Madogo wa Kiume, Acheni Tabia ya Kuja Inbox Kuomba Hela

Madogo wa Kiume, Acheni Tabia ya Kuja Inbox Kuomba Hela

Namba Ile Ile 😎
ndiyo mkuu, na nishafika eneo la tukio tayari, unasubiriwa wewe tu tajiri..!🫠
IMG_6642.jpeg
 
Jamani madogo hasa new members acheni hii tabia ya kuingia inbox za watu kuanza na Bro naomba hela ya kula.Ukienda inbox za watu 100 ukitegemea mmoja atakutumia pesa hiyo siyo sawa.

Pesa hutafutwa, siyo kuombwa ovyo. Kama kweli umekwama siku hiyo na una njaa anza kutafuta msaada mtaani kwenu hukohuko kwa majirani. Hata migahawani kuna uwezekano ukapata msaada wa chakula kuliko kutuma copy-paste kwa members

Bora hata uombe fursa, kazi au connection kuliko kuomba hela moja kwa moja. wanadhani kila mtu wa JF ni tajiri. Ukweli ni kwamba sisi ni akina nyie tu tupo hapa kutafuta madini, maarifa na habari.

Yaani ndani ya wiki moja nakuta meseji tatu tofauti zote zinaanza na Bro sikujui hunijui ila nina shida, nisaidie hela ya kula.
Sawa wanakosea lakin hata wew umekosea na sio kila mtu anauwezo wa kukabiliana na matatizo yake mwenyew yeye kakuomba msaada akiwa na iman utamsaidia wew unakuja hum kutangaz na unasema akaombe msaada mtaani kwao je kam ameanzia hjko mtaan na wameshindwa kumsaidia wew kam ulikua hauna uwezo ama hutak kumsaidia ungemwambia na si kuja kutuambia sis wanajamvi
 
toka mwaka jana October nilipokata mguu JF, juzi tu nimerud, nimetumiwa pm ya kuombwa hela. Sasa mpaka najiuliza hivi hawa watu wanatumia njia gani kufanya vetting kwamba huyo nimuombe hela? Nikajiuliza au ji wadau ambao wanakufahamu ila wanakuja na id mpya?
 
Mtu kakufata inbox na wewe unakuja kumuanika hapa mkuu instead umalizane nae huko huko. Nini maana ya inbox? Kumwambia huna unashindwa nini ndugu yangu na umwambie huko huko mambo yaishe. Na afu mtu kuomba mwingne pesa kwani ni dhambi bro. Au hauna na yeye anakuvuruga bure.
Mm mwenyew nimeshangaa anakua na tabia za jinsia KE
 
Back
Top Bottom