Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Dakika kumi huwezi kula hotel na watoto zaidi ya kuachwa na basi beba chakula kupunguza gharama
 
β€’ kwa nini tuishi kwa biscuit na juice, mamlaka zinakazi gani,?
β€’ Hapa tunazungumzia Abiria kuwa huru wakati wa safari, mbona tren inahuduma zuri angalau, na inasimama kwenye vituo vya kawaida kabisa.
Shida ni kutaka kila kitu serikali itatue. Biashara huria, ukiona basi linakupeleka sehemu ya ghali, badilisha basi; ikishindikana badilisha usafiri; ikishindikana badilisha utaratibu wa ulaji.
 
Kabisa msosi bure, kulala bure ..ukija na muchepuko huulizwi chochoteπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
😁😁 Nyie Madereva mnazingua sana, mnawatesa watoto wa kimaskini, njia zima wanashindia maji au juice
 
Njiani sio sehemu za kula kula,kale kwako.
Kwani ukiwa safarini, na ukiwa kwako njaa huwa zinauma tofauti?

Iambie serikali ndio ijenge hizo sehemu za kula watu masikini inawezekana kama inaweza Jenga stend haishindwi.
Siyo kwamba serikali ijenge hotels za maskini, kwani utaratibu wa zamani ilikuwaje, au mwenzetu ndo umezaliwa 2022?


Hizo hotel wamewekeza pesa nyingi na kila dereva na makonda wanakula Bure.
Huu ndo ujinga wa mtu Mweusi sasa, mjengo amejenga vizuri, lakini vyakula anauza vibichi, vimechacha,
 
Zamani sio sasa,Sasa ni ushindani,
Kama pesa haitoshi unafunga masaa TU kama kubeba hotpot mzigo
 
Vyakula vingi vya njiani ni sub standard huwa nashangaa watu kula hovyo njiani utadhani wanasafiri kufanya utalii WA kula,kale kwenu
 
Shida ni kutaka kila kitu serikali itatue. Biashara huria, ukiona basi linakupeleka sehemu ya ghali, badilisha basi; ikishindikana badilisha usafiri; ikishindikana badilisha utaratibu wa ulaji.
ukiona basi linakupeleka sehemu ya ghali, badilisha basi
Utabadilishaje gari, wakati magari yote yaendayo Mikoani inafanya huo upuuzi!

ikishindikana badilisha usafiri;
Usafiri upi, Ndege? Kama chakula tu shida hizo garama za choppa anatoa wapi?
 
Tafuta tuu hiyo afu nane, watu wameshalamika sana, ila ukumbuke cheap is expensive... Utauziwa afu tatu kilomita mbili nyingi tumbo linaanza kuvuruga
Hata hivyo vya bei matumbo yanavuruga kama kawaida. Silagi njiani labda nitakapo kuwa na familia hasa watoto wa kike wakiume nitakomaa nao.
 
Usichojua ni kwamba dereva sio kwamba anapaki kwa bahati mbaya, hapana kuna vigezo na masharti umpelekea kupaki kwenye hotel hiyo, sharti la kwanza mwenye hotel lazima atoe hela kwa dereva nadhani ni sh 10,000 au 20,000 pili sahani moja bure ya dereva, tatu toileti ziko sawa, nne anauwezo wa kuhudumia watu 50+ kwa muda mchache yaani dk 15? , tano parking.Uzuri na bei ya chakula sidhani kama wanazingatia, vigezo ni hivyo hapo.
 
Vyakula vingi vya njiani ni sub standard huwa nashangaa watu kula hovyo njiani utadhani wanasafiri kufanya utalii WA kula,kale kwenu
Ndo maana nasema, Vyakula vipo chini ya kiwango, lakini bei inakuwa siyo rafiki kabisa,.

nashangaa watu kula hovyo njiani utadhani wanasafiri kufanya utalii WA kula
Kula ovyo ovyo kiaje, kwa hiyo mkuu unaweza safiri masaa 14 bila kula chochote?
 
Mimi nachangia tu kuwa
Zile hoteli wanazopaki ni safi, na huduma nyingine za kijamii ni nzuri (Usafi umeboreshwa)
Pendekezo; Badala ya kuweka bufee pekee yake, waweke pia vyakula vya watu wa kawaida
mfano: Wali maharage au wali mboga mboga, (maandazi/Chapati/chai) Chips kavu za buku au pengine
viazi vya kukaanga vya buku nk nk
 
Hotel za ajabu ajabu na mpya ndio ambazo zina maslahi mazuri kwa dereva na konda. Nyie mkienda kupigwa jua dereva yeye anakunja 20K yake na anakula sahani moja bure
 
β€’ Chazo cha maisha magumu kipo hapa ✍️.
β€’ uchaguzi ukifika huwa tunasahau kabisa shida zote, tunabaki kuhongwa kofia tu.
Usichokikumbuka ni kuwa kipindi cha uchaguzi hela inamwagwa kwa maskini huko kuwapumbaza pamoja na hizo kofia na tsheti.
 
Kweli, hapa itapendeza zaidi,
 
Asante 🀝
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…