Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Dakika 10, kwa ajili ya kula ni ndogo sana, Abiria wanapelekeshwa utadhani, tunaenda kuwahi vitu vya maana tunakoenda.
Sahihi kabisa!! Halafu jiulize bus lenyewe wanalipatia huduma gani?

Hapa mamlaka inapaswa iwashinikize ukaguzi wa gari pale abiria wanashuka kwa ajili ya mahitaji , who nao wafanye ukaguzi wa CHOMBO.
1 - TYRES
2- BRAKES
 
Sahihi kabisa!! Halafu jiulize bus lenyewe wanalipatia huduma gani?

Hapa mamlaka inapaswa iwashinikize ukaguzi wa gari pale abiria wanashuka kwa ajili ya mahitaji , who nao wafanye ukaguzi wa CHOMBO.
1 - TYRES
2- BRAKES
Kabisa mkuu, lakini hayo hawafanyi kabisa, wakitoka wametoka.
 
Binafsi sioni gharama kama kuna huduma nzuri, ishu ni dereva kupaki gari sehemu ambayo huduma ni mbovu, hii huwa inanikwaza sana kmmk. Mfano kuna upumbavu upo pale Mdaula kwa mbele kama unatokea DSM au Ubena kwa mbele kama unatokea Moro, ule mgahawa pale ni takataka ***** zao. Huwa napenda sana dereva akipeleka basi bale Msolwa, kwanza panavutia kabla hata hujanunua chochote na kamwe huwezi kulalamikia bei pale.
 
Mimi ishu kubwa kwangu sio madereva kusimama sehemu ambazo vyakula ni bei juu ila ishu kubwa ni kwamba ni kwanini sehemu nyingine chakula kiuzwe sahani TZS 2000/= na sehemu nyingine kiuzwe TZS 5000/=?.
Mfano sehemu hiyo yenye kituo Cha bus Mchele ni TZS 1,500/= kwa 1KG lakini ukitoka pembeni kidogo na kituo wali sahani utanunua TZS 2,000/= ila ukiwa kwenye kituo Cha bus kwenye eneo hilo hilo utanunua wali TZS 5,000/=. Kwahyo serikali itoe muungozo juu ya Hilo ili kupunguza unyonyaji.

Mfano mwingine: sehemu nyingine Soda 300mls inauzwa TZS 600/= na sehemu nyingine Soda hiyo hiyo inauzwa TZS 1,000/=.
Kwasababu hata kama mtu ameamua kufanya biashara angani au majini haimaanishi kwamba anakuwa na haki ya unyonyaji.

Kwahyo serikali itoe miongozo kuhusu hilo.
 
usilolijua ni sawa na usiku wa giza hizo sehemu wao madereva hupewa ofa ya kula bure...
 

Binafsi sioni gharama kama kuna huduma nzuri, ishu ni dereva kupaki gari sehemu ambayo huduma ni mbovu, hii huwa inanikwaza sana
Kinacho umiza zaidi huduma zinakuwa za hovyo, alafu chakula Chao ni garama, ni kero sana aise,
 
Asante sana mkuu kwa hoja zuri, Ukiona hivyo wanafanya makusudi, kwamba hawa Abiria lazima watanunua tu, na kutokana ikiwa dereva analipwa posho na wali sahani kadhaa, basi atahakikisha anawaburuza abiria mpaka sehemu anayo lipwa posho.
 
usilolijua ni sawa na usiku wa giza hizo sehemu wao madereva hupewa ofa ya kula bure...
• Ndo tupo hapa, tunajadili haya masuala ya Giza,

• Dereva hata akisimama sehemu, na abiria wakanunua chakula , Dereva kupewa hela atapewa tu.
 
Apo dawa ni kusafiri na msosi tu kwenye hotpot wao wakishuka kwenda kula wewe unafungua hotpot lako unajisevia.
 
Apo dawa ni kusafiri na msosi tu kwenye hotpot wao wakishuka kwenda kula wewe unafungua hotpot lako unajisevia.
Mkuu, upo sahihi, Siyo kila mtu unaweza beba hotpot, wengine wanasafiri kwa mda mrefu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…