Wewe ulikuwa segerea nn wkt wanasema vifungu vilivyomo kwenye mkataba? Kama huyo mama yenu ni mkweli na mwenye kutaka mema kwa watu wake apeleke Bungeni huo Mkataba ukachambuliwe
Bunge lipi, la spika Ndugai?
 
Halafu hata ukipelekwa upya bungeni kwa sasa napata tashwishi .

Kina nani watasoma huo mkataba between lines?

Kina nani watausoma kwa umakini ?

Kama haitasomwa kwa umakini hata mjadala wake hautakuwa na manufaa.

Waliosemekana kuwa hodari wa kusoma mikataba na nyaraka bungeni ilisemekana ni wabunge wa upinzani kwa kiasi kikubwa,

Je wapo ?

Kina Dr. Slaa, Lissu, Zitto Kabwe, John Mnyika, Heche n.k

Jamaa walikuwa hawalali wanasoma kwa umakini mkubwa sana.

Wakati wengine wameenda kwenye starehe na kulala wao wanakomaa kusoma kwa manufaa ya Umma.

Siku hizi kina nani watakesha kusoma mikataba, budget na nyaraka kabla ya kujadiliwa na kupitishwa na bunge?
 
Well, hana cha kupoteza. Watu wanawahi 2025, the "Gangsters" hawako tayaari kufanya makosa mara 2. Cha msingi kwa sasa tuwaunge mkono ili wakati wa kulia, tulie wote.
Dah
 
Hivi mikataba si ndio siri?
 
Wanaolalamika ni wavivu wa kazi na kufikiri, Africa imewalalamikia wazungu kwa miaka yote na kila siku wanawalaumu kuwa ndio chanzo cha umasikini, ukweli umasikini ni uamuzi wao, China ilikubali kushirikiana na wazungu na sana ni Matajari, Lazima tukubali kushirikiana na nchi zilizoendelea ili kupata maendeleo, Na ushirika lazima uwe wa muda mrefu.
 
Hata Dubai wangeugomea uwekezaji wa matrilion ya dola miaka hiyo leo hii nchi yao isingekuwa HUB ya dunia kwa usafiri wa anga na mahotel ya kifahari.

Watanzania msiogope uwekezaji...hiyo ni roho ya kimaskini.
Hatuogopi ila tunataka tuwekwe wazi na uwe wa win-win situation

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Nyie Mataga Pori sasa mnatuchanganya.
Sio nyie mliosema kuwa Wachina ni ndugu zenu??
 
Yani tuna bandari mbili karibu hv kwanini bandari hiyo isijengwe Tanga au Mtwara.. Yani sasa bandari ya Dar itakuwa na kazi gani
 
Hata Dubai wangeugomea uwekezaji wa matrilion ya dola miaka hiyo leo hii nchi yao isingekuwa HUB ya dunia kwa usafiri wa anga na mahotel ya kifahari.

Watanzania msiogope uwekezaji...hiyo ni roho ya kimaskini.
Akili huna hiko ndio minachojua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…