Madai ya watu kuishi Hifadhi ya Ngorongoro na wanyama pori kuwa ni kuvutia utalii ni ujinga

Madai ya watu kuishi Hifadhi ya Ngorongoro na wanyama pori kuwa ni kuvutia utalii ni ujinga

Maswali muhimu kujiuliza.

1. Idadi ya watu na mifuko hifadhini inaongezeka au la?

2. Kuna idadi ya watu au mifugo ikifikiwa hifadhi itakuwa hatarini kuharibika au hata kutoweka?

3. Idadi hiyo ikifikiwa nini kifanyike?
Kwa nilivyomwlewa mimi amedai watoto wanakufa,kwa jinsi hiyo hakuna ongezeko la watu,labda mifugo.
 
Maswali muhimu kujiuliza.

1. Idadi ya watu na mifuko hifadhini inaongezeka au la?

2. Kuna idadi ya watu au mifugo ikifikiwa hifadhi itakuwa hatarini kuharibika au hata kutoweka?

3. Idadi hiyo ikifikiwa nini kifanyike?
Hao waandishi hopeless kabisa wanatoa tu idadi ya masai walioongezeka hawatoi idadi ya wanyama porii walioongezeka

Ukiangalia wanachosema utadhani wanyama pori hawaendelei kuzaliana tena wamesusa kuzaliana ngorongoro hadi masai waondoke ndio watazaliana kuongezeka

Ujengaji hoja wao hafifu sana na zero

Masai hali nyama pori ndio maana waliruhusiwa kuishi mbugani sio threat kwa wanyama pori kuwa watawaua hata wanyama pori wanawajua masai ni rahisi kukuta mtoto mdogo wa kimasai ngorongoro anachunga mbuzi au ndama katikati ya tembo na wanyama pori wengine kibao mtoto haogopi na wanyama pori hawamtishii maisha
 
Mkimaliza muende na kwa Wahadzabe mkawafurumushe
Muondoke hifadhini hili linapaswa kuwa lazima sio hiari ,zaidi ya 50% ya ardhi ya Tanzania haijatumika kuna sababu gani ya wamasai kuendelea kubaki hifadhini?
 
Tatizo kubwa la serikali ni la kutokufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Hali hii hupelekea tatizo la kisheria kutotatuliwa kwa muda mrefu, na hatimaye wananchi wanafikia kujiona wapo kisheria ijapokuwa kiuhalisia huwa wanavunja sheria.

Mifano ipo mingi sana, ambapo wananchi wanaendesha biashara ama kujijenga kimaisha hali serikali ikinyamazia uvunjaji na ukiukwaji wa sheria. Mathalani, tumeshuhudia ujenzi wa makazi katika maeneo hatarishi, yaliyotengwa kwa matumizi maalum, ama katika hifadhi za barabara, viongozi wa serikali na mamlaka wakiwa wapi kimya kama vile hawaoni kitu kinachoendelea.

Ujenzi ama shughuli za kibiashara, pale zinapoanza kuibuka, kunakuwa hakuna onyo ama katazo lolote linatolewa. Kibaya zaidi vibali vya huduma muhimu kama umeme, maji, elimu, simu n.k hutolewa hali ikifahamika vinakwenda kinyume kabisa na sheria.

Hili suala la Maasai kuvamia maeneo ya hifadhi ya Ngorongoro halijatokea kwa siku moja, ni jambo ambalo limepuuziwa na kuacha likikuwa mpaka limefikia kiwango hiki cha malumbano. Maasai waliachwa kwa makusudi wavunje sheria ili kuvitia zaidi biashara ya utalii.

Kuonekana kwao kama kabila duni lenye kuweza kuishi maisha "primitive" na wanyama hayawani wa mwituni ilionekana ni kichocheo cha kuwaacha wafanye shughuli zao za ufugaji katika hifadhi hii. Sasa ongezeko lao na ukubwa wa shughuli zao leo ndiyo vinaonekana kuwa hatarishi.

Ni lazima muafaka wenye kuzingatia masuala ya kiutu ufanyike. Ndiyo! Ukubwa wa tatizo sambamba na athari zake zimethibitika, lakini ukweli ni kwamba uvamizi huu haukutokea kwa siku moja. Ni lazima serikali iwaelimishe kwanza kabla ya kuanza matumizi ya nguvu ya kuwatoa hapo na kuwaamishia maeneo mengine ambayo hayajaandaliwa vyema kwa ajili ya maisha yao ya kifugaji.
 
Back
Top Bottom