Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

Nilipokuwa natumia subaru kuna jamaa yangu alinishutumu kuwa sijui kuitumia, sikumjibu kitu. Niliwaza tu kwa barabara zipi!! na nikajua yeye hajawai hata kupiga honi ya subaru maana kwa uchumi tuliokuwa nao kipindi kile angekuwa hata na idea ya wese la subaru ukiiletea sifa...

Kwa hiyo hata hawa wanaotusumbua mijini wengi wao ndio uwezo wao wa wese huo, ukimpeleka highway haendeshi hata 100km na kurudi
Na ndio maana nawaambia waache ujinga.
 
Subaru mlio wake unanyegesha hata kama ungekuwa na vitz ukapewa subaru siku hiyo unakuwa chizi Altezza tu watu wanachizika sasa Subaru Impreza si ndo shida STI acha kabisa
 
Muundo wa injini ya magari haya nitofauti na magari mengine kwa hiyo inazifanya ziwe zinatoa sauti ambayo mtu kama sio makini inakupa hamasa ya kuikamua zaidi.
Ha ha ha; hamasa ya kukamua zaidi kama pikipiki (bodaboda) vile.
 
RRONDO sio bongo tu hata huku nilipo mambo ni yale yale tatizo la hizi gari zina mzuka mbaya sana hasa kwenye wepesi wa spidi (take over) ulaini wa steering na brake za kunasa

Kwanza tusitibu jipu kwa kulitumbua tu ni lazima tujue kiini cha jipu husika...mimi nadhani tukitaka kujadili Subaru tuwajadili kwanza wavumbuzi wake! Sijui walilelewaje hawa jamaa maana kwanza gari yenyewe ina sauti kuuuubwa kuzidi hata umbo lake achilia mbali fujo zake bara barani! Mwenye CV ya kijana mgunduzi wa Subaru ailete hapa tumpigie kura ya kutokuwa na imani naye!
 
Kwanza tuzitibu jipu kwa kulitumbua tu ni lazima tujue kiini cha jipu husika...mimi nadhani tukitaka kujadili Subaru tuwajadili kwanza wavumbuzi wake! Sijui walilelewaje hawa jamaa maana kwanza gari yenyewe ina sauti kuuuubwa kuzidi hata umbo lake achilia mbali fujo zake bara barani! Mwenye CV ya kijana mgunduzi wa Subaru ailete hapa tumpigie kura ya kutokuwa na imani naye!
Hahhahahaaaa mvumbuzi hana kosa ni sawa na kumlaumu mvumbuzi wa munde kwa mlevi aliyejikojolea bar
 
Hahhahahaaaa mvumbuzi hana kosa ni sawa na kumlaumu mvumbuzi wa munde kwa mlevi aliyejikojolea bar

Ndugu yangu mshana jr japo undugu wetu hauna fungamano na masuala yetu yaleeee ya mazombie ila kuna kitu ambacho naona sisi wapenda mbio tunaonewa....inawezekanaje gari Speedometer inatakiwa 210KM/H upigwe tochi kwa kutembea 54km/h? Kwanini wasizuie magari bandarini wangoe huo mwendokasi waweke wao wa 50km/h ili tupunguze kushikana mashati na hizo tochi wakapimie mwendokasi wa mawimbi baharini?
 
Ndugu yangu mshana jr japo undugu wetu hauna fungamano na masuala yetu yaleeee ya mazombie ila kuna kitu ambacho naona sisi wapenda mbio tunaonewa....inawezekanaje gari Speedometer inatakiwa 210KM/H upigwe tochi kwa kutembea 54km/h? Kwanini wasizuie magari bandarini wangoe huo mwendokasi waweke wao wa 50km/h ili tupunguze kushikana mashati na hizo tochi wakapimie mwendokasi wa mawimbi baharini?
Wewe utabaki kuwa ndugu yangu siku moja barabara ya bagamoyo msata ukishapita kiwangwa nikakutana na tochi ya kimagumashi
Uzuri jamaa alikuwa Mwelewa sana akasema hizi sheria zimepitwa na wakati ni sheria za wakati wa mchonga na maland rover yake mpaka leo hii hazijawa uptodated
Gari niliyo kuwa nayo ni speed 240 na hapo nilikuwa naenda 80 BTW speed zinataka hekima na ufahamu ni wakati gani na mahali gani pa kwenda spidi gani
 
Back
Top Bottom