Madai ya tabia ya baadhi ya magari ya abiria kuzuia wanafunzi kupanda

Hujambo? Kadri jamii inavyoendelea kuniTag kuhusu hoja mbalimbali, nitaendelea ku reply kadri ya mipaka ya majukumu ya wizara hii na kuwaongoza kuhusu nini zaidi kifanyike iwapo wanahitaji maelezo zaidi. Ahsante sana.
Sijambo Dr,

Unafanya vizuri ila pia kama ulivyochukuwa wajibu wa kuwaeleza wananchi juu ya sheria mbalimbali pia ungechukua maoni yao kuyapeleka sehemu husika ili yakafanyiwe kazi kuliko kutaka mwananchi mmoja mmoja ayapeleke mwenyewe wakati wewe upo kuwawakilisha wananchi huko serikalini
 
Umenikumbusha aisee..!! Kwenye DCM unatanguliza bag unalirushia dirishani halafu nafata mwenyewe kupitia dirishani 😹😹😹
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Wala hasweki ndani na mtu yoyote ila unabaki unamtazama tu ligi ya maneno makombe yote abebe yeye maisha yaendelee mbele
Ila waziri hili suala la usafiri muwafikirie na wafanyabiashara, huwezi kupakia wanafunzi route ya Temeke-Tegeta kwa 200..!!

Ikitokea wamepakiwa wanafunzi 10 watapeleka hesabu gani kwa matajiri wao?
 
Huu uzi huu unasomwa moja kwa moja na LATRA. Ninachofanya mimi siku zote huwa ni kuwafungua macho jamii wajue mifumo na miundo na wajibu na majukumu ya vyombo mbalimbali Ili siku ingine wasiwe wanahangaika wanapokuwa na hoja kumtafuta gwajimad. Siku moja hatakuwepo na elimu itabaki kwao na itawasaidia. Uzoefu umenionesha kuwa, wengi hawajui miundo, mifumo, vyombo na taasisi na majukumu yao na hata wizara mbalimbali pia hawazijui, nani sasa atoke kuwapa elimu? Si kama hivi sasa tunapeana elimu 🤗
 
Kundi fulani lipi?
Coca ushaanza kutaka kutetea vidampa!! 😀
 
Mbona serikali haiamuru wanafunzi kula mgahawani Bure? Kwani watoto hawapati njaa shuleni
Kwanini serikali iwaonee daladala, serikali haijui hii ni biashara
Msimamo wangu: ili kuepuka usumbu wanafunzi walipe nauli kamili
Wanafunzi hawasafiri bure, bali wamepangiwa nauli kwa kuzingatia uwezo wao, na kuwa watu wazima wanavyolipa nauli inafidia msafirishaji asipate hasara. Hivyo sio sahihi kwa msafirishaji kukataa kubeba wanafunzi.
 
Umenikumbusha aisee..!! Kwenye DCM unatanguliza bag unalirushia dirishani halafu nafata mwenyewe kupitia dirishani 😹😹😹
Eheeeeee yaani nadhani we unaelewa nichozungumza maisha ni vita hao madogo wachangamke aisee🤣🤣
 
Sio kuwa hawana elimu bali mifumo ya serikali ndio mibovu hata ukitoa maoni sehemu husika kwa mwananchi wa kawaida hayafanyiwi kazi

Wenye mamlaka ndio mmeshikiria kila kitu na huu ndio uhalisia, wewe unadhani hao makonda hizo sheria zinazowakandamiza wao hawazioni? Je unadhani hawalalamiki? Je malalamiko yao yanafanyiwa kazi?

Ndio maana wanaona waiadabishe jamii kuliko kuendelea kulalamikia kitu ambacho hakifanyiwi kazi, kwao suluhisho ni kuwakataa wanafunzi wasipande kwenye vyombo ambavyo wamenunua kwa pesa zao

Hivyo Dr, tumia ufahamu wako kwa jamii ya kitanzania kutatua tatizo hili la watoto kupata shida na wala usitumie ufahamu wako wa sheria za kitanzania kutatua tatizo hili

Peleka haya maoni wizarani na bungeni au kwa Mh raisi itasaidia pakubwa humu wengi wametoa maoni mazuri sana
 
Wamezidi kudeka mno, hawajui maisha mapambano..!!
Yaani ni vizembeee....kuna familia nilienda mtoto kamaliza form 4 hajui kkoo,nilichoka sana.....sasa huyo ndio akapande daladala konda akimpiga biti moja analala stand....Wakati enzi zako shoga yangu ukitoka shule huyooo mara ukaogelee mto mzinga,mara siku nyingine uko Rongoni,mara ununio yaaani ni tafrani🤣🤣🤣🤣🤣
 
😹😹😹 umenichekesha mpk machozi yani nilikua na hekaheka jamani..!!
 
Wazazi pia inabidi wajiongeze,ukijifanya kuna sheria itamlinda mtoto hakika watakao umia ni watoto wetu....Hii nchi yenyewe inaeleweka hata ukilipeleka hilo gari LATRA bado na kesho utaliona linapiga route hapo ndio utajua hujui....Tulinde watoto wetu,waatengezenezee mazingira rafiki kwenye kusaka maarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…