Machozi yamenitoka kusikia Bandari ya Bagamoyo itajengwa, tena na Wachina

Mkuu baada ya Nyerere aliyekuwa na machungu na nchi hii aliyefuatani Raid Mpendwa Magufuli. Waliobaki na mamisheni town tu!!!
 

Tumerudi kuwa shamba la bibi. Inaleta uchungu mno. Wanaotaka kutula wanafanya kama wapendavyo. Serikali imerudi kwao. Angalia mfano wa COVID 19. Serikali tayari imeshaagiza chanjo sasa inahaha kuwaaminisha wananchi kuwa hiyo chanjo inahitajika. Wanasema mgonjwa hakohoi wala kupiga chafya; lakini wanasisitiza barakoa. Hewa haijachafuliwa kwa kikohozi wala makamasi, sasa barakoa ya nini? Ndio maana wakati mwingine inabidi tusipuuze sana kuwa aliyepinga mambo yote hayo kwa nguvu zote kaondolewa duniani na binadamu. Huu mkataba wa bandari ulizungumzwa na masharti yake ikaonekana ni wa kuihujumu nchi. Yule mkurugenzi wa bandari mjuaji wa mambo ya bandari kawa wa kwanza kufukuzwa kazi. Tena naamini yuko hatarini sana. Hawa wachina wanaojua kuwa yeye ndiye anayefahamu ukweli hawana amani wakimwona akiwa yu huru na hai.
 
Umeandika Upu.uzi kabisa. ama kweli Jiwe alishika akili za wengi
 
Inasikitisha sana Jiwe alifanikiwa sawa ku brainwash wajinga wengi. kwani miradi mingapi imefanyika nchini umeiona mikataba yake?
 
Wala hata haujui kwa undani ulichoandika na unachokilalamikia.
Yani sisi ardhi yetu itapoteaje wakati hatukopi hela ni watu wanakuja kuwekeza pesa yao??? Pendeni kufanya research kabla ya kuja kulalamika huku
 
Kwa tulivyoelezwa na JPam kama yalikuwa kweli basi inasikitisha sana kwamba kuna watu wako tyr kulinda maslah yao kuliko ya Nchi duh ! Mbona hawakumjibu kwa kuitetea kuwa bandari hii Ina maslahi kwa Taifa ??!!! Aisee nimehuzunika, hatuna msimamo kila ajaye ana lake mmh
 
Uzuri ni kwamba Sheria za kimataifa zinaruhusu nchi husika kuvunja mkataba Kwa maslahi ya Taifa.

Hivyo hawa mabeberu acha waingie mkataba wao wa kilaghai.

Wajenge bandari Yao feki.

Mungu wetu mkuu atainua wakala wake , ataufutilia mbali.
 
Haya ndiyo matokeo ya kuwa na utawala wa majaribio ambapo anayetawala ni mwingine. Nadhani Kikwete sasa karudi madarakani kwa mlango wa nyuma. Huyu mama muda si mrefu atageuka maafa. Naona kama ruksa ya mwinyi na ubabaishaji na uzururaji wa Kikwete vinarudi kwa mlango wa nyuma. Hapa anachofanya mama ni kuzidi kuiumiza CCM. Wamejisahau baada ya Magufuli kuwaokoa na tishio la kutupwa nje.
 
Inauma SANA, kila mmoja anakuja na lake
 
Uzuri ni kwamba Sheria za kimataifa zinaruhusu nchi husika kuvunja mkataba Kwa maslahi ya Taifa.

Hivyo hawa mabeberu acha waingie mkataba wao wa kilaghai.

Wajenge bandari Yao feki.

Mungu wetu mkuu atainua wakala wake , ataufutilia mbali.
Amen
 
Uzuri ni kwamba Sheria za kimataifa zinaruhusu nchi husika kuvunja mkataba Kwa maslahi ya Taifa.

Hivyo hawa mabeberu acha waingie mkataba wao wa kilaghai.

Wajenge bandari Yao feki.

Mungu wetu mkuu atainua wakala wake , ataufutilia
Unaelewe maana ya mkataba au unajifurahisha
 
Ikiwa asili yako ni Iringa unasubiri nini kumaliza kesi?
 
Hizi zote, mazingaombwe n.k yamo kwenye earmarks za ilani ya CCM.
 
Katika hiyo miradi yote kuna nchi au kikundi cha watu wanao umiliki?
 
Mijitu ya bara bwana mnajifanya mnauchungu na nchi eti machozi yananitoka.yote wivu kuona mikoa ya pwan inazidi kuinuka.
 
Magufuli si alisema wachina ni ndugu zetu?
 
Mleta mada usilie asilimia 99 ya Bunge wapo mjengoni Kwa juhudi za Magu, watahakikisha wanapigania maono yake na bahati nzuri wana mamlaka ya kuitisha mkataba. Kama huwaamini kuna katiba day twitter, jiunge japo umechelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…