Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Mkuu muwe mnatumia akili . hivi inaingia skilini unawanyima misada wananchi wako wakati wa maafa afu siku nyingine unasaidia Msumbiji, Zimbabwe kwenye maafa mengine ?
Magufuli ni mtu mmoja ambaye katika saikolojia yake inawezekana kavurugwa huko nyuma.

Inakuwa kama kapigwapigwa alivyokuwa mdogo, hakupata mapenzi ya familia, sasa anaona kakimua kapata cheo, na yeye zamu yake kupiga watu.

Ndiyo maana kauli zake ni za kupigapiga, kusengenyasengenya, za ujingaujinga tu.

Mara atapiga wapinzani mpaka shangazi, mara anaita watu walioshindwa kufauku katuka nchi ambayo haina mifumo vilaza, mara anakaripia watendaji kuhusu lift kinyume na sera za serikali yake mwenyewe.

Ni mtu wa ovyo sana. Kapewa urais!

Hizi si za staha za kirais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndio ukweli, nani alikutuma ujenge mabondeni? Unaenda bonds la mto msimbazi mtu kajenga ukingoni kabisa mwa mto, anatumia milioni kadhaa huku akiona kabisa hapafai kukaa nyumba pale.

Haya maisha ukibembelezwa sana unakuwa mjinga.
 
Kuna watu hawana hata mawasiliano na serikali huko.

Ndiyo maana, nasisitiza mifumo kwanza kabla ya lawama.
Ushahidi unao, wa watu kutokuwa na mawasiliano, kunyimwa yote hayo uliyoorodhesha?
 
Kuna vitu vinachekesha sana nimejaribu kufikiria hadi enzi za historia yetu kama nchi
 
Huo ndio ukweli, nani alikutuma ujenge mabondeni? Unaenda bonds la mto msimbazi mtu kajenga ukingoni kabisa mwa mto, anatumia milioni kadhaa huku akiona kabisa hapafai kukaa nyumba pale.

Haya maisha ukibembelezwa sana unakuwa mjinga.

..hata milimani kunaweza kutokea MUDSLIDE / MAPOROMOKO YA UDONGO.

..ukweli ni kwamba Jpm ana roho ya KIKATILI. hata walioathirika na tetemeko la ardhi badala ya kuwafariji aliwatolea lugha za MATUSI.

..suala la mafuriko lina sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni serikali kutokuweka MIUNDOMBINU ya kupitisha maji [ ya mvua na maji machafu ]. Sehemu ya pili ni wananchi waliojenga kimakosa mabondeni.

..
 
When it comes to people's life the stakes are too high to make it a political agenda.
There are hundred safe ways to prevent any political leader from being re-elected for a second term.

If you live in dangerous areas that are prone to floods, it is you who is going to lose big, you either lose your beloved ones or you lose your life. And there is no 100% guarantee the politician you hate the most won't be re-elected after your loss.

Ukikaa mabondeni anaekufa sio Mugufuli bali wewe na ndugu zako, maeneo yaliyo juu ni mengi sana kuliko mabondeni.
Kwani umefungwa na nati au umechomelewa na umeme hapo mabondeni kiasi cha kushindwa kwenda kuanzisha makazi maeneo mengine?
 
Sasa nimekuelewa,we are on two different pages though we are reading same book
 


Sio tu kufariji, ila hata kusema ukweli. Anachosema Rais ni kwamba hata iweje, mtu kwanza kupata hasara ya mafuriko ni yule atakuwa amejenga kwenye mkondo wa maji.
 

Ni kweli kabisa, maana hata Madaraja yaliyotengenezwa na serikali kwa fedha za walipa kodi, yalipobomolewa na mafuriko, serikali haikuchukua hatua maana hayo madaraja yalifuata maporomoko.
Pia kingo za mito zilipobomolewa na maji, na yale maji yakaelekea kwenye makazi ya watu, hizo kingo ndo zilifuata hayo maji.

NB:
Kauli kama hizi ndizo wanaccm wanazipenda na kuzipigia makofi bila kujua aliyezitoa hana muda nao na anawaona kama mizigo kwa serikali. Tujifunze na tuchukue hatua.
 
Kwanini hayajatokea dodoma ambako hakuna misitu kabisa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushahidi unao, wa watu kutokuwa na mawasiliano, kunyimwa yote hayo uliyoorodhesha?
Ushahidi gani unataka, unajua kipato cha wastani tu cha Mtanzania, GDP per capita, ni ushahidi tosha?

Hakiwezi kupanga bajeti ya mtu anayetakiwa kuishi kwa viwango vya utu wa dunia ya leo.

Yani GDP per capita ya Mtanzania haitoshi hata kununua bando ya internet kwa mwaka.

That is if huko mabondeni kuna mawasiliano ya kumuasa kuwa mvua zinakuja ondokeni mabondeni.

Sasa hapo mtu atafanyaje mawasiliano kiasi cha wewe umlaumu kwamba hajafanya mawasiliano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…