Madudu yaliyoibuliwa bandarini na Rais Samia mbona hayasemwi?

🤣🤣acha kutetea ujinga🙏mwambie there's always a second chance in life,Mungu amempatia baraka hii,asiichezee,aitumie vizuri,btw hakuna uzee katika kusoma,arudi darasani,nafasi yavkuajiri private tutor international anayo,aitumie vyema,anahitaji mtaalamu wablugha na international relations,"muzungu"kufikia Hilo🙏akifanya Hilo she will be untouchable 🙏bado tunampenda na ana nafasi ya kufanya marekebisho hayo madogo🙏
 
Swwali zuri sana, hayo ndiyo yakuwauliza waliopewa amri ya kuchukuwa hatua.

Hii vita siyo ndogo lama mnavyodhania.
Kama alitoa amri haikuyekelezwa, tuwaulize waliopewa amri au aliyetoa amri kafanya nini baada ya kupuuzwa?
Au alivyoona kapuuzwa ndo akachukua hatua ya kuwaleta Waarabu kama comeback?
 
Mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka bandari yetu tu. Yani mnauza wavaa vijola.
Asante
 
Wewe una haki ya kufikiri upendacho. Lakini ukweli ni huo. Tena hayo ni machache sana.

Jiulize, kwanini mwaka huu tumeweza kuipiku bandari ya Mombasa kwa wingi wa mizigo kuliko miaka yote ya nyuma?

Nini kilikuwa kinafanyika?
Pumbavu zao "stupid"

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Miezi michache baada ya kuapishwa Urais. Rais Samia Suluhu Hassan alivunja bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Meli kwa kuwaondoa wenyeviti wake baada ya kutoridhishwa na utendaji wao.

Rais Samia alitangaza uamuzi huo Jumamosi Desemba 4, 2021 wakati wa uzinduzi wa gati namba 0 hadi 7 katika bandari ya Dar es Salaam.

Kabla ya tangazo hilo, Rais Samia alieleza baadhi ya mapungufu yanayoikabili mamlaka hiyo, baadhi yake yakiwa katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akihoji kwa nini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi sasa.

Bodi ya TPA inaundwa na mwenyekiti wake Prof Ignas Rubaratuka na naibu wake ni Dk Delphine Magere. Wajumbe hao ni Malata Pascal, Dk Jabiri Bakari, Masanja Kadogosa, Jayne Nyimbo, Mhandisi Ephrem Kirenga na Eric Hamissi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Bandari.

Aidha, ameitaka PCCB kuchunguza bodi hizo kwa kile kinachoendelea bandarini na kuwachukulia hatua waliohusika na upotevu wa fedha uliotajwa katika ripoti hiyo.

"Mkurugenzi, PCCB nakuagiza uchukue hatua dhidi ya watu hawa haraka iwezekanavyo na kama hakuna taarifa nitakupa maelezo ya kilichotokea hapa," alisema Rais Samia.

Alisema mifumo ya malipo bandarini kwa muda mrefu imekuwa ikiendeshwa na watumishi jambo ambalo linaonesha kuwa mizigo imekuwa ikilipiwa langoni lakini kwa maana halisi si kweli inasababisha upotevu wa mapato kwa nchi.

Alitoa wito kwa shirika la kupambana na rushwa kuja na majibu ya kwa nini yote haya yanatokea bado bodi na wafanyakazi waliohusika bado wako ofisini.

Pia aligusia juu ya idhini ya zabuni bandia na Shirika la Usafirishaji, huku akijua kuwa vigezo sahihi havikufuatwa na bodi ilihusika katika idhini na serikali ilikuja tu kujua baada ya kutuma watu nchini Uturuki kuchunguza kampuni hiyo.

Alimtaka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuchukua hatua za haraka na endapo atashindwa, anapaswa kumjulisha ili kuchukua hatua zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kumteua waziri mpya.

Chanzo: Tanzania: President Samia Dissolves Tanzania Ports Authority, Shipping Corporation Boards
Mama aligundua Biswalo Maganga ametuibia 27 billion na kwenda kuzificha China. Amemchukulia atua gani?
 
