Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Madeni: Je, umewahi kudaiwa mpaka ukajuta kwanini ulikopa?

Hapa penyewe kuna hela ya mkopo naisikilizia!
a3dda7ff99625034d78f0a1dda1c0ba9.jpg
 
Watanzania sio walipa madeni. Mtu anadaiwa halipi kwa muda kama makubaliano yanavyotaka, mwisho wa siku ndio kauli hizi kuna watu wanadai vibaya na wengine utasikia hela yenyewe laki tu unanisumbua utafikiri nini! Sio kwa watu binafsi sio kwa taasisi za fedha kote huko kuna madeni sugu yasiyolipwa na wadaiwa utawakuta mitaani wakijisifu kutokulipa taasisi au watu fulani. Ndio maana riba za mabenki ziko juu na hatuna finance system ya kueleweka kusaidia watu kwenye maendeleo.
Mkuu ni changamoto sana
 
😅😅 ujasiri kama huo unapata wapi
😂Kuna mda uta zoea tu baada ya kuamua liwalo na liwe maana mambo hayaendi na ela ya kulipa hauna kweli

na ukifika iyo stage amna comeback unakua legend yani adi utashangaa uogopi polisi wala mahakama😂😂

kwanza unajua kabisa madeni haya daiwi na polisi kwaiyo hata akija naona kama ana poteza mda
 
Watanzania sio walipa madeni. Mtu anadaiwa halipi kwa muda kama makubaliano yanavyotaka, mwisho wa siku ndio kauli hizi kuna watu wanadai vibaya na wengine utasikia hela yenyewe laki tu unanisumbua utafikiri nini! Sio kwa watu binafsi sio kwa taasisi za fedha kote huko kuna madeni sugu yasiyolipwa na wadaiwa utawakuta mitaani wakijisifu kutokulipa taasisi au watu fulani. Ndio maana riba za mabenki ziko juu na hatuna finance system ya kueleweka kusaidia watu kwenye maendeleo.
Yeah kiukweli nilimcheleweshea nilipitisha siku kama nne hivi za makubaliano ila chamoto nilikiona🙌🙌
 
😂Kuna mda uta zoea tu baada ya kuamua liwalo na liwe maana mambo hayaendi na ela ya kulipa hauna kweli

na ukifika iyo stage amna comeback unakua legend yani adi utashangaa uogopi polisi wala mahakama😂😂

kwanza unajua kabisa madeni haya daiwi na polisi kwaiyo hata akija naona kama ana poteza mda
We nomaa aisee😅
Mimi najijua siwezi kabisa
 
Shida siyo kudaiwa tu, shida ni unadaiwa na nani?

Mimi roho yangu ni ndogo sana Hata nikidaiwa 50,000 tu siwezi kulala usingizi mpaka nilipe
Nakosa amani kabisa

Twende kwenye mada

Madeni yanaweza kumharibu na kumuathiri mdaiwa kwa kiwango kikubwa kuliko tunavyofikiria, hasa pale anapogundua uwezo wake wa kulipa umekuwa mdogo

Hali inakuwa mbaya zaidi kama anaanza kupokea presha kutoka kwa anayemdai

Yaani kuna watu wanadai vibaya 🤣

Baadhi ya madhara ambayo mdaiwa anaweza kuyapata ni:

Kukosa utulivu
Kila akikumbuka ana deni, mood inabadilika

Kutumia muda mwingi kuwaza namna ya kulipa deni, mpaka anapata msongo wa mawazo na kushindwa kuzingatia mambo mengine

Kuwa na hasira za hapa na pale bila sababu

Kukosa hamu ya tendo la ndoa, au hata mkiwa katikati ya tendo, mood inakata... babu analala yoo! 🤣 Kwa mwanamke pia inaweza kusababisha ukavu

Kuogopa kupokea simu, hasa namba usizozijua

Mwisho wa siku unaweza ukaacha kupokea simu muhimu yenye dili zuri kwa sababu ya hofu

Kukosa uhuru wa kutembea kwa kuogopa kukutana na anayekudai

Na mara nyingi mtu akiwa na deni huwa mnyonge sana

Halafu kuna watu wanajua kudai vibaya sana! 🤣

Kwa hiyo, kama huna ulazima mkubwa, usikope pesa za watu

Na ukilazimika kukopa, basi iwe ni kwa jambo la msingi na ukiwa huna njia nyingine

Je, wewe umewahi kukopa pesa za watu zikataka kukutokea puani?

Ukakosa amani na kujuta?

Baada ya hapo uliendelea kukopa, au ulikula kiapo kwamba hurudii tena?

Ongezea pia ni madhara gani mengine ya kihisia anayoweza kuyapata mdaiwa hasa pale anapogundua kua hana uwezo wa kulipa kwa wakati huo

ShesRise_1 ✋️
Pesa nayodaiwa kwa kukadiria ni kama milioni ishirini na nane madeni yana miaka kama kumi na saba hivi ila InshaAllah nitawalipa wanaonidai.
 
Back
Top Bottom