Kipindi cha awamu ya tano Mheshimiwa Raisi Magufuli alipiga marufuku sana ya maduka yaliyo nje ya hospitali za serikali, kwani ilionekana kuwa hayo maduka ndo chanzo cha Kukosekana dawa ndani ya hospitali hizi za serikali.
Wengi tulishuhudia huduma nzuri pamoja na upatikanaji wa dawa ndani ya hospitali lakini leo mambo yamejirudia pale pale.
Leo hii Mwananchi wa kawaida anaona ni bora akapate huduma katika Hospitali binafsi kuliko ya serikali kutokana na huduma mbovu zitolewazo katika Hospitali za umma.
Ndani ya hospitali za serikali mara nyingi utapimwa vipimo lakini baada ya majibu kuja utaandikiwa paracetamol na dawa nyingine utaambiwa kanunue duka lililopo nje ya geti.
Kwa upande wa kina mama wanaojifungua tunaambiwa ni bure lakini Hospital nyingi za umma huwa wanalipishwa, huku wajawazito wakiamriwa waje na vifaa vya kujifungulia kama vile pamba. Gloves nk.
Wizara ya afya wafuatilie na pia wawe wakali maana Hospitali za umma zimekuwa changamoto sana kwa wananchi wa kawaida.
Kabla ya malalamiko yoyote twende tukajifunze mfumo wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kwenye hospital zetu na control system yake. Ni nani anahysika na mnyororo mzima. Bajeti ni kiasi gani na inatolewa kiasi gani?
Msisikie hoyahoya huko nje na kusema ilikuwa hali nzuri, bali watu walizimwa kusema. Ulikuwa unawekewa kaa la moto mdomoni lakini unatakiwa useme ni mkate.
Tutafakari pia kwenye:
1: Elimu
2: Afya
3: Ujenzi
4: Sheria
5: Kilimo
6: Biashara ie Bank
7: Mawasiliano ie. Simu
Ni wapi serikali inafanya na kuishinda sekta binafsi kwa ujumla kwenye nchi hii? Haya mambo yanahitaji kushirikiana na kwekeana mazingira mwafaka.
Vitu vya serikali huwa vinaelea hapo kati kutokana na kubeba jukumu la kutoa huduma zaidi kuliko biashara hivyo kuhitaji imput kubwa. Je serikali inaweza kusustain huo mzigo?? Hapo unahitaji mfumo imara na si mtu imara.
Watu walioko kwenye hizo sekta hawajitumi ipasavyo. Kwani hawategemei moja kwa moja malipo toka pale walipo.
Ni wafanyakazi wangapi wa serikali wana objectives na zinakuwa reviewed kila mwisho wa mwaka na kuulizwa utimizaji wake na kuweka mpya au ndo ile theoretical OPRAS.
Je uliwapa vitendea kazi?
BRN ilifia wapi?? Hata utekelezaji wake ulionekana mzigo kwa serikali kutokana na hitaji lake.
Maduka ya dawa nje ya hospitali ni ya kushukuru, kwa kuwa yanasuppliment deficit kwenye institution hizo. Ukitaka ujue umuhimu wake yafunge yote kwa mwezi mmoja tu.
Kuna wakati watoa huduma ya afya wanagawiana gloves na kukaa nazo mifukoni kutokana na uchache wake, si kwa kupenda. Fikiria mama mmoja anaweza kuhitaji kupimwa mara nne kabla ya kujifungua. Nawe umepewa gloves kumi kwa siku???
Tunasema huduma bure kwa watoto chini ya miaka mitano na wazee, uliza hospitali inayopeleka idadi ya hao watu wanaopata huduma bure na kupewa bujeti yake ili kufidia deficit yake kila mwezi na kupewa hela hiyo kama utaipata. Hili ndilo linalofanya ukifika dirishani unaambiwa kanunue hii dawa ya mtoto au mzee.