Yakiwekwa wazi yatawaumbua wenyewe.

Nchi hii ni ya ajabu Sana mtu ambaye anasimama Jukwaani na kuhamasisha ulipaji Kodi ndiyo anakuwa wa kwanza kukwepa Kodi.

Vigogo wa Chama na Serikali ndiyo wanao ongoza kuua Bandari yetu kwa kupitisha Makontena bila kulipa Kodi.
Ni kweli kabisa hapa ungeongeza na wafanya biashara maarufu baadhi na hata sheria nyingi zinavunjwa na na hao hao huku mitaani, kwenye hili ni ukweli 100% wala ushingae kuona gari ya Judge inapita mwendokasi lakini yeye ndio anasimamia sheria za nchi. Ni wakati tukabadlika sheria ziheshimiwe ndio maana hili la bandari kunaweza kuwa na mapungufu lakini ukweli linawaumiza wengi sana wapinzania, CCM na wafanya biashara kuna watu walishawazoea sana mfumo wanapiga tu simu mambo yao yanaenda sasa mabadiliko watu watapoteza mamilioni hili lipo tukiacha na mengine mapungufu ya kimkataba lakini wizi bandarini wa mazoea watu wana connection sio mchezo, hili wanaliogopa sana na Tz huwa tunatabia kuogopa changes, hatupendi.
 
We jamaa unateseka sana aisee,unahangaika sana.naona jahazi linazama ila tu unajaribu kupiga mbizi japo huna utaalamu wa kuogelea,DPW wakianza kazi sijui utabadili hiki ki ID chako!

Una acha kujadili mada unarukia vitu vingine kabisa,upigaji Bandarini utakua historia.
Kwenye kipengele gani cha mkataba wa DPW kwamba upigaji utakuwa historia

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Wewe una haki ya kufikiri upendacho. Lakini ukweli ni huo. Tena hayo ni machache sana.

Jiulize, kwanini mwaka huu tumeweza kuipiku bandari ya Mombasa kwa wingi wa mizigo kuliko miaka yote ya nyuma?

Nini kilikuwa kinafanyika?
Inakuwaje rais amesema sisi bandari hatuwezi kuiendesha? Kama mpaka mombasa tumewapiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miezi michache baada ya kuapishwa Urais. Rais Samia Suluhu Hassan alivunja bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Meli kwa kuwaondoa wenyeviti wake baada ya kutoridhishwa na utendaji wao.

Rais Samia alitangaza uamuzi huo Jumamosi Desemba 4, 2021 wakati wa uzinduzi wa gati namba 0 hadi 7 katika bandari ya Dar es Salaam.

Kabla ya tangazo hilo, Rais Samia alieleza baadhi ya mapungufu yanayoikabili mamlaka hiyo, baadhi yake yakiwa katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akihoji kwa nini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi sasa.

Bodi ya TPA inaundwa na mwenyekiti wake Prof Ignas Rubaratuka na naibu wake ni Dk Delphine Magere. Wajumbe hao ni Malata Pascal, Dk Jabiri Bakari, Masanja Kadogosa, Jayne Nyimbo, Mhandisi Ephrem Kirenga na Eric Hamissi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Bandari.

Aidha, ameitaka PCCB kuchunguza bodi hizo kwa kile kinachoendelea bandarini na kuwachukulia hatua waliohusika na upotevu wa fedha uliotajwa katika ripoti hiyo.

"Mkurugenzi, PCCB nakuagiza uchukue hatua dhidi ya watu hawa haraka iwezekanavyo na kama hakuna taarifa nitakupa maelezo ya kilichotokea hapa," alisema Rais Samia.

Alisema mifumo ya malipo bandarini kwa muda mrefu imekuwa ikiendeshwa na watumishi jambo ambalo linaonesha kuwa mizigo imekuwa ikilipiwa langoni lakini kwa maana halisi si kweli inasababisha upotevu wa mapato kwa nchi.

Alitoa wito kwa shirika la kupambana na rushwa kuja na majibu ya kwa nini yote haya yanatokea bado bodi na wafanyakazi waliohusika bado wako ofisini.

