Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Inatakiwa kwanza ujue Kati ya Mkopo na Deni.
Mkopo nikile unachopewa baada ya makubaliana maalumu mfano Riba na mkopeshaji.
Deni linakuja baada ya kushindwa kulipa mkopo hii ndio mbaya.
Mimi nadhani Deni ndio linaleta fedhea ila kuhusu mkopo sioni kama ni kitu kibaya kama unaweza kuutumia vizuri kuongeza wigo wa mambo yako ya msingi kama biashara
Kajaribu kukopa utajifunza kitu.
Hata wale wanaokopa na kuaibika mwanzoni huwa na mawazo mazuri kama yako ila ukikopa tu mzunguko wa hela unagoma
 
Afadhali ya taasisi kubwa/benki tambulika wanafuata miongozo na maadili.Kuna vile vikausha damu vinatuma mabaunsa wakung'unte mangumi wadaiwa.Kuna wadaiwa wameshawahi kupoteza maisha.
Eti wanakung'uta mangumi 😀
Na hii imepelekea microfinance zote ukienda kukopa lazima wakuulize umeajiriwa ukisema ndiyo ,raha yao useme wewe ni mwalimu ,mtendaji na wengineo wanyonge wa mama ila ukiwaambia mimi sijui askari gani ,sijui askari pori ,mara askari barabara ,au sijui askari mipaka umeshakosa hela maana wanajua hawawezi kuja kukudunda kienyeji kama kwa hao wanyonge wa bi mkubwa
 
Ulidhani nakuongopea wa wa kwetu ,huko ukikopa tayari umetangaza vita na uhakikishe unaweza kupambana haswa kupigwa viboko mbele ya mmeo na mkeo ni kawaida kwa madai ya umeleta jeuri
Mwili wangu unavyoumwa hata nikijikwaa aisee sitaki hata kufinywa

Hiyo mikopo hainifai
 
Eti wanakung'uta mangumi 😀
Na hii imepelekea microfinance zote ukienda kukopa lazima wakuulize umeajiriwa ukisema ndiyo ,raha yao useme wewe ni mwalimu ,mtendaji na wengineo wanyonge wa mama ila ukiwaambia mimi sijui askari gani ,sijui askari pori ,mara askari barabara ,au sijui askari mipaka umeshakosa hela maana wanajua hawawezi kuja kukudunda kienyeji kama kwa hao wanyonge wa bi mkubwa
Mara si punde;TANZIA!Nini?@moise kakoyongwa mangumi na mabaunsa wa kausha-blood hadi kakata moto kwa kushindwa kurejesha "alfu salasini na tisa"!😜😜😜😜
 
Mara si punde;TANZIA!Nini?@moise kakoyongwa mangumi na mabaunsa wa kausha-blood hadi kakata moto kwa kushindwa kurejesha "alfu salasini na tisa"!😜😜😜😜
Rafiki yangu mmoja ni ticha wa primary alikopa laki .ila mambo yakamwendea kombo ikabidi asubiri mshahara kuwalipa .
Kila wakienda kwake anawakimbia na kujificha ,siku wakaamua wamfuate shuleni alipowaona na kagari kao akaona cha kufia nini ?

Akaunga mbio kwa mkuu wake wa shule kuomba msaqda kabla heshima yake haijanyoloshwa ,kila nikimkumbusha anasema hawezi kurudia kukopa kabisa maana wale jamaa ni kama wamesomea kudai maana kuna muda walikuwa wanamuiwinda mpaka bar tunafanya kumficha
 
Back
Top Bottom