Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Hakuna Sheria inayomruhusu "Konda" wa Gari la abiria kuzuia wanafunzi wasipande magari hayo. Hapo ni kuwa, "Konda" huyo anakuwa ameamua tu kukiuka Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)
Hakuna uzimamizi wa sheria, wanaotakiwa kufanya hivyo wamelala, bodaboda hawavai helmet, gari mbovu ziko road, service road zimejaa biashara, jumlisha hili la kunyanyasa wanafunzi.

Wanaowajibika kusimamia na kutekeleza sheria, na sisi wananchi tuko kimya.
 
Siyo lazima nijibu Kila kitu kwa kuwa haya ni maoni na siyo mahakamani ambako lazima ujibu hivyo, kama unayo mengine tiririka tu kwa kumbukumbu na matumizi ya baadae tafadhali 🤗
Mie ukinijibu lile swali, basi ndo nitaendelea na mengine kutiririka. Maana ni muhimu lile swali kujibiwa na kutolewa ufafanuzi.
 
Maoni hata wewe unaweza kuyapeleka tu moja kwa moja Ili yabaki original bila usanifu. Namba zenyewe kwa urahisi wako ndiyo hizo hapo tafadhali
Sitaki maoni uyapeleke kwa LATRA, nataka uyapeleke huko Serikalini, kwenye vikao vya bunge, na baraza la mawaziri.

Najua umeelewa sasa.
 
😂😂😂😂We jamaa bwana,kwa hiyo matusi yako ndio ukajua konda kaogopa?
 
Na vitoto vya siku hizi mayaimayai sana...Wenzao tushakula rumba sana kwenye DCM za TMK -Mwenge,na unasukumana na konda hadi unawahi kwa Kipingu....sasa siku hizi konda anawaambia hao watoto hakuna kupanda vimekaa tu kama vi broiler vinapelekwa kibra.We LIKUD njoo huku uone raha ya kusoma shule za serikali.
 
1. Wanafunzi wapelekwe shule za karibu ambazo wanaweza Kutembea kwa mguu.

2. Serikali iweke idadi ya Wanafunzi kuingia kwenye daladala kwa kila trip.

Serikali isiingilie biashara za watu Kwa kisingizio cha Sheria.

Kama serikali inajali Sana inunue mabasi ya serikali kwaajili ya huduma hiyo. Au wapande Mwendokasi.

Au itoe fungu au kupunguza sehemu ya Kodi kwa wamiliki WA daladala kwa lengo hilo.
 

Kama inajali.
Na sio ijali kwa gharama ya biashara za watu binafsi. Hiyo ni dhulma
 
🤣🤣🤣🤣

Haya sasa twende kazi. Kimbia haraka Sana Hadi kwenye shule ya Ems kawatoe watoto wako huko uwalete Kayumba.

Thank me later
 
Sitaki maoni uyapeleke kwa LATRA, nataka uyapeleke huko Serikalini, kwenye vikao vya bunge, na baraza la mawaziri.

Najua umeelewa sasa.
Wewe ndugu nahisi unapenda ligi za maneno 😅... Nimesha reply hoja zako nyingi, sasa hapa lazima apatikane mmoja ajiongeze kuwa, kunyamaza nako huwa siyo ujinga, ni kuruhusu hekima ijidhihirishe. Haya Kila la heri ngoja niangalie na wengine wanasemaje mimi ligi za maneno hapana kabisa😅
 
Acha

Huu ndo ujinga wa ccm nguvu nyingi bila akili .
 
1.Hilo ni tatizo sugu hapa mjini,mzazi anakaa msakuzi anapeleka mtoto diamond au Bunge..ni sifa za kijinga zinazo mtesa mtoto

2.walishatoaga idadi nadhani ni 2 up to 5 kama sikosei

3.Serikali ni mfumo wa kukandamiza wanyonge,ndio maana hata ardhi japo unailipia kila simu bado serikali imejitanabaisha ni mali yao,usishangae hata hizo daladala wanaona ni zao

4.Ukiongelea Mwendokasi ndio jinamizi lingine jipya,hao watoto wenyewe ndio wanabanwq mle hadi unakaonea huruma...huo mradi ni failure
 
Dr nimesoma reply zako nyingi ukiongelea kutoa maoni hii hoja yako watafuta utetezi uonekane kwenye kitengo chako wewe huna kosa

Wewe ndio umeleta mada humu sisi tunatoa maoni kulingana na mada uliyoleta usingeileta tusingeshughulika nayo kwahiyo usikwepe majukumu, wewe ni mtu wa serikali lakini pia ni mwanajamii peleka haya maoni huko kwenye vitengo vyenu na bungeni mtoe hizi sheria kandamizi utakuwa umesaidia Sana kuliko kujiona sio part ya tatizo hili
 
🤣🤣🤣🤣

Haya sasa twende kazi. Kimbia haraka Sana Hadi kwenye shule ya Ems kawatoe watoto wako huko uwalete Kayumba.

Thank me later
Aaaaah thubutuuuu
Mama yao nilishakula sana hizo mbilinge wao wanasubiri honi hapo getini🤣🤣🤣🤣
Halafu mbona hizo shule watoto wenu wanawahi sana kurudi?juzi nimemuona mtoto wa jirani std1 kaenda saa nne karudi saa sita au ndio ule mtaala mpya umeamua kupumzishe watoto akili?
 

Hatari Sana.

Wewe unakaa Bunju au Kijichi huko unataka upeleke mtoto Bunge kwa kutegemea hisani za makondakta. Mtoto kutwa nzima kuhangaika na hekaheka za barabarani.
Ndio maana Dsm ni Moja ya mikoa inayofelisha Sana hapa nchini.

Kama kila kata kuna shule ya serikali kwa nini Watoto wapande daladala kwa gharama za wafanyabiashara? Mbaya zaidi inakuwa lazima hapo ndipo dhulma ilipo.

Labda hiyo Sheria iwe ilitungwa zamani shule zikiwa chache lakini Kwa sasa haina Tija Sana
 
Ndugu yangu Lamomy nakuomba uje umchukue udugu wako cocastic yupo huku anabishana na vyombo vya dola watamsweka rumande😂😂
 
Kwanza nashukuru nimepata wasaa wa kujibizana nawee mama Vicky, maana kusemezana na waziri sio jambo dogo.

Afu ujue nn, mie nakukubali sana, tena mnoo, afu ni shabiki ako toka uko wizara ya Afya. Napenda pia unajipambanua wazi wazi ktk kutatua changamoto za wizara yako, hata za wizara nyingine ikiwa utahitajika uhusika wao.

Kongole kwako mama Vicky, bado nina jambo nawee kuhusu kundi maalumu fulani, nikitulia nitaleta hapa km uzi, na nita kutag ili uweze kutoa hata suluhisho na wengine wafaidike pia.

Uwe na siku njema!! 💖💖
 
Kwanini unaishi duniani? Ukijibu Hilo swali nitakupa jibu lako
 
Hujambo? Kadri jamii inavyoendelea kuniTag kuhusu hoja mbalimbali, nitaendelea ku reply kadri ya mipaka ya majukumu ya wizara hii na kuwaongoza kuhusu nini zaidi kifanyike iwapo wanahitaji maelezo zaidi. Ahsante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…