Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sahihi kabisa!! Halafu jiulize bus lenyewe wanalipatia huduma gani?Dakika 10, kwa ajili ya kula ni ndogo sana, Abiria wanapelekeshwa utadhani, tunaenda kuwahi vitu vya maana tunakoenda.
Ni kweli kaka lkn huduma kwa mwanadamu 10 min ni ndogo na ukaguzi wa gari brakes na matairi ni muhimu sana.Mkuu zamani mnakaa saa nzima maana na dereva kachoka kufukia mashimo anapumzika.
Siku hizi ni mbio tu
Kabisa mkuu, lakini hayo hawafanyi kabisa, wakitoka wametoka.Sahihi kabisa!! Halafu jiulize bus lenyewe wanalipatia huduma gani?
Hapa mamlaka inapaswa iwashinikize ukaguzi wa gari pale abiria wanashuka kwa ajili ya mahitaji , who nao wafanye ukaguzi wa CHOMBO.
1 - TYRES
2- BRAKES
Mimi ishu kubwa kwangu sio madereva kusimama sehemu ambazo vyakula ni bei juu ila ishu kubwa ni kwamba ni kwanini sehemu nyingine chakula kiuzwe sahani TZS 2000/= na sehemu nyingine kiuzwe TZS 5000/=?.Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.
• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma
Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.
Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.
1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?
2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini
Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
usilolijua ni sawa na usiku wa giza hizo sehemu wao madereva hupewa ofa ya kula bure...Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.
• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma
Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.
Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.
1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?
2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini
Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
Binafsi sioni gharama kama kuna huduma nzuri, ishu ni dereva kupaki gari sehemu ambayo huduma ni mbovu, hii huwa inanikwaza sana kmmk. Mfano kuna upumbavu upo pale Mdaula kwa mbele kama unatokea DSM au Ubena kwa mbele kama unatokea Moro, ule mgahawa pale ni takataka ***** zao. Huwa napenda sana dereva akipeleka basi bale Msolwa, kwanza panavutia kabla hata hujanunua chochote na kamwe huwezi kulalamikia bei pale.
Kinacho umiza zaidi huduma zinakuwa za hovyo, alafu chakula Chao ni garama, ni kero sana aise,Binafsi sioni gharama kama kuna huduma nzuri, ishu ni dereva kupaki gari sehemu ambayo huduma ni mbovu, hii huwa inanikwaza sana
Asante sana mkuu kwa hoja zuri, Ukiona hivyo wanafanya makusudi, kwamba hawa Abiria lazima watanunua tu, na kutokana ikiwa dereva analipwa posho na wali sahani kadhaa, basi atahakikisha anawaburuza abiria mpaka sehemu anayo lipwa posho.Mimi ishu kubwa kwangu sio madereva kusimama sehemu ambazo vyakula ni bei juu ila ishu kubwa ni kwamba ni kwanini sehemu nyingine chakula kiuzwe sahani TZS 2000/= na sehemu nyingine kiuzwe TZS 5000/=?.
Mfano sehemu hiyo yenye kituo Cha bus Mchele ni TZS 1,500/= kwa 1KG lakini ukitoka pembeni kidogo na kituo wali sahani utanunua TZS 2,000/= ila ukiwa kwenye kituo Cha bus kwenye eneo hilo hilo utanunua wali TZS 5,000/=. Kwahyo serikali itoe muungozo juu ya Hilo ili kupunguza unyonyaji.
Mfano mwingine: sehemu nyingine Soda 300mls inauzwa TZS 600/= na sehemu nyingine Soda hiyo hiyo inauzwa TZS 1,000/=.
Kwasababu hata kama mtu ameamua kufanya biashara angani au majini haimaanishi kwamba anakuwa na haki ya unyonyaji.
Kwahyo serikali itoe miongozo kuhusu hilo.
• Ndo tupo hapa, tunajadili haya masuala ya Giza,usilolijua ni sawa na usiku wa giza hizo sehemu wao madereva hupewa ofa ya kula bure...
Kinacho umiza zaidi huduma zinakuwa za hovyo, alafu chakula Chao ni garama, ni kero sana aise,