Pia aligusia juu ya idhini ya zabuni bandia na Shirika la Usafirishaji, huku akijua kuwa vigezo sahihi havikufuatwa na bodi ilihusika katika idhini na serikali ilikuja tu kujua baada ya kutuma watu nchini Uturuki kuchunguza kampuni hiyo.

Alimtaka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuchukua hatua za haraka na endapo atashindwa, anapaswa kumjulisha ili kuchukua hatua zinazohitajika ikiwa ni pamoja na kumteua waziri mpya.

Chanzo: Tanzania: President Samia Dissolves Tanzania Ports Authority, Shipping Corporation Boards
si ndio maana wanapiga kelele mpaka wameajiri wa kuwasaidia huku kwenye mitandao ya jamii. We unafikiri ni watanzania wa kawaida walipa kodi ndio wanaopiga kelele humu, kila siku wanaokoteza mauzushi. Ndio haohao wanaona sasa watanyanganywa tonge. Rais wangu akaze mwendo awapuuze hawa wezi na majambazi wa mapato ya nchi yetu. Sasa hivi wezi ndio wanajifanya wazalendo zaidi. Shughuli za bandari lazima zibinafsishwe ili tupate kuona matunda km nchi siyo watu wachache, wao waendelee kuhonga watashtukia pesa za kuhonga zimeisha na DP World ndani ya nyumba
 
Yote hayo yanajulikana na tumekuwa tukiyapigia sana kelele kwa miaka mingi. Tunavyombo vya kiuchunguzi, tuna vyokbo vya usalama, tuna uongozi tuna kila kitu lakini bado yote hayo yamefanyika mbele ya vyote hivyo.
Suluhu ya hayo haikua kuletewa mapendekezo ya kipumbavu vile utadhani nchi ni ya mazezeta.
we ndio zezeta, uamuzi na direction anayoichukua rais ndio mwarobaini
 
Wewe una haki ya kufikiri upendacho. Lakini ukweli ni huo. Tena hayo ni machache sana.

Jiulize, kwanini mwaka huu tumeweza kuipiku bandari ya Mombasa kwa wingi wa mizigo kuliko miaka yote ya nyuma?

Nini kilikuwa kinafanyika?
Usiwe kama mtu ambaye hafahamu kinachoendelea ni kipi usichojua kuhusu kuongezwa kwa kina cha bahari ili kuruhusu meli kubwa kutia nanga?? Matrilioni yamewekezwa na serikali sio Ticts wala hao DP ili kuongeza kina kuwezesha meli kubwa kupakua mizigo yake
 
Yakiwekwa wazi yatawaumbua wenyewe.

Nchi hii ni ya ajabu Sana mtu ambaye anasimama Jukwaani na kuhamasisha ulipaji Kodi ndiyo anakuwa wa kwanza kukwepa Kodi.

Vigogo wa Chama na Serikali ndiyo wanao ongoza kuua Bandari yetu kwa kupitisha Makontena bila kulipa Kodi.
Umenikumbusha vile vigari vilivyogeuzwa kuwa ambulence eti viliokotwa bandarini..!! Inasemekana PM alikuwa na mkono wake, na ndiyo maana yakaishia hewani
 
Swwali zuri sana, hayo ndiyo yakuwauliza waliopewa amri ya kuchukuwa hatua.

Hii vita siyo ndogo lama mnavyodhania.

duh sasa kiongozi umetoa amri, na hakuna aliyetekeleza hiyo amri, ina maana kuna watu wanamiguvu kuliko Rais.
 
Yakiwekwa wazi yatawaumbua wenyewe.

Nchi hii ni ya ajabu Sana mtu ambaye anasimama Jukwaani na kuhamasisha ulipaji Kodi ndiyo anakuwa wa kwanza kukwepa Kodi.

Vigogo wa Chama na Serikali ndiyo wanao ongoza kuua Bandari yetu kwa kupitisha Makontena bila kulipa Kodi.
Pale amejaza wazanzibar wenzake ataweza kuwachukulia?
 
Back
Top Bottom